Umri huo ni wa kujiwekeza kweli kweli, iwe kiuchumi au kielimu. Una plan za kuwa daktari kama kina Musukuma then it's high time uende shule ukamalizie ukichotaka kufanya.
Ni umri wa kuanza/kumaliza mambo ya uzazi, kama ukichelewa kwenye 20s hukupata watoto, ndio mda pekee ulionao wa kuwatafuta.
Kiuchumi, aisee here is where unatakiwa kupigana kiume kabisa, kibongo hapa uwe na walau kiwanja, yaani kiwepo na uanze ujenzi kabla majukumu ya malezi/elimu hayajakutinga. Ni ngumu sana kujenga ukiwa na watoto huko "yellow-bus-schools".
Ukifika 40s uwekezaji uwe unaonyesha matunda, yaani kama ni ajira basi ipo na ya uhakika, kama ni investment zipo na zinatija coz ukichelewa hapo it will be almost too late to regroup yourself, utaishia kulaumu, kuomba siku zirudi nyuma ili ufix baadhi ya mambo.
Bahati mbaya sana, 20s naona wengi wa vijana wapo tu, yaani kijana yupo 26 anajiona bado mdogo sana, tena binti anakuambia kabisa yeye bado mdogo...dadeq!