#COVID19 Baada ya Kumsikiliza na Kumuelewa vyema Dk. Seche Malecela, Kesho najipeleka mwenyewe Kupata Chanjo yangu ya UVIKO 19 niwe salama zaidi

HABARI YA JANA HII
EPUKENI RAMLI
Sawa

[https://m]MATANGAZO YA MOJA KWA MOJA YA TV

[https://m]

IDHAA YA KISWAHILI

MASUALA YA JAMII

Biden kutoa dola 100 kwa kila atakapigwa chanjo ya COVID-19

30.07.2021

[https://static]

Rais wa Marekani Joe Biden amesema kila mwananchi atakaekubali kupigwa chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 atalipwa dola 100. Marekani ni nchi yenye chanjo za kutosha, na idadi kubwa ya watu wanaopinga kuchanjwa.

Rais wa Marekani Joe Biden amewashauri viongozi wa majimbo na miji yote nchini humo kuwalipa wakazi wao dola 100 ili wapigwe chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19.

Aidha ameweka sheria mpya zinazohitaji wafanyakazi wote wa serikali kuonyesha uthibitisho wa kupigwa chanjo au kulazimika kupimwa ugonjwa huo mara kwa mara, kuvaa barakoa pamoja na kuwekewa vikwazo vya kusafiri.

Soma zaidi: Marekani yaidhinisha chanjo ya BioNTech/Pfizer kwa watoto wa 12-15

Hatua hizo za hivi karibuni ni miongoni mwa juhudi za Biden kujaribu kuwahamasisha Wamarekani wenye kupiga chanjo, huku aina mpya ya virusi vya corona iitwayo Delta ikiwa inaenea kote nchini humo, hasa miongoni mwa watu ambao bado hawakuchanjwa.

Marekani inashika mkia miongoni mwa nchi zilizoendelea kwa viwango vya watu waliochanjwa, licha ya kuwa na chanjo za kutosha zinazotolewa bure. Juhudi za Ikulu ya Marekaniza kuhamasisha wananchi kuchanjwa zimegonga ukuta, hasa kutokana na vuguvugu kubwa linalopinga chanjo hiyo, habari za uwongo zinazosambazwa kuhusu chanjo pamoja na migawanyiko ya kisiasa.

[https://static]

Uamuzi wa Biden kuhitaji mamilioni ya wafanyikazi wa serikali na makandarasi kuonyesha uthibitisho wa kupigwa chanjo unaonyesha kuwa Ikulu imeamua kuchukua msimamo mkali zaidi huku virusi hivyo vya aina ya Delta vikiwa vinazidi kuenea.

Biden amewaambia waandishi wa habari wa Ikulu, kwamba watu wengi sana wanafariki dunia au wanapoteza watu wanaowapenda.

Idadi kubwa hawakuchanjwa Marekani

Kulingana na Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC), takribani watu milioni 163.8 nchini Marekani ndiyo waliochanjwa dozi kamili ya chanjo kati ya idadi ya watu milioni 330.

Serikali ndiye mwajiri mkubwa zaidi nchini Marekani, na hatua ya Biden inaweza kuwa mfano wa kuigwa na makampuni binafsi ya kibiashara na taasisi nyingine wakiwa wanajitayarisha kurudisha wafanyakazi maofisini.

Wafanyakazi wa serikali ambao watashindwa kuonyesha uthibitisho wa kuchanjwa watalazimika kupimwa ugonjwa wa COVID-19 kila wiki au mara mbili kwa wiki pamoja na kuwekewa vikwazo vya kusafiri.

Soma zaidi: Marekani yapoteza nusu milioni kwa COVID-19, Ujerumani yasambaza chanjo

Wizara ya Fedha imesema serikali za majimbo zitatumia dola bilioni 350 zilizotengwa kwa ajili ya kupambana na corona kuwalipa wananchi dola 100 kila atakaekubali kupigwa chanjo ya kuwakinga na ugonjwa huo wa COVID-19.

Biden amesema anafahamu kuwa wale ambao tayari wameshachanjwa hawatofurahichwa
 
Kwa hiyo Marekani inajiambukiza? Ni bora hoja ikawa kwenye ufanisi wa chanjo kuliko kuzusha eti chanjo inaeneza covid
 
Tuko mguu mmoja....

