Baada ya kulipa Mahari kwao Ndipo nimegundua ana Majini

Baada ya kulipa Mahari kwao Ndipo nimegundua ana Majini

Tafuta namna ya kumsaidia kumtoa hayo majini au jipange vile utaweza kuishi nae na Hali yake ukishindwa hayo sema nae kwa amani mtapata muafaka wa pamoj

Hakuna mkamilifu harafu kama ndani ya miaka 3 hakuna usumbufu kuna ubaya gani akioa,mbona mimi ninayo huu mwaka wa nne niko na baba chanja wangu😀
Una uelewa na hayo mambo?
 
Aisee bora malaya kuliko mwenye majini, anaweza akakunyonga usiku ufe 😆

Wakati wa tendo majini yanaweza yakapanda akatoka nje nduki mkaanza kimbizana mtaani uchi 😆
Umewahi kusikia wapi mkuu mtu mwenye majini kamnyonga mpenzi wake wakati wa tendo wale nao wanaheshimu furaha ya mtu😁😁😁
 
Wakuu kwema?
Ipo hivi, nimekuwa kwenye mahusiano na binti fulani Kwa muda wa miaka mitatu.

Mwanzoni mwa mwaka huu nikasema sasa ni muda muafaka wa Mimi kwenda nyumbani kwao nikatoe mahari ili nimiliki mke rasmi.

Kweli tarehe za mwanzo wa mwezi January mwaka huu, nilipeleka ujumbe wangu kwao na binti, tukakubaliana mahari, nikalipa kiasi chote cha mahari tulichokubaliana.

Sasa wakati tukiwa tumeanza taratibu zingine ili tufunge ndoa ya bomani kwa maana tunatofauti ya kiimani Kati yetu, Ndipo nimegundua hii kitu.
Binti ana maruhani/majini, nimeshuhudia kwa macho yangu akifanya jambo lisilo la kawaida.

Tulikiwa tunakula chakula wote, mara gafla akaanza kudai kifua kinamuuma na akaanza kujishika kifua chake karibu na shingo na kujibana.

Kwakuwa sikuwahi kumuona kwenye hali hiyo, Nilinyanyuka gafla kutoka kweny kiti nilichokuwa nimekaa ili kumpa msaada Lakini nilikutana na upinzani wa hali ya juu sana kutoka kwake. Niliomba msaada kwa majilani ndipo walitokea watu wa wakunisaidia na hapo hapo nikapiga simu kwao ili nipate ufafanuzi labda hii hali wanaijua, wakaniambia nimwache atatulia mwenyewe.

Baada ya siku mbili kupita nimekaa nae chini kumuuliza kwanini alikuwa vile majibu yake ni kuwa ana Majini, nimejaribu kuuliza baadhi ya ndugu zake nao kumbe wanafahamu.

Nimemuuliza kwanini hakuniambia mapema majibu yake eti ningemuacha, sasa nifanyeje ndugu zangu na mahari nimeshalipa?
Msamehe tu alafu usimuache tafuta namna ya kumsaidia
 
Mkuu mahari sio kitu, wala sina shida kuiacha, ninachowaza ni je sitapatwa na ivo vitu? Pia ni MTU anayenijali Sana kama mume wake na amekuwa akilia nisimuache Kwa sababu ya ilo tatizo lake, kwaio namimi ninamuonea huruma kumuacha
Inaonesha binti hayuko tayari kukuacha, mpe sharti, kama anataka kuendelea kuwa na wewe umpeleke kwa watumishi akaombewe huo uchafu umtoke. Akikataa mrudishe kwao.
 
Mpeleke kwenye maombi

Yaani mahari ya mke mmoja nae kaja na faida ya michepuko ya kijini😋 Zari la Mentali ndilo hili🤣🤣
Mkuu hata Mimi nilikuwa nachukulia mambo kimasihara hivi hivi humu jamvini kama wew, paka pale yamenikuta ndio Naona kumbe kuna kupatwa na maswahibu
 
Back
Top Bottom