#COVID19 Baada ya Kukubali Chanjo, na Rais Samia Kuchanja, Kiongozi yeyote anayepinga Chanjo hadharani ni 'Insubordination' na usaliti

Naunga mkono hoja, hiki alichokisema Waziri Gwajima, ni kitu cha kweli, kama serikali yako imekubali chanjo na rais wako kachanja, wewe kiongozi wa umma, lazima uonyeshe uongozi kwa vitendo na kwa mfano, kwa viongozi wote wakuu wa umma lazima wachanje hadharani, ule uhiari, hauwahusu viongozi wa umma, kwa viongozi wa umma kuchanja ni lazima, asiyechanja aachie ngazi!.

Niliwahi kusema mahali, chanjo ya Korona japo inasemwa kuwa ni hiyari, hii ni hiyari ya lazima, kuna nchi mtu huruhusiwi kuingia bila cheti cha chanjo ya Corona. Hivyo sasa tunaanza mdogo mdogo kwa viongozi wa umma, chanjo sio hiyari ni lazima,
kama wewe ni kiongozi wa umma na huamini chanjo, achia ngazi!.
P.
P
 
Rahisi Sana mkuu haina haja ya kuanzisha vitisho.

Subili mtaona kwa macho yenu wenyewe..

Mimi ni mtumishi wa umma Sasa leteni huo upuuzi wenu muone Kama sitawaachia ofisi yenu halafu nikawajia kwa namna nyingine.yaani hapa tusije tukalaumiana na msidhani watu tuna njaa kihivyo kiasi Cha kuwaabudu.
 
Wito huu ni muhimu sana, kilichobaki ni CCM kuonyesha uwezo wa kuwashikisha adabu.

Mtu huwezi kumdharau rais wa JMT na Mwenyekiti wa CCM. Najua wote watapiga magoti kuomba msamaha, nashauri kwa Polepole na Gwajima, msamaha wao iwe ni kuchanja hadharani, kisha wawahamasishe wafuasi wao kuchanja. Jerry Slaa asamehewe tuu bila masharti.
P
 
Kama wewe ulivyoshikishwa adabu ya kamati ya bunge ya haki na madaraka ya bunge ndio furaha yako..............
 

Hili ni zoezi ni la hiari kuchanja au kutochanga. Binadamu sio mifugo, watumwa uwaambie wafanye unavyotaka kuhusu afya yao.
 
Mbona hukuwahi kusimulia ama kwa njia ya makala au kwenye chombo cha habari kilichojili kilikuwa kitu gani ili watanzania watambue kwa yakini kwamba uliwabwaga kwenye mashitaka yao?
Sisi wengine ni watu wa adabu na heshima, ukiitwa na mtu mkubwa wa heshima ya baba yako, ukapandishwa kwenye a boxing ring, halafu ukajua ukipandisha ma Jeb, na ma upper cut, utam knock out on the first round, hivyo ili usimuaibishe baba, unaruka ruka tuu ili kutengeneza a technical knock out, that is what happened. Tanzania tungekuwa na a responsible media, ingeisha hoji what happened!, it's very unfortunately, hatuna!.
P
 
Why can't you speak it out through your own media (Press and Public Relations-PPR) based on your journalism and legal consultancy expertise?
 

 
Why can't you speak it out through your own media (Press and Public Relations-PPR) based on your journalism and legal consultancy expertise?
Vitu vingine sio vya kusemwa. Kama aliyekuita alitangaza Bungeni live kuwa tutamuita fulani mbele ya Kamati kwa kujidhalilisha Bunge, na siku ya kuhojiwa akatangaza unahojiwa na picha za kikao cha mahojiano aka release, na baada ya hapo alipaswa kutoa matokeo, kama amenyamaza, who M, I kusema?. Vitu vingine ni kuviachage tuu.
P
 
Pole sana kwa yaliyokusibu pale TVT mkuu ila kumbuka siku zote Allah husimama na wanaosimamia haki
 
Mzee wangu Pascal pole kwa yaliokukuta lakini unawajibu kwenye hili, kama kiongozi wa mfano na mtu mwenye ushawishi.
Nasikitika kuwaza kuna namna umeathirika na matendo labda ya dola au wewe mwenyewe kwa sababu sentensi zako hazina nuru ziko kama za mtu mwenye mengi ya kusema lakini amezibwa kwa kizuizi fulani ambacho kwa maneno yako ni kama kipo nje ya uwezo wako.
Nikutumie moyo hakuna binadamu aliyetuleta duniani sote tunaishi kwa nguvu zilizo nje ya uwezo wetu, na kwa kupenda au kutopenda lazima siku moja tuondoke. Wasii wangu ni usitende kuwafurahisha kundi fulani hawana mamlaka unayotaka kutuonesha kwamba unawapa.
Ni kijana mdogo sana kukushauri ila ukiona hata chembe moja yenye hoja ibebe hoja nyingine nyingi mfu niachie niishi nazo dunia ni mwalimu mzuri huenda ni kajifunza kwayo.

NB: Sijachoma chanjo ila ninacheti cha waliochomwa kwa shughuli zangu. Sina hofu wala homa yeyote, namtukuza Mungu na mtumishi wake JPM kwa kuniondolea hofu dhidi ya corona
 
Pascal yuko sawa.
Sheria iko wazi hutaki au hukubaliani na Rais. Inatakiwa utoke wewe kwa kujiuzulu. Mengine ongezeni nyie.

Orodha ya waliowai kujiuzulu baada ya kutokubaliana na Rais hni wachache.

1. Oscar Kambona
2. Edwin Mtei
3.kingunge

Ongezea

Wengine. Slowx2 na Gwaji ni macho ku mchuzi tu .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…