Baada ya kufiwa na ndugu yangu ndiyo nimegundua Tanzania tunachemka

Akiwa kama Amir Jeshi Mkuu, Rais alipaswa kutupatia takwimu za maambukizi na vifo kila siku, kutoa muongozo wa kujikinga pia kutufariji raia wake.
hakuna faraja katika kujua idadi ya maambukizi,labda mna ajenda zenu kisiasa,hata kauli yako inakinzana.maana utachukua muongozo baada ya kuogopa.

nadhani muungane sasa na watanzania wanaoitakia mema nchi kwa ku campaign njia bora za kujikinga,badala mara mmekimbia bungeni,mara mlilie lockdown.mtaonekana matapeli zaidi.
 
Pole kwa msiba ndugu.
Lakini naona unalalamika vipimio vipimo kwani ukipimwa ndo unapona corona.

Tuendelee kuchukua tahadhari na kujitibu kwa njia mbadala
utadhania ndugu yake angepona kwa vipimo.
 
nadhani wewe ndio ungekaa kimya.kama corona imekuja kuwa kirusi katika maisha yetu ya lazima,ulitegemea rais afunge kazi halafu ule mablanket ndani??
 
Ukiguswa na msiba wa corona ndiyo utaona machungu ya
Weka cheti cha kifo kuthibitisha kama marehemu alikufa kwa corona
Acheni kujitisha,si kila kifo ni corona
Inawezekana ni homa ya mapafu (pneumonia),homa ya ini Hapetitis B,au shambio la moyo yote hayo yanaua kwa changamoto za kupumua
Watu tupp bize na corona,tunasahau homa ya ini,nayo inaua fasta
 
Andika majina yao acha porojo wewe wa Kwanza kufiwa ? hata ukifiwa toa taarifa za wazi na kweli sio za kutunga
Una laana mkuu, nilitaka nikae kimya wacha niongee. Usituongezee machungu nimepoteza marafiki wawili last week yaani kwa interval ya siku 3 tu. Kuwa na utu japo kwa kipindi hiki basi. Nimejilockdown kwa muda sasa sasa pengine na mimi ningekuwa kama wao kwani tulikuwa very close. Si lazima upinge kila kitu mkuu.
 
tuwekee vyeti vyao vya vifo vinavyoonyesha wamekufa kwa corona tukuamini vinginevyo Wewe ni mwongo tu kama waongo wengine ila wako umekubuhu kwa kuwa unapitia kwenye kusingizia vifo hewa
 
tuwekee vyeti vyao vya vifo vinavyoonyesha wamekufa kwa corona tukuamini vinginevyo Wewe ni mwongo tu kama waongo wengine ila wako umekubuhu kwa kuwa unapitia kwenye kusingizia vifo hewa
Hivi wewe kiazi mtu anapata faida gani kusingizia kifo? hivi kichwani kwako upo sawa kweli wewe
 
Hivi kwani hata akipimwa na kutest positive unafikiri kuna dawa??

Unafikiri hata nyie mkipima mtapata matumaini?

Anyway malalamiko mengine hayana maana.....mi naona ile mashine haina maana ni kutoa tu data zinazotisha watu ila dawa hatuna....wee ukiona dalili piga tiba lishe zilizoshauriwa....piga nyungu maisha yaendelee
Sent using Jamii Forums mobile app
 
tuwekee vyeti vyao vya vifo vinavyoonyesha wamekufa kwa corona tukuamini vinginevyo Wewe ni mwongo tu kama waongo wengine ila wako umekubuhu kwa kuwa unapitia kwenye kusingizia vifo hewa
Mungu akusamehe mkuu, kwa heri na endelea na kazi yako.
 
Hivi wewe kiazi mtu anapata faida gani kusingizia kifo? hivi kichwani kwako upo sawa kweli wewe
Hatutaki porojo aweke vyeti vyao vya vifo hapa tuvione asituletee misiba hewa ya corona isiyo na ushahidi wowote?

kwa hiyo tumuamini tu hewani kuwa nduguze wamekufa kwa corona tuanze kumpa pole hewa za vifo hewa?


Haya ngoja basi nimpe pole hewa

Mleta mada nakupa pole hewa kwa Vifo hewa vya ndugu zako hewa vilivyosababishwa na ugonjwa Wa corona hewa na kuzikwa kwenye makaburi hewa

Nakutakia uwe na matumaini hewa katika kipindi hiki kigumu hewa cha kuondokewa na wapendwa wako hewa
 
Achukue tahadhari gani kwa mfano.
Amekwambia huyo ndugu yake ameupatia kazini na asingekuwa na maamuzi ya kulala tu asiende kazini atakula nini.
Tahadhari tunachukua kwa kadri ya uwezo wetu lakini kuna vitu vingine havikwepeki.
Kwa mfano kama hivyo umepata msiba na hauna usafiri binafsi itakulazimu upande basi hadi mkoa mwingine na ukishuka kama ndugu zako hawana gari binafsi itakulazimu upande daladala kama unapokwenda ni nje ya mjini.
Unadhani kwa kesi hii utanusurika kirahisi kwa kunawa maji tiririka na sabuni au kwa kuvaa tu barakoa halafu unakuta abiria wenzako hawajavaa barakoa?
Ndugu zangu watanzania tujifunze kuthink beyond na kuchekecha mambo.
Sasa wewe kila siku unaambiwa chukua tahadhali corona inaua unafikiri wanatania?



Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
akikuletea vyeti utafaidi nini wewe, au utamsaidiaje! Unafikiri pole yako ina msaada gani kwake kwa sasa, by the way lengo lake siyo kupewa pole bali kuelezea hali halisi aliyopitia kuhusiana na msiba wa ndugu yake, Period
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…