mganda og
Senior Member
- Feb 23, 2023
- 134
- 445
Wakuu kwema?
Ipo hivi, nimekuwa kwenye mahusiano na binti fulani Kwa muda wa miaka mitatu.
Mwanzoni mwa mwaka huu nikasema sasa ni muda muafaka wa Mimi kwenda nyumbani kwao nikatoe mahari ili nimiliki mke rasmi.
Kweli tarehe za mwanzo wa mwezi January mwaka huu, nilipeleka ujumbe wangu kwao na binti, tukakubaliana mahari, nikalipa kiasi chote cha mahari tulichokubaliana.
Sasa wakati tukiwa tumeanza taratibu zingine ili tufunge ndoa ya bomani kwa maana tunatofauti ya kiimani Kati yetu, Ndipo nimegundua hii kitu.
Binti ana maruhani/majini, nimeshuhudia kwa macho yangu akifanya jambo lisilo la kawaida.
Tulikiwa tunakula chakula wote, mara gafla akaanza kudai kifua kinamuuma na akaanza kujishika kifua chake karibu na shingo na kujibana.
Kwakuwa sikuwahi kumuona kwenye hali hiyo, Nilinyanyuka gafla kutoka kweny kiti nilichokuwa nimekaa ili kumpa msaada Lakini nilikutana na upinzani wa hali ya juu sana kutoka kwake. Niliomba msaada kwa majilani ndipo walitokea watu wa wakunisaidia na hapo hapo nikapiga simu kwao ili nipate ufafanuzi labda hii hali wanaijua, wakaniambia nimwache atatulia mwenyewe.
Baada ya siku mbili kupita nimekaa nae chini kumuuliza kwanini alikuwa vile majibu yake ni kuwa ana Majini, nimejaribu kuuliza baadhi ya ndugu zake nao kumbe wanafahamu.
Nimemuuliza kwanini hakuniambia mapema majibu yake eti ningemuacha, sasa nifanyeje ndugu zangu na mahari nimeshalipa?