Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,899
- 10,415
1. Viongozi wote wa tume ya uchaguzi wanatakiwa wachaguliwe na wananchi na wasiwe na chama chochote wala wasihudhurie vikao vya chama chochote wao wafanye kazi yao. Hivyo wajitokeze watu kadhaa kuwania nafasi hizo kisha wapigiwe kura.
2. Spika wa bunge na naibu spika wanatakiwa wachaguliwe na wananchi na wasiwe na chama chochote wala wasihudhurie vikao vya chama chochote. Hivyo wajitokeze watu kadhaa kuwania nafasi hizo kisha wapigiwe kura.
3. Mwanasheria mkuu wa serikali asiwe mbunge wa chama chochote na anatakiwa achaguliwe na wananchi na asiwe na chama chohote wala asihudhurie vikao vya chama chochote. Hivyo wajitokeze watu kadhaa kuwania nafasi hiyo kisha wapigiwe kura.
4. Viongozi wakuu mahakama wasiwe wa chama chochote na wanatakiwa wachaguliwe na wananchi. Hivyo wajitokeze watu kadhaa kuwania nafasi hizo kisha wapigiwe kura.
5. Wananchi tuchague kiongozi wa chama chochote mwenye uwezo wa kufanya maamuzi sahihi tusiangalie anayeweza kuongea mbele za watu. Tusibague vyama ni dalili ya kutokuelimika.
6. Kiongozi mzuri ni yule anayeweza kufanya maamuzi sahihi na sii anayeweza kujieleza zaidi mbele za watu.
7. Watu wanaokula rushwa na kufanya ufisadi akili zao zinafanana na akili za wezi wanao iba mali za watu. Kinachomfanya mtu aibe ni kwasababu ya kutoelimika na mtu aliyeelimika hawezi iba kitu cha mtu. Elimu ya katiba na sheria ifundishwe kutoka shule ya msingi ili watu wapate kuelimika. Wakielimika tangu wakiwa wadogo hawatoweza kuiba.
Yapo mengi ila naomba kwa leo niishie hapo.