Baada ya kukosa mchumba natafuta mwanaume wa kuzaa nae tu

Baada ya kukosa mchumba natafuta mwanaume wa kuzaa nae tu

Mambo ayo wow!..uko tuendako tunaenda kuoa wanawake ata kumi,.. Mungu ni Mwema!
 
Yaan we humu jf umekuja saka wachuchu naona nyuzi zako zote ni kusaka wachumba haya bana,,,nasubiri uzi wa kusema nataka yeyotee tu ili mradi mwanaume[emoji23][emoji23]
 
Najikuta natamani kuwa kahaba tu kwakuto kupata mwanaume wa kweli naombeni ushauri wenu maana nimesha kata tamaa na hawa wanaume
Tatizo lako limeisha mkuu,hapa hakuna linaloshindikana,utawapata wengi mpaka uwakimbie mwenyewe
 
Najikuta natamani kuwa kahaba tu kwakuto kupata mwanaume wa kweli naombeni ushauri wenu maana nimesha kata tamaa na hawa wanaume
Hebu jaribu na hapa, tatizo ni kwamba tunapishana njia. Naomba usifanye hicho unachowaza, thamani yako ni kubwa mno na bado great future ahead. Niko tayari niwe nawe tu karibu as a friend kwa muda wa 2-3 months naamini utabadilika kabisa na kuwa na sura na mtazamo mpya.
 
Hebu jaribu na hapa, tatizo ni kwamba tunapishana njia. Naomba usifanye hicho unachowaza, thamani yako ni kubwa mno na bado great future ahead. Niko tayari niwe nawe tu karibu as a friend kwa muda wa 2-3 months naamini utabadilika kabisa na kuwa na sura na mtazamo mpya.
Naomba namba
 
Usifanye hivyo dada ,kuwa na subira utapata mwanaume sahihi wa kuwa nae.ukahaba ni uzinzi ni dhambi before God!
 
Ila kuna watu mnashangaza ina maana furaha yako ipo kwa mwanaume? Hebu kua busy na kutafuta hela na maendeleo utampata mwanaume unaemtaka...hao wanaume wenyewe.... siku hizi wanapenda kulelewa....

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahhahahah napita tu mie best

Jesus is my saviour and a friend
 
Najikuta natamani kuwa kahaba tu kwakuto kupata mwanaume wa kweli naombeni ushauri wenu maana nimesha kata tamaa na hawa wanaume
Je wewe ni mwanamke wa kweli!? Usitafute kondoo kwenye kundi la chui.
 
Ukahaba uko moyoni. Kuna watu wakiwa bado wadogo unajua kabisa ataishia kuwa kahaba. Ndo maana kati ya machaguo mengi yaliyopo umeamua kuchagua ukahaba.
 
Tatizo mnachagua weeeee, mara mwenye degree 2, awe ana kipato kisichopungua 10 million kwa mwezi, awe mweupe mrefu,... Sifa Mia nane kidogo.. Looh, utadhani unaumba mwenyewe!... Maisha hayako hivyo, maisha yanatengenezwa na nyie wote wawili,... Unaweza ukapata mume wa hovyo tu, ukamshape mwenyewe na ukamtia moyo na akawa kama umtakavyo......

Soma hii!
Eti wanaume ni Malighafi!

Jamani....

Nikiwa safari kuelekea Nairobi nilifanikiwa kuonana na mama mmoja Mchaga aliyefanikiwa sana. Ana hoteli Arusha, Moshi na pia ana export kahawa.

Nilijiuliza sana huyu mama amewezaje?
Ikabidi nianze kumchimba.

Aliponiambia wanaume ni Malighafi, nilishtuka sana. Nikaomba anidadavulie ....

G: Unasemaje ? Wanaume ni malighafi? Sikuelewi? Una maana gani?

M: Usinielewe vibaya, kwanza inabidi ujue maana ya malighafi. Nadhani unajua malighafi ni nini. Malighafi ni bidhaa inayohitaji kuongezewa thamani ili upate faida zaidi. Au unahitaji kuisindika kabisa ili iwe na thamani kwa faida yako.
Mimi kama mwanamke kwangu mwanaume ni malighafi inayotakiwa kuongezewa thamani kwa faida yangu.

