Lengo sikuharibu uzi, ila ni kuonyesha tatizo...
Soon nitakuwekea reference kuanzia picha alizotumia mfano hiyo picha za ya huyo anayedai ni max nitakuwekea alipoitoa.
Amedai kafika eneo iliko hiyo nyumba Lukhovitsy japo yeye hata spelling kakosea ila hata kupiga picha hakupiga kaenda kuchukua picha toka mtandaoni ndiyo kawawekea.
Na hiyo ni guest house inaitwa Distantsiya iko hapo Lukhovitsy.
Na hakuna mtu anaitwa Falz kurbashnov hata utafute google hakuna mtu yoyote aliyewahi tuhumiwa ugaidi kwa hilo jina bali kuna Fazliddin Kurbanov ndiye mwenye scandal ambayo walau inataka kufanana na hii kitu.
Sasa jiulize kwanini hizi story za hawa watu haya majima hayana reference yoyote ina maana stories zao ndizo za siri sana kiasi kwamba huwezi pata redfrence kokote?
Hakuna tukio lolote la kigaidi au gaidi yoyote utakayemskia ukamtafuta mtandaoni usipate habari zake kasoro majina ya huyu mleta mada.
Any way enjoy the story.
Kumbuka siyo kwamba naharibu story ila hii ni forum na forum ni sehemu ambayo people debate na ku debate ni kutofautiana mawazo.