Baada ya kumjali na kupigania mafanikio yake, leo nimegeuka kuwa mshamba

Pole Sana Mkuu!!!,Hawa viumbe Ndivyo walivyo huwa hawakumbuki mema waliyotendewa.
 
Bro nahisi ushauri huuu hapa umeupata..... Thanks bro carlos ushauri amaizing sana
 
Kama uliweza kumpigamia na kapata Kaz, baadaye kiburi na makucha ya nyodo, mi nakushaur pigaNia hafukuzwe kazi, Kama umempandisha kumshusha rahisi kweli, ungekuwa umemsomesha ingekuwa na ugumu, kumfukuzisha mtu Kaz kitu simple kweli, unacheza michezo hapo kazini kwake.
 
Pole sana kwa changamoto hakuna haja ya kuwa na mawazo kuna maisha baada ya kuachwa, songa mbele endelea na mambo yako achana naye kabisa huyo hakufai ipo siku atakutafuta.
 
Kamwe usije ukampenda mwanamke akiwa kwenye shida ila kama nikumsaidia msaidie tu. Furaha au huzuni huwa vinatafuta pakupumzikia kwa muda.
Pole bro endelea na maisha yako yana umuhimu mno kuliko huyo uliekutana nae ukubwani.
Uko sahihi mkuu
 
Kwa waliopitia hii hali mtakuwa mnajua kuwa maneno ya ushauri kama hayana msaada vile! Hata Rais akushauri au malaika akutokee akushauri bado tu maumivu yatakuwepo! Wengine watakuambia achana nae usimtafute au usiombe mtu akumbembelezee ilihali ndio kitu unachofanya!
Sasa ni hivi TIME HEALS kwa sasa huna la kufanya zaidi ya kukaa dawa ikuingie haswa, ujifunze jinsi binadamu tulivyo! Alafu as time goes unaizoea hali, labda after two years utakuwa umemsahau permanently!
Usiache kuongea na watu pale utapoona hali mbaya zaidi, pia ongea na watu wakupe exprience zao na jinsi wamesurvive sahivi wako poa. Kwa sasa dawa lazima ikuingie
 
Mkuu ña mimi namuongeza 1
ashukuru kuna kitu Mungu kuna kitu amemuepusha.
 
Hapo mm ndio huwa nakuwaga tofauti kidogo na wengine. Kama ni wake, basi hataondoka. Kitendo cha kuondoka tu, huyo sio wake. Yani aende huko apelekewe moto weee, mambo yakiwa magumu ndio arudi tena kwa jamaa???
Sina hakika sana lakini ninachojua watu wengi wanapitia changamoto mbalimbali wanapokuwa pamoja. Wengine wanaishia hata kuachana, wanaishi miaka kisha wanarudiana. Wengine hasa wanaume uwa wanaweza kumuacha mtu wake kwa tamaa ya mwili tu akidhani ni upendo. Ila akimaliza haja iliyompeleka akili inarudi. Maisha yanaendelea.
So mambo ni mengi na watu wamebeba stori tofauti za maisha hasa za kimahusiano. Huyo mwanamke anaweza kurudi na muhusika akajilaumu sana kupoteza muda kwa kuhuzunika kuondoka kwake. Yote yanawezekana.
 
Duuuuh haya mapenzi yana run duniaa ,alikiba aliiimbaaa
 
Atakuwa ni mpenzi wako wa kwanza huyo.

Ukipata mwingine akakupiga tukio kama hilo tena ndo utakuwa umefuzu.

Utakuwa sawa muda si mrefu, ila ukiendelea na ujinga wako wa kukaa ndani utachelewa kuwa sawa.
Kabisaaa
 
Bado una kaujana,under 25 hapo. Hayo mambo ya kawaida. Wapo wenzio walisomesha kuanzia form 1 mpaka chuo,bado demu anageuka. Unapoteza muda tu kujifungia ndani. Ni rahisi sana jifikirie tu mademu kibao,utawapata tu mbele huko. MUHIMU kwako kwa sasa ni kupambana sana kupata life la maana. Maana utambue tu amekukimbia sababu huna life la uhakika. So hiyo ikupe hasira kupambana kupata life ndefu. Huyo msahau haraka,tena wewe una bahati hujapteza aset zako nyingi na muda kwa huyo demu. Na bahati nyingine amekuonyesha makucha kabla hamjafika mbali kuwa mke. Msahau,endelea mbele. Na ipo siku tena atakutafuta nae akitendwa huko. Narudia tena wewe una bahati sana. Jione una bahati sana.
 
Sina Zaid ya kukuambia Mungu kakuonuesha mapema kwa sababu Nia yako ilikua Safi lakini huyo sio mtu kwako achana nae Mungu atakulipia na ipo siku utaleta mrejesho hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…