Ni kweli pombe ,fegi na papuchii watumiaji baadhi ya hivyo tupo .shida ni kuwa covid 19 yenyewe ni ya kutatanisha inahoja kibao ,mara vita ya kiuchumi mara sijui china imeleta,pili hizo chanjo zake pasua kichwa mara hatari na tunaona kupitia shuhuda nyingi madhara ,mara wanazuoni wanabishana wengine ni hatari wengine ni salama ,mara J&J wazungu hawaitaki inamadhara(u.s.a).ndo hizohizo wamezileta bongo haohao sirikali wanalumbana mara wengine hivi wengine vile.Sigara na pombe tunawaona ndugu zetu Toka wanakua madhara yapo ila ni accidentally,hili jipya Kwa sie wenye low IQ linatuyumbisha sio la kwenda nalo haraka watupe elimu ya kutosha .Ufukara unatusumbua Tena tuanze kuhangaika na effects za hayo machanjo si ndo kifo chenyew mkuu.In short unapew Bure ila sidhani Kama utatibiwa Bure ukipata changamoto.
Kwa ilo nachagua pombe,sigara na uzinzi .
The problem, mengi ya hayo uliyotaja kama sio yote yanaenezwa na hao hao watu aina ya Askofu Rashid!!
Tatizo kubwa la Tanzania ni moja....
Kwa bahati mbaya sana aliyekuwa Rais wa nchi alikuwa anatia kasoro kila kinachoongelewa na watalaamu kuhusu corona!!
Kutokana na hilo, viongozi walio chini yake karibu wote wakawa wanalazimika kuimba tune ya Mwenye Bendi,
Wafuasi wake ambao ni wengi kabisa wakalazimika kuimba tone ya mwenye band!!!
Tatizo la sasa sio tena kwa viongozi kwa sababu viongozi wamepata mkuu mpya na hivyo wanalazimika kuimba tone ya mkuu mpya!!!
Wale wafuasi KATU hawawezi kukubali kirahisi kubadili tone ya yule waliyekuwa wanamuunga mkono kwa jasho na damu kwa sababu, kufanya hivyo itakuwa ni kama wanamkosoa kwamba hakuwa sahihi!!
Hawa, sio kwenye chanjo tu, ni kama wameapa kulinda na kutukuza misimamo yote ya Mwendazake!!!
Hata hapa ukifuatilia, asilimia kubwa ya wapinzani wa haya hii ni Wafuasi Kindakindaki wa Mwendazake!!!
Hata huyo Gwajima, I doubt kama angekuwa na msimamo huu lau kama Mwendazake angekuwa na mtazamo tofauti!!