Sasa hapo ndipo penye utata..
Kwa maelezo yenu shika aliwahi kuwa mmiliki wa kampuni kubwa yenye private jets, assett n.k.
Hivi ni kampuni gani iliwahi kuwa kubwa ambayo zaidi ya tovuti mfu hakuna reference nyingine ya habari yake?
Watu wanaodai kuwa walikuwa wapambe/wenzake wake according na mleta thread wengine walikamatwa kwa makosa ya ugaidi.. hiyo ni story ya kukamatwa kwa kosa la ugaidi ukafungwa miaka 20, lazima huyo mtu habari zake ziwepo mtandaoni.
Yani there is no way kwa haya matukio na uwezo tunaoaminishwa wa hawa watu kusiwepo references zao.
Mimi ukinikosa kawaida sina tukio lolote kubwa lakini leo hii nikamatwe kwa kosa la ugaidi, references zangu zitakuwa kila mahali nimekupa mfano wa yule kijana mzenj aliyekamatwa kwa ugaidi akapelekwa Marekani ambapo mama yake mpaka leo analia hajui mwanae nini kinaendelea.
Sikatai kuwa Dr aliwahi ishi Urusi, lakini kuna mambo mengi yameongezwa chumvi..