Nimemsikiliza kwa makini daktari bingwa Malecela.
Ameelezea vizuri sana ila tu kuna sehemu mbili zinahitaji mjadala zaidi.
Suala la hizi chanjo za mRNA kuwepo kwa muda mrefu kabla ni sahihi lakini kwa kiasi kikubwa kipindi hicho anachosema kilikuwa Exploratory and pre-clinical stage.
Chanjo inapokuwa developed inapitia stage kuu kama tatu hivi;Exploratory stage,kipindi ambacho wataalamu wanaumiza vichwa kwa research za kugundua na kutengeneza dawa/vidudu pandikizi ambazo zitaendelezwa na kufanyiwa testing ili kuona kama zinafaa kukinga magonjwa fulani wanayoyalenga.
Then wakishazitengeneza wanaanza kuzifanyia testing maabara kwa kuzipandikiza kwenye vitu fulani vinaitwa culture pamoja na wanyama ili kuona kama zina ufanisi kwa kusudio husika.Hii inaitwa pre-clinical stage.
Chanjo ikivuka hapo ndipo inakwenda kutafutiwa kibali cha kufanya majaribio kwa binadamu halisi(clinical development) ambayo nayo huwa na stages kuanzia watu wachache hadi kuhusisha watu wengi.
Sasa nadhani watu wanapozungumzia muda mfupi wa chanjo hizi za covid wanamaanisha clinical development stage.(na nadhani wana hoja ya msingi sana hapa).
Kirusi cha covid kimegunduliwa mwaka 2019.Kabla ya hapo kilionekana kwa popo kikiwa hakina uwezo wa kuhamia kwa human host.
So hili ni somo jipya kwa wanasayansi ambalo lilihitaji muda wa kutosha kuelewa nini kinaendelea kwa mgeni huyu kuingia kwa binadamu.
Suala la pili ni pale aliposema kuwa habari ya chanjo hizi kuathiri DNA ni arguments za mitandaoni..with all due respect hapana..huu ni mjadala wa kisayansi umeanzishwa na wanasayansi na unahitaji majibu ya kisayansi.It's not a mere belief,its scientific argument.
Sayansi ya mRNA vaccine imechukua advantage ya sayansi ya mwili ili kufanya matibabu mwilini.How?
Katika seli kuna kitu kinaitwa nucleus,ndio makao makuu ya seli ambamo chembe ndogo inayobeba taarifa zote za uundaji na uendelezaji wa kiumbe husika inahifadhiwa.Chembe hiyo huitwa DNA.Sayansi yote ya binadamu imo ndani ya DNA.Ramani nzima ya utu wako imo humo.If anybody tamper with it,then you are finished.
Inapotokea mwili unataka kufanyika kitendo fulani cha uundaji au maintenance,DNA hutoa taarifa za kinachotakiwa kufanyika na kuiweka taarifa hiyo kwenye muundo fulani unaoweza kusomeka(message) na sehemu nyingine za seli.Huo muundo unaitwa RNA.
RNA(message) inakwenda kwenye sehemu nyingine ya seli inayohusika na utengenezaji inaitwa cytoplasm.Ndani ya cytoplasm kuna kitu kinaitwa ribosomes ndicho kinadecode RNA message na kutengeneza protein (matofali) zinazokwenda nje ya seli kufanya ujenzi au tukio lililokusudiwa.
Covid 19 virus anachofanya ni kuingia kwenye seli ya mwili na kutuma RNA zake kuinstruct seli itengeneze genetic materials kuunda more viruses.Kwa maana zaidi ni kuwa anaiteka na kuigeuza seli kuwa kiwanda cha kuzalisha virus wenzie zaidi.
Katika kufanya ufedhuli wake huo huyu virus anatumia kiungo fulani mwilini mwake kujiunganisha na seli ya host wake.Hicho kiungo kinaitwa spike protein.Ni kama hook fulani ambayo anainasisha kwenye cell surface ya host na kuigeuza mrija wa kupitishia RNA zake.So presence ya spike protein kwenye mwili wa virus ndio silaha kuu ya kujipenyeza na kuidhibiti seli ya host wake.