Njia moja......

Baada ya ufafanuzi wa mh.Rais SSH.....

Baada ya ufafanuzi wa mh.Waziri wa afya ,Dr.Gwajima.....

Akafuatia Dr.Malecela.....

Nimeshibishwa vyema....elimu imeniingia.....

#TujitokezeniKuchanjwaJ&J
#ChanjoNiBoraKulikoTiba
#NchiKwanza
#KaziIendelee
 
Kasemaje??

Kama ni mtaalamu na IQ kubwa si atengeneze chanjo yeye mwenyewe!
Kasemaje??

Kama ni mtaalamu na IQ kubwa si atengeneze chanjo yeye mwenyewe!
Kasemaje??

Kama ni mtaalamu na IQ kubwa si atengeneze chanjo yeye mwenyewe!
Anaishia kuwa mwalimu wa Sayansi tu ya chanjo .

Pamoja Na mazaifu mengi ya JPM lakini aliweza kuwaumbua wanasayansi wa Kitanzania.

Walipewa nafasi wajifungie Lab Na watoke Na studies inayoeleweka lkn wakaishia kufafanua maelezo ya Wanasayansi wa Magharibi

Ni aibu kubwa sana bora hata Legacy ya babu wa LoliondoπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
USIPOTOSHE kuhusu umuhimu mkubwa wa chanjo ya COVID-19.
 
Taarifa hizi hazitakiwi kbs Chief
 
 
Haya wafuate "wataalamu" wenzako, nenda na wenzako mkapate chanjo, sisi wajinga tuache na ujinga wetu na hizo barakoa zenu tutazivaa kama " gate pass"
 
Naona Vibaraka wa Mabeberu tumepata mfuasi nguli....

Usisahau kupeleka a/c number yako pale ubalozi wa Yu Esi Eii ili uingiziwe kabisa mkwanja
unang'ela panga'ng'a huku UKIMEZA "KUNDE"....

Nazo pia zinatoka kwa "mabeberu"....

Anyway ,Leo unamkataa J&J ,ila umesahau kuwa ndio ALIOKUFANYA USITOKE VIPELE VYA JOTO wakati wa uchanga na utoto wako....nawe unaendeleza kwa VITOTO VYAKO....

"Powder ya baby Johnson"....

#TujitokeziKuchanjwa
#NchiKwanza
#KaziIendelee
 
Labda wasingechanja wasingekuwepo kabisa
 
Chanjo ya Covid sio sawa na kununua majembe au majungu

sijasili kwenye portal ya wizara upate appointment ndipo uchanje
 
Tuna watu wa ajabu sana,mtu anakwambia hio ndio Chapa ya 666,kwahio ukiikwepa unasubiri kunyakuliwa na Yesu,mtu anasema hayo yupo baa analewa baadae anatafuta Malaya halafu anasema anasubiri kunyakuliwa.

Amesahau kwamba kuna amri kumi za Mungu.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Kazi kwelikweliπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Imeeleweka kwa urahisi sana. We waache tu watakutana na moto wenyewe.
 
Aisee bwashee unahangaika mitandaoni!!

How much are you paid?
 
Aisee bwashee unahangaika mitandaoni!!

How much are you paid?
"Wewe wasema" bwashee.....

I am not paid a single penny ,it's my zealousness to my beloved peaceful country ,happened to be called HOME....

#TwendeniTukachanjwe
#ChanjoNiBoraKulikoTiba
#KaziIendelee
 
Wewe masikini huna lolote Nani atake kukuua takataka Kama wewe
 
Alitimuliwa kwa upotashaji leo tunamchukulia mtu muhimu
Alitimuliwa na serikali iliyopita....

Rais wa Serikali mpya ni Msikivu mh.Samia Suluhu Hassan.....

#TujitokezeniKuchanjwa
#KaziIendelee
 
Kibwetere aliyechangamka aliyeko Ubungo Mkoani Dar es Salaam ambaye anajinasibu ni Mchunga Kondoo wa Bwana wakati kumbe ni Tapeli tu wa Kiroho
Turi kumwe πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜‚πŸ˜‚ daah!...mbavu zangu jamani...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…