Hali si nzuri!Siku moja nilimkuta Daktari mmoja hapo Rufaa Mbeya akadai eti Nina kansa ya tumbo!Akaniandikia dawa nyingi kweli na akaniamuru nirejee baada ya mwezi!Niliporudi sikumkuta niliyemkuta akadai majibu niliyopewa kuwa nina kansa si sahihi!!Akaniandikia kipimo cha OGD!Nikaenda kukipimia Muhimbili kwani rufaa mbeya hakipo!Nilipopimwa Muhimbili wakadai tumboni Nina vidonda ila siyo vidonda vya tumbo daktari kaniandikia dawa za kutumia kwa miezi Tisa!Nimejaribu kutumia hizo dawa ila hakuna nafuu yoyote!