Baada ya kufiwa na ndugu yangu ndiyo nimegundua Tanzania tunachemka


Pole sana mkuu.

Wengi wamekaa ki mkuki kwa nguruwe. Unayoyasema hayako mbali na hapa:

Kwako Rais Magufuli sasa pasipo na kupepesa maneno: Kwa unavyoshughulika na Corona sasa - NO! - JamiiForums

Inafikirisha kwa mheshimiwa rais kutelekeza watu wake kufa kwa tamaa ya kuhami uchumi.
 
Wewe unataka je kama kujifungia si unaruhusiwa wewe na familia yako,mbona unajifanya unawahurumia sana watu wengine?
Pole sana kwa msiba uliowafika, kwa kifupi huwezi kujua namna hili janga linavyochukuliwa poa na madhara yake yanaumiza sana, huwezi kuelewa mpaka litakapofika kwa watu wako wa karibu.


R.I.P Ndugu Yetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
pole sana, huu ugonjwa sasa utakuwa umeshasambaa sana. kama Kenya wanakaribia 800 je hapa kwetu patakuwaje?. Nchi za wenzetu wanataka sana kujua idadi ya wagonjwa hapa TZ kwa lengo moja tu. ni kulinganisha na nchi zilizo lockdown kama kenya halafu wapime waone nani zaidi? ila wakuu wameshagundua hiyo kitu....hapo ndio pagumu
 
Pole sana mkuu,endelea kuchukuwa tahadhari,siyo watu wote wenye maambukizi wanaugua.
 
Hiyo habari ya maabara sijui "mashine mbovu" kiuhalisia ni cover tu ila lengo hasa na nia ni kutotangaza chochote kama alivyoshauri Mwigulu.

Kauli nyingi za Mhe akiwa Chato ndo zimelitoa taifa kwenye reli juu ya haya mapambano.
 
Hiyo habari ya maabara sijui "mashine mbovu" kiuhalisia ni cover tu ila lengo hasa na nia ni kutotangaza chochote kama alivyoshauri Mwigulu.

Kauli nyingi za Mhe akiwa Chato ndo zimelitoa taifa kwenye reli juu ya haya mapambano.
True,yaani aliongea tu bila ya kujua anafifisha mapambano..

Kila mtu atumie akili yake ajilinde aisee
 
Morogoro hospital (jina kapuni) nurse alifariki kwa corona just few weeks past na ilijulikana ni Corona baada ya vipimo kurudi vikiwa positive na tayari akiwa ameshazikwa. Eneo hilo kila siku wanazika na idadi ya waliokufa bado ni hiyo hiyo 16

Pili rafiki yangu kaka yake alikuwa France na kurudi Tanzania akiwa hana dalili za Corona,wamemuweka karantini siku 14 na kumruhusu kwenda nyumbani,amefika siku chake akabanwa na kifua (matatizo ya kupumua),homa na kichwa nae tumezika idadi iko palepale 16!! Acheni kutupeleka kama Karne ya 17 buana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo habari ya maabara sijui "mashine mbovu" kiuhalisia ni cover tu ila lengo hasa na nia ni kutotangaza chochote kama alivyoshauri Mwigulu.

Kauli nyingi za Mhe akiwa Chato ndo zimelitoa taifa kwenye reli juu ya haya mapambano.
Vifo vilivyotokea mapaka sasa vingi vingeweza kuzuilika kama serikali ingechukuwa hatua kama nchi nyingine. Na mbaya zaidi baada ya kuona watu wanafariki kwa wingi wakaamua kuingilia upimaji ili kuficha mambo.

Najua watanzania wengi tuu waoga na ndiyo maana wanafanya hivi. Lakini ogopa watu wanaodhulumiwa lakini hawaongei.

Mwisho wake kuna siku utafika na hawa watalawa hawataamini jinsi watakavyoishia vibaya. Roho zinazopotea kwa uzembe na ukaidi wa kiongozi mmoja zitalia kwenye ardhi ya nchi hii.
 
Uzuri wa hili janga halichagui wakupitanae,,, awe kiongozi, tajiri, masikini, chadema, ccm,mchawi, mganga, mwenye kifua kama tembo n.k.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…