Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jamani mbona mnampa tuhuma za uongo tena...yeye ameleta kile anachokijua kuhusu Shika na sie tumemsikiliza Dr. Shika hivyo na wewe leta nondo kuhusu Dr. Shika kisha wadau tusiojua chochote kuhusu sakata hili tutapima na kuona nani yupo sahihiwe jamaa ni muongo kinoma ngoja niandae details nijekukulipua maana unatufunga sana kamba
La kuchat na kubashorovuAcha ufinyu wa mawazo, sasa group la nini.
Hivi itakua hana kadi ya 'chama cha magamba' kweli...?Mazwazwa wapo wengi humu mkuu, muda wote wanawaza siasa, kila kitu wao ni siasa tu, sasa Dr. Shika na siasa wapi na wapi?
Group la kumjadili Dr Shika!La kuchat na kubashorovu
Afu cjakuambia wewe usidandi mada
Lancefort Ltd ni kampuni iliyosajiliwa nchini Russia miaka kadhaa iliyopita, na kwasasa haifanyi kazi kwa kipindi kirefu baada ya watendaji wake kupotea gafla kwa mazingira ya kutatanisha.
Kutoka mjini Rostov on don napokaa mpaka Moscow ni mwendo mrefu kidogo ambao ni km 1200 na zaidi, kwa mwendo wa trein ni 5hrs,
nimefika mjini moscow na kuanza kuuliza hasa legality ya kampuni hiyo ndani ya moscow na Urusi kwa ujumla, nimefanikiwa kupata maelekezo ya kukutana na Mtanzania mmoja anaisha mtaa wa Tverskaya Street, ambaye kanikaribisha na kuanza kufanya uchunguzi wangu, nikaamua kwanza nipate hifadhi ndani ya hotel ya Sputnik.
Baada ya kwenda kwa watanzania wanaoishi huku nimegundua huyu mzee alipata matatizo kwa kuhisiwa ni spy wa Marekani, ambaye kapandikizwa kutokea Afrika, na amekuwa akitafutwa na kufuatiliwa nyendo zake zote kuanzia kwenye kampuni yake na nyumbani alipokuwa anaishi.
Mke wake bi Luisa Kvonkov ndo alibanwa na kueleza kwao ni Tanzania Magu, Lakini inasemekana kwamba kuna kampuni kubwa la kimarekani aidha shirika la upelelezi ambalo liko nyuma ya kampuni ya Lancefort, ndio chanzo cha kutiwa msuko suko uko alikokuwa anamiliki kampuni hiyo.
Shirika la Lancerfort limekuwa likimiliki asset kubwa nchini urusi na kwingineko duniani wakati chanzo cha hela yao hakijulikani, hivyo moja kwa moja kuhisiwa ni miongoni mwa mashirika ma spy ambao wafadhili wake ni wamarekani ambao wana uhasama wa mda mrefu na Urusi.
Wametelekeza mali nyingi kukiwemo na private jets na magari ya thamani.
Kupitia wapelelezi wa ndani ya urusi ambao walilichunguza shirika ambalo inasemekana rais wake ni Dr Luis Shika kwa kipindi kile, waligundua mawasiliano ya karibu na baadhi ya mashirika yafuatayo AMNESTY INTERNATIONAL, CIA, FBI , HGRE, OKLE, ambayo mara nyingi huwa ni waanzilishi wa upelelezi katiKa nchi nyingi,
Baada ya kugundua hayo walitekwa na kuwekwa mateka na wawili kuuwawa, mmoja wapo akiwa mkenya Edward Koinange na mwingine wa Siera Leone Yunusu AKhbu, Na wawili kukimbilia Tanzania lakini Rais wao akapelekwa hospitali baada ya kuwatoroka akiwa ameumizwa vibaya, hakutibiwa Urusi alitoroshwa kinyemela mpaka mjini Dnipro Ukraine, na kutoroshewa Tanzania,
Baada ya kufika Tanzania hakuenda moja kwa moja kwao akajificha mjini Dar es salaam, (Haya ni maelezo kwa mujibu wa mtu wake wa karibu)
Baadae kutorokea Uhispania Mjini Malaga , amekaa malaga miez 8 Na kurudi Tanzania,
Mwaka 2012 wakaidhinisha malipo kutoka marekani ambayo bado yapo kwenye mlolongo wa
kukamilisha mchakato,
WITO KWA BALOZI ZETU TUNAOMBA MUWASAIDIE HAWA WATANZANIA WANAOKUWA NA MATATIZO MUWASAIDIE
Tukiachana na Shika wapo watanzania wengi wanaokosa msaada wa karibu sana kutoka Kwa balozi zetu hizi ,
Ukisoma ukatafakari haitadhuru
Tufanye nimemaliza
KUNA MENGI SITAYAANDIKA HAPA KUTOKANA NA KUJUA KWAMBA KUMBE HII ISHU NI CRUCIAL , NA KULINDA USALAMA WA DR,
PIA YATAENDELEA KUWA KUMBUKUMBU ZANGU NA KUZIPELEKA MAALI ZITAITAJIKA KWA KUMSAIDIA DR,
USIKURUPUKE KUKOPI HABARI HII, MAANA CODES ZOTE NINAZO MIMI UTASHINDWA KUITETEA,MTU PEKEE MWENYE UWEZO WA KUWEKA EVIDENCE NI MIMI, IKITOKEA UKAKOPI SEMA UMEITOA WAPI,
Britanicca
![]()
=============Muendelezo=========
Kurbashnov Max Ni Kijana mwenye Umri wa miaka 34, ambaye ni mdogo wa Bwana Falz kurbashnov ambao wote walikuwa wameshaanza kujitambua mwaka 2001 na kujua kilichoendelea baina ya baba yao na Dr Luis Shikamwanafunzi aliyetokea Africa Akitaka kuwekeza wakati akisoma, nimekutana naye baada ya kuuliza ni kina nani walikuwa na hisa katika kampuni ya Lanceford na kupelekwa moja kwa moja kwa kijana ambaye baba yake alikuwa na hisa,
ambaye kanipa mkasa mzima ulivyoenda mpaka familia yake kuhusika kwenye Biashara hiyo na kuingia matatizoni, aeleza uhusiano wa Shika na kikosi cha marekani.
