Mange Kimambi ameshangazwa na hali ya Kiuchumi ya makamanda na kuhoji kwa nini makamanda wanaojitoa kwa moyo wote hawathaminiwi kwa kulipwa mishahara.
Mange ametoa rai hiyo kufuatia hali mbaya ya KIFEDHA inayowasumbua makamanda wengi akiwemo HENRY KILEWO ambaye mke wake JOYCE KIRIA (Mwanaharakati wa haki za wanawake) amelalamika kuhusu ukata unavyoisumbua familia huku majukumu muhimu kama ada na chakula yakitimizwa na Joyce bila msaada wa KILEWO.
Baadhi ya majirani wa HENRY KILEWO wamepata mashaka kuwa iwapo KILEWO atapata ubunge Mwanga 2020 iwapo atawahudumia wananchi au tumbo lake. Watu wa ndani wamegusia kuwa hali tete Kiuchumi pia imemkumba Yerico Nyerere ambae siku za karibuni amekuwa akiuza vitabu ili kuweza kujikimu.
Hali tete Kiuchumi kutokana na kutothaminiwa kwa makamanda kumepelekea baadhi ya makamanda kujiona kama makarai na kuamua kuacha siasa au kuhamia vyama vingine.
MANGE KIMAMBI ameitaka CHADEMA kuwaingiza kwenye Payroll makamanda na kuacha kuwakatisha tamaa huku Watu wachache wakinufaika.