NO NO NO. MO Dewji ni kirusi kikali sana. Post nyingi za kumtuhumu Mangungu anazifadhili MO Dewji. Kisa ni kuwa kwenye kugombea nafasi ya Mwenyekiti wanachama wa Simba walimpa kura nyingi Mangungu kuliko yule mgombea aliyekuwa na sapoti ya MO Dewji. Kwa mtazamo wake huyu anayejiita mfadhili ni kuwa Simba wakifungwa basi wanachama watachachamaa wamwondoe Mangungu madarakani, Ushahidi wa kimazingira unaonyesha kuwa Dewji alihusika Simba kufungwa goli 5 na Yanga. Simba aliifunga Yanga kombe la hisani. Akacheza na El Ahly African Football League mechi mbili japo alitolewa lakini aliiheshimisha Simba. Ghafla anakuja MO eti anaunda mkamati ya kumsaidia kuiongoza Simba siku chache kabla kucheza na Yanga. Matokeo tunayajua. Ile kamati haijasikika tena. Na wajumbe wa ile kamati ni mashabiki wa yule mgombea aliyeshindwa na Mangungu kwenye uchaguzi. Tahadhari wapewe viongozi wa Simba kuwa kama ni msaada wote kwa timu autoe ila kamwe wasomruhusu MO na watu wake kwenda kambini kabla ya mechi na Yanga. MO anataka Simba ipate aibu kubwa zaidi ili iwe sababu kumwondoa Mangungu