Baada ya kukaa kanda ya ziwa kwa miaka 5, nimejifunza yafuatayo

Baada ya kukaa kanda ya ziwa kwa miaka 5, nimejifunza yafuatayo

Kinuju

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2021
Posts
2,386
Reaction score
5,325
Watu wa kanda ya ziwa ni wengi sana nchini na ndiyo maana kila mgombea urais huwa anakimbilia huko kuomba akubalike. Watu wa kanda ya ziwa wanakadiliwa kufikia million 32 kwa mjibu wa sensa ya 2002.

2. Kanda ya ziwa imetawaliwa na kabila la Wasukuma ambao wamejaa mikoa ya Simiyu, Shinyanga, Mwanza, Geita na Tabora. Maeneo yote haya watu wanazungumza lugha ya kisukuma iwe mjini au vijijini.

Nimejifunza kabila la wasukuma ni kama maji usipoyanywa utayaoga.

3. Kanda ya ziwa ni wachapa kazi sana lakini hawana tamaa ya pesa kabisa ukilinganisha na kanda ya Kaskazini na siyo wanafiki kabisa.

Kanda ya ziwa wana msimamo usioyumba kabisa.
 
Sasa kama ulitaka kuwazungumzia wasukuma kwa nini uzunguke zunguke kama mwenye kuharisha!

Wewe ni kati ya wasukuma wabaya. Kanda ya ziwa kuna waTanzania wengi, wakiwemo wasukuma ambao hawana tabia za hovyo kama ulizo nazo wewe, za ukabila.
 
Mwanza ni kitovu cha kanda ya ziwa sasa mikoa ambayo hupokea mwamko kutoka Mwanza ni kama ifuatavyo, Shinyanga, Simiyu, Tabora, Mara, Geita, Kigoma, Kagera na Katavi ukitoka hapo unakuja kumalizia Mbeya, Songwe, Rukwa hizo ndio kanda za uchaguzi kwa mgombea Urais ukiungwa mkono huko tayari maana mikoa hiyo wakishika msimamo ni mmoja.

Dar ni wengi kwa idadi lakini hakuna wapigakura, Lindi na mtwara wao lolote twende hawana msimamo, Iringa, Njombe, Ruvuma mikoa hiyo hua wao ni CCM kwenye Urais japo wakiamua lao ni lao lakini hakuna kura nyingi kama kanda ya ziwa magharibi ambayo kura hua ni nyingi, Kanda ya kati hawa hawawezi kuamua urais, Arusha na kilimanjaro pia hawawezi kuamua Urais kwa sababu ya idadi yao, Zanzibar haina kura za kuamua urais hata iweje

Hivo nakuunga mkono sema kwenye uchaguzi kuna hiyo kanda ya ziwa magharibi ni nyeti mno hao wasipokuunga mkono umekwisha
 
Hiiiiiiiiii Baghosha, Mbona Hawa ma Gwajima wawili hawana msimamo kabisa?

Askofu Gwajima alisema yeye kugombea urais ni kujishusha cheo, yeye ni zaidi ya rais, kwani anamwakilisha/ anauwakilisha ufalme wa mbinguni hapa Tanzania (yeye ni balozi wa Mungu hapa nchini) lakini baada ya muda mfupi akaenda kugombea ubunge Kawe, ambapo kwenye kura za maoni alikula mweleka mbaya Sana, akaangukia pua huko kwenye nafasi ya tatu.

Urafiki wake na mwendazake ukamuokoa.

Alisema yeye alishawahi kuwa Muislam, na jina lake lilikiwa Rashid, lakini akaachana na Uislam akarudi kweny Ukristo, msimamo wa namna gani huu?

Alikuwa mtu wa CHADEMA, Hadi kuweza kumleta LOWASSA ndani ya chama kugombea urais, ghafla akaibukia CCM.

Yule Gwajima daktari alikuwa anakula Hadi mananasi yaliyooza enzi za mwendazake, Leo ameachana na upotolo ule anawasihi watu wachanjwe
 
Roho zao nzuri zinasababisha wahamiaji haram kujifanya wasukuma..
Wanahifadhi wahamiaji haram wengi kanda ya ziwa
Watu wa kanda ya ziwa hatuna roho mbaya, hatuna kinyongo. Halafu pia sisi hatukatai watu. Mtu akikimbilia kwako unampa hifadhi, huwezi kumtupa.

Muhimu zaidi shughuli zetu ni za kilimo na ufugaji hivyo warundi ama warwanda ama wakongo wakija kwetu tunawakaribisha halafu tunawatumia kama wafanyakazi.

Sisi akija mtu kwako hiyo ni neema maana umepata nguvu kazi ya shamba ama kuchunga ng'ombe. Ukatae mtu ili iweje?

Hilo moja, la pili, makabila mengi yaliyoko upande wa nchi nyingine yako pia huku kwetu, Mara mpakani kuna wajaluo na wakurya kenya, kupande huu wa Tanganyika hivyo hivyo. Hivyo unakuta hao ndi ndugu zetu hatuwezi kuwafukuza.

Ukija kagera kama misenyi, Biharamulo, Ngara kote huko ni warundi na warwanda, hawawezi kuwafukuza ndugu zao wa Burundi ama Rwanda wakiwakimbilia. Hata ndugu zetu wa kigoma hivyo hivyo.

Ukiangalia kwa mantiki hiyo ya kupenda labor ndio maana tunazaliana sana kule.
 
Back
Top Bottom