Tangu mwaka Jana unaweka matangazo ya kutafuta waume ila unaambulia patupu...
Nakushauri Dada Yangu punguza masharti.. Weka masharti "Constructive" kwa Mme unaetaka kuwa nae.. Achana na vigezo ambavyo mtu akivisoma anakuona hauna vigezo vya kuwa Mke bora..
Eti unataka mwanaume mweupe !! Sasa weupe una mchango gani kwenye familia yako ? Unataka mwanaume mrefu ! Urefu utapeleka Watoto wenu shule ???...
Ukiendelea na hizi sifa na vigezo vyako utaishiwa kuchezewa na kuachwa ... Andaa na tafuta wanaume wenye vigezo "Jenzi" ..
Habari zenu wanachama wa jf Natafuta mwanaume ambae mungu akitujaria awe mwana ndoa wangu umri kuanzia miaka 27 kuendelea,Awe na kazi yoyote anapenda kujituma maji ya kunde urefu futi 5,Mkiristo awe na mapezi ya dhati Kwa upande wangu sijawai zaa,sijawai olewa, mcheshi na mwenye msimamo thabiti...
www.jamiiforums.com
NB: Kuna wanaume serious wanatafuta watu wa kuoa ila inabidi uwe makini sana kwenye mabandiko unayoandika kutafuta hao wanaume ... Maneno yako machache yanaweza kuwajengea picha jinsi ni mwanamke wa namna gani ulivyo ..