Kama kuna mambo yanakera na kuumiza ni kumuita mwanamke Malaya! Ndugu zetu wa CCM baada ya kuzidiwa points wameamua kuhamia kwenye matusi.
Huyu ni Mwakilishi wa CCM ngazi ya Wilaya huko Tarime akimuita Esther Matiko kama Malaya, kwakua huyu ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya tunaamini anachoongea ndio msimamo wa CCM Taifa kuwa CCM siku hizi wanawachukulia wanawake kama Malaya.
Cha kushangaza hutasikia NEC wakikemea jambo hili, hutasikia CWT wakikemea jambo hili, hutasikia hata Polisi wakikemea jambo hili.
Nawaomba wanawake wote, kwa umoja wenu, kataeni kudhalilishwa kisa tu ni kampeni. Utu wenu ni zaidi ya siasa.
Leo ameyasema kwa Matiko, kumbuka kesho itakua wewe, mama yako au wanao kuitwa Malaya.
Nimeweka ni video hapo, credi kwa Maria Tsehai
Kuna mtu alisema nimeweka kipande tu, sasa nimeweka video nzima
Sasa mnapoambiwa CCM kama chama kimelaniwa na utendaji wa maovu yote makubwa na madogo yapo huko, si umeona wale wasanii wanasaminiwa wakati ule tu wanapopafomu, ila ndani ya CCM hawana maana wala thamani hata inayofikia senti ishirini.
Huyuu kada wa CCM anajua ata mama Samia Suluhu Ni mwanamke pia. Mhh!!! kwaiyoo anamaanisha ata yeye. Acha ninyamaze kesi isije hamishiwa kwangu. Maana kunya anye kuku akinya Bata kahara.