Baada ya kukosa mchumba natafuta mwanaume wa kuzaa nae tu

Baada ya kukosa mchumba natafuta mwanaume wa kuzaa nae tu

Ukisoma kwa pupa thread hii utadhani anatania...
Soma mara tatu au nne kwa utulivu na hisia... Fumba macho na ufumbue Utajua yuko serious au la...
Mi Nimekuelewa... Nitalifanyia kazi
 
Najisikia kulia tuuuuu nimechoka kuwa mpweke
IMG_20180118_165842_433.JPG
 
ngoja niwaambie ukweli wenu ninyi msioolewa,
01.mume unamtengeneza wewe mwenyewe.....mwanamke una hiyo karama ya kutengeneza mume.....tatizo lenu sasa mnataka kumpata mume aliye tengenezwa nani kakutengenezea?
02.wakina dada wengi muda wa kuolewa wao huwa busy either na wasio waowaji au waliotengenezwa na wenzao ambao tayari wana wake. so fursa inapotezwa
03. ukifika muda wa wewe kuwa mke usiwe kama enzymes.....hii ni aina ya mimeng'enyo ambayo ina react katika chakula tutiacho tumboni sifa ya hii midubwana ni kwamba ipo very selective & SPECIFIC so hata ukila mchanganyiko wa chakula yenyewe bana wa wanga ataenda kwenye wanga wa protein ataenda kwenye protein na fat ataenda kwenye fat na ndio hawa dada zetu walivyo wengine wanapenda magali .,wengine starehe viwanja nk nk baadaye mume unamkosa.
 
Najisikia kulia tuuuuu nimechoka kuwa mpweke
Kuna dem flani alikuwa na malalamiko kama yako,ni mzuri tu ...basi nikamfuata tukaanza mahusiano,.

Nilijitahidi kumuonyesha mapenzi yangu ya dhati bila kificho...mara gafla akajisahau akawa na kiburi na jeuri..dah nikajitahidi kumbadilisha lakini wapi..

Mara akawa ananiforce kwenda kujitambulisha kwao,nikamwambia mama subiri kwanza coz bado muda wakufanya hivyo sababu hatuna hata miez minne tangu tujuane.
Hee akabadilika na kuongeza jeuri na kiburi...NIKAPIGA CHINI MAZIMA MPAKA LEO ..Nasikia eti analalamika kwa rafiki yangu et nimemuacha bila sababu.
 
Pole sana muomba Mungu hachoki na usikate tamaa ipo siku utampata mwanaume aliye sahihi kwako hujui Mungu anakuepusha na nini
 
Tatizo mnachagua sana ndo mana hebu weka kwanza picha tuone mana hata nami nina hitaji la mke
 
Duuh pole sana mamii,.watu tunapiga mwaka wa pili sasa teh teh tehee[emoji13]kama ni hitaji lako la msingi kwa sasa huna budi kukaa magoti pa Mungu dia,sugua goti kwelikweli lakini sio unaomba sana huku unaonjwa utachelewa utasikia shuhuda kwa wenzio tuu,.kaa UWEPONI mwa Mungu kwa UAMINIFU hakika nawe utashuhudia.
 
Najisikia kulia tuuuuu nimechoka kuwa mpweke
Kati ya sehemu ambazo niliamini kuwa kuna Mungu ni kwenye hii taasisi ya ndoa. Wakati we unaona Mungu amekuacha ndio wakati wa kumweleza Mungu unahitaji mtu wako, wakati unaona umeachwa na kuwa mpweke ndio wakati wa kushuka chini na kusema Mungu nipe mtu uliemuandaa kwa ajili yangu, take it from me Mungu anakuletea mtu ambae mwenyewe hutoamini, lakini ishara zote atakazokuja nazo huyo mtu ndizo zitakazokwambia "YES, NI YEYE".

Tenga hata siku moja kwa imani umwombe Mungu. Mwambie Mungu uko tayari sasa unamhitaji mwenzako, utaona maajabu. But Forgive and Forget first about all disappointments....
Ni tendo la imani, memorise kama kuna maagano yeyote ulishawahi kufanya.."Fanya Toba".

Siri ni moja tu, Mwombe Mungu kwa imani, Mungu atakuletea mtu wako......
 
Pole Sana Dada...
Ila inaonekana umepoa sana socially, ongeza ushiriki wako katika social activities... Yaani chamgamka.
 
Back
Top Bottom