DPW ule ulikuwa ni mkataba wa hovyo serikali iliyoingia na waarabu kuendesha bandari zetu, sasa ukisema unaamini waislamu walitumia ile kama kigezo cha kulipa kisasi hapo unaonesha kumbe hao waislamu watakuwa wajinga.
Wajinga kwasababu madhara ya ule mkataba wa hovyo waliyoingia yatatuumiza wote, hayatachagua mwenye dini au mpagani, sasa kwanini wakatumia kigezo hicho kulipa kisasi kwa jambo litakalowaumiza mpaka wao wenyewe?!
Hii mada yako ni ya kufikirika zaidi, haijasimama inavyotakiwa, na umeharibu zaidi pale uliposema unaamini wanatupiga ila hujui how?!
Sent from my SM-G900H using
JamiiForums mobile app