FYATU
JF-Expert Member
- Dec 7, 2011
- 5,567
- 4,683
Baada ya mtangazaji maarufu nchini, zamaradi mketema, kujifungua mtoto wa mwingine ,mashabiki wake wamemjia juu mtangazaji huyo na kudai kuwa kitendo cha kuzaa nje ya ndoa ni kosa kwa mtoto wa kiislam kama yeye, kwani kinaonyesha kuwa hakulelewa kwenye maadili mazuri kama dini yake inavyotaka.
Mashabiki hao wamelaani kitendo cha mtangazaji huyo kuendelea kuzaa bila kufunga ndoa, kitendo ambacho watu wamekitafsiri kama uzinifu na uhuni.
Matumizi ya hii sentensi huwa yananikwaza kupita maelezo, laiti soe tungefuata maandiko ya dini zetu dunia ingekuwa mahali salama sana pa kuishi.
Hakuna dini inayoruhusu waamini wake kukiuka maandiko na maelekezo yao, ila ni wazi kuwa awe ni muisilamu au mkristo bado maandiko na maelekezo ya dini husika yamekuwa yanawashinda wafuasi wao na hata kwa viongozi wao..hata hao Masheikh na Wachungaji wamekuwa wakiukaji wakubwa wa miongozo ua dini zao.