Baada ya kufungiwa ndani miezi 4, Yanga yamtoa nje Kambole

Baada ya kufungiwa ndani miezi 4, Yanga yamtoa nje Kambole

Kwa hiyo umefurahi, au umenuna? Chagua kimojawapo kati ya hivyo viwili.
Sometime tutumie akili kidogo siyo ushabiki ndo haya haya ya Morrison, Fei Toto. Tukatae huu Upuuzi. Maana mashabiki sasa tunakuwa kama mandondocha. Mnafanya Haji atambe kuwa alisema kweli wenye akili wawili tu.
 
Shida iko wapi mkurugenzi kwa huyo mchezaji kubakia Avic Town na wenzake? Alisajiliwa kwa lengo la kuisaidia timu. Bahati mbaya akapata majeraha! Na sasa amepona, na hivyo benchi la ufundi limeona apewe nafasi nyingine.

Halafu huyo Haji Manara unayempa kiki, ni nani hasa katika maisha yetu ya kila siku? Au unavutiwa na ule mdomo wake mchafu, na usiochuja maneno ya kuzungumza?

Don't complicate things. Life is too short.
Usiongee kama simba. Manara ni msemaji wetu sema tu ameweka figisu figisu. Mheshimu huwez mlinganisha na wewe hata kidogo. Mchango wa manara kwetu ni mkubwa na tumeuona. Wewe una changia nini yanga?
 
Haya, ameshatoka kula hayo mapumba na unga! Mjiandae sasa kwa maumivu na vilio.

Maana unaambiwa yule Mayele anaye watetemesha kila siku, ni cha mtoto kwa huyo Kambole.
Utajua mwenyewe na fingo lenu
 
Usiongee kama simba. Manara ni msemaji wetu sema tu ameweka figisu figisu. Mheshimu huwez mlinganisha na wewe hata kidogo. Mchango wa manara kwetu ni mkubwa na tumeuona. Wewe una changia nini yanga?
Manara siyo msemaji wa Yanga. Kama bado ni msemaji, na Ali Kamwe ni nani pale Yanga? Na kiufupi Manara alikuwa ni mwajiriwa tu wa GSM. Hivyo hana mchango wowote ule kwa Yanga kama Yanga! isipokuwa GSM na biashara yake kwa ujumla.

Kuhusu kuchangia Yanga; kiufupi ninachangia vingi tu. Tena kuliko huyo Popoma Manara.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
We jamaa unapata wapi ujasiri wa kumponda Manara hivyo? GSM si ndo Yanga yenyewe? Yaani unataka kusema wachezaji waliosajiriwa na GSM hawahusiki na Yanga?

Au wewe ni Mkia unajidai Yanga? Mbona unataka kutuvuruga? Manara kakiri mwenyewe anaipenda Yanga toka kitambo na tumembeba sisi, amekuwa akitusemea team yetu kabla ya figisu. Wanayanga wanamsikiliza sana manara wewe nani wewe pale yanga?

Acha hizo usije ukajilinganisha na manara hata kidogo. Huyu ameibadili yanga sana tu.
 
Mmejiandaa lakini kwa maumivu? Maana huyo Mayele anayewatesa kila siku, ni cha mtoto kwa Kambole. Imagine yule Moses Phiri wenu, akimuona Lazarus Kambole, mwili unaishiwa nguvu.
Misimu 4 ana goal 1 ndo amsumbue mosses phiri
Shida yenu kubwa mnajitoa ufahamu sababu ya mwiko huko nyuma
 
Aibu iko wapi! Kuna watu mnapenda kukuza mambo mpaka basi.
Tatizo kubwa ni ajira na ukosefu wa pesa, ukiona kijana kazi yake ni utimu asubuhi mpk usiku ujue maisha yake magumu. Sehem pekee inayompa furaha ni kukashfu na kutusi wengine
 
Mmejiandaa lakini kwa maumivu? Maana huyo Mayele anayewatesa kila siku, ni cha mtoto kwa Kambole. Imagine yule Moses Phiri wenu, akimuona Lazarus Kambole, mwili unaishiwa nguvu.
Kambole yule aliyecheza jana na KMKM au mwingine?Unajua ukikosa mwanga wa jua kwa muda mrefu akili zinafumbaa.Kukaa darini sio mchezo.
TFF inalinda sana ujinga.
 
Kambole yule aliyecheza jana na KMKM au mwingine?Unajua ukikosa mwanga wa jua kwa muda mrefu akili zinafumbaa.Kukaa darini sio mchezo.
TFF inalinda sana ujinga.
Kwa Kambole yule wa jana, naomba tu kufuta kauli yangu.
 
Back
Top Bottom