Anaanza
"Mara ya mwanzo walikutana na Baba yetu bwana Kurbashnov katika mgahawa unaoitwa Istoriya unaopatikana,Verkhnyaya Krasnoselskaya ulitsa, Krasnoselsky, 107140 Moscow,
''Baba yetu alipenda sana uwekezaji hasa kujificha nyuma ya wawekezaji kutoka nje ya Urrusi ni jambo ambalo lilimfanya kila anapokutana na mtu anayeonekana kutoka nje ya Rusia lazima amuulize juu ya Fursa za kufanya au kuwekeza kwa kutumia jina la mgeni, maana kwa kipindi kile kulikuwa ni vigumu kuanzisha biashara kwenye sera za kikomunist na ukiangalia ndipo tulikuwa tuna mda mchache tumejitenga katika USSR hivo nchi nyingi zilizojitoa mfano uzerbakistan tunapotokea sisi walikuwa na ushirikiano na Slovenia, na macedonia, ziliona kama zimekosa soko la uwekezaji na wakitaka kurudi hapa walichajiwa hela nyingi kwa kuwakomoa, ndiyo maana warusi wengi waliona ni bora kuwekeza kwa kutumia majina ya wageni ila kwa makubaliano maalumu,''
alielezea bwana kurbashnov Max
Anaendelea:
"Baba yeye ni mbobezi wa masuala ya finance aliyosoma chuo kikuu cha moscow university touro kwahiyo alihisi ni vema kupata mwekezaji ambaye ni mtaalamu wa upande wa finance pia, ila kwa bahati Mbaya Dr shika alionekana kutaka kuwekeza zaidi kwenye chemical na mbolea suala ambalo baba hakulipenda maana watu wa kilimo walipata moja kwa moja msaada toka serikalin hivyo ilikuwa ni ngumu kupata wateja." anaeleza
Anaendelea:
"Baada ya Dr shika kuonekana ana hela kulingana na maelezo ya mzee Shika alikuwa na Russian ruble 2,900,000 ambayo ni sawa na dollars 50,000 za marekani kwa kipindi hicho ambayo ingetosha mtaji mzee wangu akaona ni fursa wangeweza kuchanganya na kupata mtaji mkubwa na hiyo ndo ilikuwa njia iliyomshawish baba yangu kuwekeza kwa kampuni ya mbolea ila aliweka asilimia 25 tu kama jaribio na Dr Shika akaweka 75,"
Baada ya miez kadhaa wakafungua kampuni kwa jina Lancerford ambayo ilikuwa maarufu kwa sababu iliendeshwa na mtu mweusi maana ilikuwa vigumu kupata mweusi anamiliki kampuni wengi wao walikuwa mawazo yao ni kuajiriwa kwenye migahawa kama waiters na kusafisha kama celaners au hotel attendant hata kama ana masters, maana kutokana na ubaguzi wa rangi ilikuwa vigumu kupata kazi za juu"
Kaka yangu Falz kurbashnov akaanza kupata msuko suko kutoka kwa watu wa usalama wakihisi kwamba anatumika na watu wa nje na anapanga mashambulizi ya kigaidi Kutokana na habari hizo kusambaa baba familia nzima ilianza kuyumbbishwa hata miradi yetu ikafungwa na baba mdogo akafungwa jela miaka 10 , baba yangu akakimbia nchi , akabaki Mr shika tu kwenye kampuni ile,
Mama yangu alijuana na afisa mmoja na akataka kufuatilia stahiki za mme wake yaan mzee wetu, lakin afisa mmoja ambaye alimwambia kwamba kuna vijana wameajiriwa katika kampuni ya Lanceford kama maspy wa KGB kujua ni nani hasa mmiliki na amepata wapi hela,mmoja ni muhasibu na mwingine ni wa security,
Baada ya kaka yangu Falz kurbashnov kuajiriwa pale kama mweka hazina msaidizi alisingiziwa kesi akafungwa miaka 20 jela kwa kosa la ugaidi, na kusaidia maspy wa nje,
alifuatwa kazini tulipouliza majirani walisema wameskia akisema kama amekabwa na watu akitamka
“I’m not a terrorist. I’ve never been one,” mbaya zaidi marekani iliweka shinikizo kumfunga jela za kwao kwamba kuna mambo wanayataka toka kwake, ilileta mzozo kidogo lakin baadae wakawekeana masharti na Rusia, urusi nayo ilisema wanamtaka, lakini marekani wakampeleka kwa kubadirishana wafungwa,
