crankshaft
JF-Expert Member
- Jun 12, 2019
- 1,427
- 3,438
- Thread starter
- #81
Unaongea kama una ubongo halafu unajichomoa.Sio lazima serikali ijenge hospitali zake kila mahali. Kama eneo tayari lina hospitali bora za kanisa, msikiti, Wahindu, Agha Khan, za watu au makampuni binafsi hakuna haja serikali kujenga hospitali eneo hilo.
Lengo ni raia wapate Huduma bora za Afya kwa ukaribu na bila misongamano. Pia hospitali zote ni za kibiashara, tofauti ni kiasi cha gharama tu ambacho wateja wanalipa.
Halafu makanisa , misikiti, makampuni au watu binafsi wakijiimarisha kwa hospitali na shule zao bora tatizo liko wapi??
Kama unanibishia hapa ukiwa unaegemea dini basi usinijibu Tena. Lakini kama unatumia akili Yako jibu.
Unasema zote biashara ila tofauti ni gharama,je gharama za serikali na private ni sawa??
Private ni kubwa sababu ni biashara Bali serikali gharama ni ndogo sababu inatimiza wajibu wake Kwa wananchi wake.
Sasa kutoa pesa za wananchi kwenda kusapoti biashara za watu ni sawa hiyo??
Sijasema kama ni tatizo Kwa makanisa kutoa huduma. Bali kutumia pesa ya umma kusapoti biashara za watu hasa hasa ya kidini,hili si haki.