G: Sijakuelewa kabisa mama.

M: Sisi wanawake tuna nguvu isiyo kawaida. Mungu akikupa mwanaume, ni kama malighafi ...unatakiwa kuongeza thamani, kumtengeneza unavyotaka kisha unamtumia kuwa unavyotaka. Mwanamke anaweza kumwamsha mwanaume aliyelala na kumfanya kuwa Rais, au mwanamuziki mkubwa halafu anaweza kumtumia kuwa anavyotaka. Wanawake wa siku hizi, wakipewa mwanaume wanataka awe amekamilika yaani finished product ili wamtumie. Huo ni ujinga. Wanawake tumeumbwa kuhamasisha. Tumeumbwa kumpandisha mwanaume. Mwanaume ni kichwa lakini kwenye familia mwanamke ni moyo.

G: Bado sijakupata kabisa.

M: Ngoja nikupe mfano. Mume wangu mimi alikuwa mwanafunzi wa chuo nilipokutana naye, mlevi na asiyejielewa kabisa. Lakini kuna kitu cha tofauti nilichogundua...alikuwa na akili. Kwangu ilikuwa ni malighafi yenye utajiri. Nikapiga mahesabu yangu, nikaingia kwenye mahusiano. Nikampa anachokitaka akapagawa. Kisha nikashika usukani. Nikatafuta njia akaacha pombe, akawa msomaji sana mpaka akafaulu chuo kikuu. Amemaliza uinjinia, nikampelekesha akanioa. Ninamjua wapi pa kumgusa. Alipomaliza chuo, nikamwambia sitaki awe mwajiriwa akagoma. Uoga. Nikamwacha, mshahara ulipoanza kuingia nilishika mimi .... Nikimpa anatumia pombe. Nikaanza kuchukua akiba yeye bila kujua, nikanunua mashamba, viwanja, nikaanzisha mgahawa. Nikamwita kama mgeni rasmi kuja kuzindua. Nikampeleka kwenye mashamba niliyonunua. Akapagawa. Nikahamisha akili yake yote, kwangu.
Tukaanza kushirikiana pamoja mpaka tukasimamisha hoteli. Mume wangu alikuwa hapendi biashara lakini baada ya kumbadili akapenda biashara kunizidi. Unajua nini kilitokea. Aliacha kazi na kuweka nguvu kwenye hoteli ndogo, tukafanikiwa mpaka hoteli kubwa ikajengwa.

Mashamba zaidi yakanunuliwa. Watoto wetu wanasimamia biashara zetu. Mume wangu ni mpambanaji hatari kwasasa. Unajua kwanini? Kwangu alikuwa ni malighafi, nikaamua kuongeza thamani.

G: Aisee!! Eeh?

M:Wanawake wa siku hizi wanatafuta wanaume walioongezewa thamani, ili wawatumie. Ukiona mwanaume yupo juu fahamu kuna starring nyuma ya pazia aliyesababisha. Mwishoni wanatumika wao kama vyombo vya kujistarehesha na kutupwa. Mwanamke unatakiwa kuwa na akili mara nne ya mwanaume, na usijivune kama una akili. Ukikuta mwanaume ana akili na unajua unaweza kumtengeneza chukua na ongeza thamani.

Ukichukua kilichoongezwa utapigwa tu. Utaachwa.

Mfano kama mimi mchaga nikiolewa na mwanaume ndani ya miaka mitano hamjajenga, asihukumiwe mwanaume. Mwanamke ndiyo kimeo.

Mwanamke ni msababishaji, uliza matajiri wakubwa duniani. Uliza watu wakubwa maarufu, uliza akina Napoleon, uliza akina Obama, uliza akina Albert, uliza utajua....nyuma yao kuna nguvu inayosababisha mambo makubwa.

[emoji124][emoji124][emoji124]USIPOELEWA MWAMBIE MUHUDUMU AONGEZE GLASS .

"Ukifuga njiwa utajua bei ya mtama"
 
Back
Top Bottom