Siku wametekeleza ilo tukio ndipo tukaogopa kusogelea maeneo yale kabisa na baadae kuona ofisi imefungwa Tiyari na hatukumuona Tena Dk shika na tulidhani amekufa maana tumepoteza mawasiliano yake,"
Maeneo ambayo Dr shika alipenda kuyatembelea sana ni pamoja na pirogoviskiy ,Pushkino na nikorina gola uko ndipo walipokuwa wamarekani weusi ambao walikuwa marafiki zake na wengi walikuwa command force ya USA kikosi 32 ambacho ni kikosi cha ushirikiano na russia kwa wakati uo,
Hayo ndo maelezo ya kurbashnov Max ambaye anaonekana kwenye picha chini
![]()
Nimefanikiwa kufika maeneo yote ya matukio kwanza nimefika eneo ambalo kulikuwa na office ile bameshabomolewa na kujengwa nyumba nyinginezo
Pili, Eneo ambalo limesemekana alitekwa nimefika lhukovisty nje ya mji wa moscow na kupaona ila liyetuonesha hakusema ndipo alipata mateso dr shika ila ametueleza tukio lililotokea maeneo hayo na muafrica aliyelipotiwa kuwa billionea aliyetekwa na kuwekwa hapo tukaoanisha picha na kuconect dot
Picha yake ni hii:
![]()
Nyumba inasemekana ni ile ile ila imefanyiwa marekebisho mara kadhaa
Imeadaliwa na Britanicca
Acknowledgement muhimu unapokopi plz
Itaendelea baadae na nitasimulia nani alimtorosha na alitumia mbinu zipi, nani anashikiria hela yake na kwanini anaambiwa ailipie bima.
Ninakutana na muhusika kesho Jumatatu asubuhi njema
Haiwezi fahamika tena na Dr. amekwambia hao Polisi walienda kumpekua na walikuta na bank statement ya Kampuni yao sijui ya Dr which had alot of Money... na wakaondoka nayo na baada ya kukukotoa amesema the statement tu kwenye akaunti moja ilikuwa na hela equivalent na 20 Billion na akasema TRA wanted only 3Bill plus sasa kwa nini tunaendelea kujiuliza muonekano wake na ukweli wa kazi yake.
Pia kwenye mahojiano amesema aliweza kuwatoroka watekaji japo aliteswa sana .. Kwa aina ya uteswaji aliofanyiwa mtu pekee ambaye anaweza kutoroka ni Mtu mwenye mafunzo ya hali ya juu ambayo Dr ameyapitia. kwa hiyo na ukiangalia anavyoongea yupe well organized na anaakili zake zote timamu na kwa utani tu aliwatania kuwa Kapuku kwa lengo la kuwakejeli.
Maisha ya Spy siyo Maisha ya akina Bashite .. Spy wa kweli hajikwezi , na moja ya sifa kuu zao hawapendi kupitwa na taarifa yoyote na kama umemsikia na kufuatilia mienendo yake yeye na kijiwe cheenye magazeti ni uji na Mgonjwa. Bado kuna watu wenye vichwa ngumu kwenye hiloo.....
Hiyo ni hazina tosha ambayo Nyerere pekee ndiye anayejua thamani yake ila sisi wachumia tumbo tutaendelea kuwaza na kumuwaza na kumuwazua kwa kuwa hatujui misingi ya Usalama wa Taifa
Mmmh kwa hili bado sijashawishika...yaaani hiyo pc imepigwa mwaka gani kukiwa na aina hizi za mavazi na umri wake inamaana amezeeka hivi karibuni.Dr Shika enzi hizo Urusi![]()
Jamani huyu sio Dokta Shika ni feki msibabaike naye ,Dk Shika original namfahamu.Mmmh kwa hili bado sijashawishika...yaaani hiyo pc imepigwa mwaka gani kukiwa na aina hizi za mavazi na umri wake inamaana amezeeka hivi karibuni.
Unless hii pc iwe ni ya kijana wake but hatuwezi kumeza kila kitu NOUU
Kabisa, lazima ilo lizingatiweMkuu risk na gharama unazopata jamii forum inatakiwa ikutetee iwapo mtu akachukua hii habari na kuipublish ktk aina yoyote ile
Mwendelezo Lin kiongoziKabisa, lazima ilo lizingatiwe
Inamuhusu shikaHii story kaandika Dr. Shika mwenyewe au? Kama tamthilia vile duuh
Mwendelezo unakuja soonMwendelezo Lin kiongozi
Inamuhusu shika
Poa Mr shikaMwendelezo unakuja soon
Poa Mr shika