Hongera kuwakumbusha Vijana wenzako walio chini ya miaka 30 kuhusu kujipanga kabla ama baada ya kufikisha umri huo.
Kwa sisi tuliozaliwa zamani, mfumo wetu wa maisha ulituandaa kujitegemea mara baada ya Kubalehe.
Mfano binafsi nilianza maisha ya kujitemegea mara baada ya kuhitimu kidato cha nne.
Kwahiyo hadi nahitimu Shahada yangu ya kwanza tayari kichwani nilishakuwa na Elimu ya kujitegemea maana tayari nilishaanza kuwekeza kweli Kilimo na biashara.
Hadi nafikisha miaka 30 tayari nilishakuwa na familia yenye mke na watoto 2 huku nikiwa nimefanikiwa Kujenga na kumiliki usafiri ambao, kwa maisha ya sasa limekuwa ni hitaji la muhimu la Vijana wengi.
Jambo la kuzingatia kama alivyosema mtoa mada, ni kujiepusha na URAIBU wa Pombe, Madawa ya Kulevya, Kamali, Wanawake n.k huku mkiwekeza muda mwingi kwenye Kufanya kazi kwa Bidii na maarifa.
Hongereni kwenye kutimiza Umri huo wa miaka 30.