Baada ya kulipa Mahari kwao Ndipo nimegundua ana Majini

Baada ya kulipa Mahari kwao Ndipo nimegundua ana Majini

Kwa Kipindi hicho chote hatukuwahi kuishi pamoja mkuu, ndio tumeishi week moja tu sasa naiona iyo hali. Pia ukisema muongo unamaanisha izo nguvu za ajabu alizonionesha mbele yangu zilitoka wapi?
Kwa maelezo yako, inaonekana binti tayari alishaingia kwenye ndoa na majini hili ni jambo ambalo lipo sana hasa kwa akina dada lakini hata akina kaka. Hayo hapo ni aina ya majini wanaita jini mahaba.

Kwa hivyo kuna mkataba wa ndoa tayari kati ya binti na jini hilo mahaba uliofanywa kwa binti kujua anafanya nini au bila kujua. Ndoa hiyo lazima ivunjwe kabla ya wewe kuweza kumwoa binti huyo. Bila hivyo hutaweza kumwoa na hata mkifunga ndoa yenu hiyo Mahakamani ni bure tu, mtaishia kupata matatizo ya kila aina, mara ugonjwa, mara mimba kutoka, mara ugomvi na mwisho lazima ndoa itavunjika.

Inategemea imani yako lakini kwa vyovyote shughulika na kuvunja hiyo ndoa na ndipo uweze kufunga ya kwako. Ipo kazi kwani majini mahaba yana wivu mkubwa.

Pia chunga sana usiporomoshwe kiuchumi kwani ndio njia yao ya kupigana vita na wanaume wanaotaka kuwapokonya wake zao, watashambulia uchumi wako ukose hata nauli ya kwenda kanisani au msikitini, kuwa makini sana. Kama huyawezi hayo achana na azimio lako.
 
Mola kakuonyesha bado unatuuliza tena?

Inaonekana haujashtuka na familia unayoingia eeeeeh unalo kama hiyo siri wote wanajua.. Na imagine siku ya mahali walivyokuona wamekupata wakishukuru mzigo unakuwa wako.

Subiri basi uende futi sita na yote yako yasepe ubaki ukijutia.
 
Wakuu kwema?
Ipo hivi, nimekuwa kwenye mahusiano na binti fulani Kwa muda wa miaka mitatu.

Mwanzoni mwa mwaka huu nikasema sasa ni muda muafaka wa Mimi kwenda nyumbani kwao nikatoe mahari ili nimiliki mke rasmi.

Kweli tarehe za mwanzo wa mwezi January mwaka huu, nilipeleka ujumbe wangu kwao na binti, tukakubaliana mahari, nikalipa kiasi chote cha mahari tulichokubaliana.

Sasa wakati tukiwa tumeanza taratibu zingine ili tufunge ndoa ya bomani kwa maana tunatofauti ya kiimani Kati yetu, Ndipo nimegundua hii kitu.
Binti ana maruhani/majini, nimeshuhudia kwa macho yangu akifanya jambo lisilo la kawaida.

Tulikiwa tunakula chakula wote, mara gafla akaanza kudai kifua kinamuuma na akaanza kujishika kifua chake karibu na shingo na kujibana.

Kwakuwa sikuwahi kumuona kwenye hali hiyo, Nilinyanyuka gafla kutoka kweny kiti nilichokuwa nimekaa ili kumpa msaada Lakini nilikutana na upinzani wa hali ya juu sana kutoka kwake. Niliomba msaada kwa majilani ndipo walitokea watu wa wakunisaidia na hapo hapo nikapiga simu kwao ili nipate ufafanuzi labda hii hali wanaijua, wakaniambia nimwache atatulia mwenyewe.

Baada ya siku mbili kupita nimekaa nae chini kumuuliza kwanini alikuwa vile majibu yake ni kuwa ana Majini, nimejaribu kuuliza baadhi ya ndugu zake nao kumbe wanafahamu.

Nimemuuliza kwanini hakuniambia mapema majibu yake eti ningemuacha, sasa nifanyeje ndugu zangu na mahari nimeshalipa?

Kama mahari ni nyingi sana yaambie majini ya kurudishie; Fala wewe
 
Kwa maelezo yako, inaonekana binti tayari alishaingia kwenye ndoa na majini hili ni jambo ambalo lipo sana hasa kwa akina dada lakini hata akina kaka. Hayo hapo ni aina ya majini wanaita jini mahaba.

Kwa hivyo kuna mkataba wa ndoa tayari kati ya binti na jini hilo mahaba uliofanywa kwa binti kujua anafanya nini au bila kujua. Ndoa hiyo lazima ivunjwe kabla ya wewe kuweza kumwoa binti huyo. Bila hivyo hutaweza kumwoa na hata mkifunga ndoa yenu hiyo Mahakamani ni bure tu, mtaishia kupata matatizo ya kila aina, mara ugonjwa, mara mimba kutoka, mara ugomvi na mwisho lazima ndoa itavunjika.

Inategemea imani yako lakini kwa vyovyote shughulika na kuvunja hiyo ndoa na ndipo uweze kufunga ya kwako. Ipo kazi kwani majini mahaba yana wivu mkubwa.
Mkuu hapana jini mahaba hana mda wa kuonesha vituko kama yupo huyo huwa anadili na ridhiki zote na kuota usiku unafanya uchafu hana mda wa kuja eti umepandisha.
 
Mkuu kwani mahari umelipa sh ngap unafikiri mkija kuzaa na kuish so called mille utaweza kutolarate ebu acha ujinga piga chini na majini yake yamuoe au yamuache
Mkuu mahari sio kitu, wala sina shida kuiacha, ninachowaza ni je sitapatwa na ivo vitu? Pia ni MTU anayenijali Sana kama mume wake na amekuwa akilia nisimuache Kwa sababu ya ilo tatizo lake, kwaio namimi ninamuonea huruma kumuacha
 
Ana vitu ambavyo vinavuta majini!
Udi,Hina,Marashi,Tasbihi,mavitabu ya dini yao,nk
Kama bado anavaa manguo meusi kama maninja!
Avichome moto na kuachana navyo kabisa.
Hapo atayapona majini.
Mwisho tafuta mlokole ye yote hapo mitaani mwako aje amfanyie maombi!
Nimekoment bila kujua kama binti huyo ni Muislamu!
 
Mkuu hapana jini mahaba hana mda wa kuonesha vituko kama yupo huyo huwa anadili na ridhiki zote na kuota usiku unafanya uchafu hana mda wa kuja eti umepandisha.
Ni kweli ataharibu uchumi, mahusiano na atafanya kupandisha pia. Hayo yametokea wiki moja tu baada ya hao kuanza kuishi pamoja, kwa hivyo hayo yote ni protest ya jini kwamba ameingiliwa ndoa yake.
 
Back
Top Bottom