OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Baada ya Yanga kumficha ndani mshambuliaji hatari Kambole kwa miezi 4 hatimaye leo ameachiwa kutoka nje.
Kambole amekuwa akifungiwa ndani huko Avic Town Kigamboni ili kuficha aibu ya siasa za usajili.
Huyu ni mchezaji aliyetajwa kuachwa na Yanga baada ya idadi ya wachezaji wa kigeni kuzidi kufuatia usajili wa Kisinda.
TFF ilihalalisha kucheza kwa Kisinda Yanga ikiwa ni uamuzi wa kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji ya TFF.
Tuliambiwa hilo lilitimia baada ya kumpeleka kwa mkopo Kambole katika timu ya Wakiso Giants nchini Uganda na ITC yake ilitumwa huko na sio Yanga tena.
Kumbe haikuwa kweli mchezaji huyo alifichwa kambini ili asionekane hadharani kukwepa aibu.
Lakini hayimaye leo ametoka nje