Mfumo wa ulinzi wa mwili huchukua muda kutambua mgeni huyu ambaye hajawahi kuonekana kabla.So wakati immune system inajivuta kumwelewa ili imshughulikie yeye muda huo anautumia kuathiri seli nyingi zaidi na kuzalisha virus wengi.Ndio maana natural immunity kama iko chini inakuwa shida kupambana na corona sababu hii by the time imetambua adui na kuanzisha vita inakuwa tayari viral load ni kubwa sasa kama mtu ana weak immunity ndio tatizo linakuwa kubwa zaidi.
Chanjo ya mRNA nayo inautumia mfumo ule ule kuusaidia mwili mapema kupambana kabla hali haijawa mbaya.
Yenyewe inaipa immune system uwezo wa kutambua virus mapema ili kumshughulikia mapema kabisa asisambae. So timing is the key.
Wazungu walichunguza genetic codes za virus wakachukua kipande kidogo cha information zinazohusu namna anavyounda ile spike protein yake wakatengeneza RNA yao maabara na kuiweka kwenye vaccine.
So hiyo RNA ya vaccine imebeba instruction ya kutengeneza ile sehemu ya kirusi inayotumika kujiunganisha na seli(spike proteins).
Unapodungwa vaccine ile RNA (mRNA) iliyowekwa humo inakwenda kwenye cytoplasm ya seli mwilini na kuinstruct seli itengeneze spike proteins.
As a result seli inatengeneza spike proteins nyingi lakini sababu ni hizo spikes tu na sio mdudu kamili inakuwa haina madhara kwa mwili ISIPOKUWA kitendo hiki kinaistua immunity ya mwili na kugundua kuna kitu kisichohusika kwenye mwili na kuanza kushambulia.
Immunity ikishatambua kuwa kitu fulani hakihitajiki basi inaweka memory hata baada ya miaka kikiingia tena kinakuwa kishatambulika na kushambuliwa.Ni kwa jinsi hiyo tunapata herd immunity.
So baadae hata akiingia virus mwenyewe as long as ana zile spike proteins ambazo immune imeshakuwa programmed kuzitambua kama antibodies anashambuliwa mapema kabla hajajizalisha zaidi na kwa namna hii ndivyo chanjo ya mRNA inasaidia.
HATA HIVYO kuna argument ya kisayansi kwamba kitendo cha seli ya mwili kugeuza DNA yake kuwa RNA ni kitendo kinachoweza kuwa reversed(reverse transcription) in presence of certain enzymes.Yaani under certain foreign influence inawezekana RNA ikageuka tena kuwa DNA.
Hapo ndipo huja hoja ya uhatari wa kutumia teknolojia hii ya kuinject foreign RNA kwenye human cell.
Kuna watu wanauliza hii mRNA ya vaccine ikishafanya kazi yake ya kuinstruct seli kutengeneza spike proteins yenyewe inakwenda wapi?
Wanaambiwa kuwa mwili ukianza kuzishighulikia zile spikes inashughulikia na hiyo RNA na host cell.
Linaulizwa swali jingine,sasa inakuwaje baadhi ya watu walioumwa na kupona covid wakipimwa kwa kile kipimo maalum kinachotambua genetic codes za virus wanaonekana kuwa positive ilhali damu zao ziko clean hazina viral load tena?hii imprint inayosomwa na kipimo inatokea wapi?kipimo kinasoma kitu gani?!!!
Kuna swali linaulizwa,je kitendo cha mwili kutegemea genetic instruction toka nje ili kutrigger immune response hakiathiri natural body immunity in the long run?
Na watu wamefanya research na kugundua wagonjwa waliopona covid kwa kuacha natural immunity response ifanye kazi wako stable na salama zaidi dhidi ya future infection kuliko wale ambao wamechanjwa.Watu wanachanjwa na bado wanaugua tena.Natural immunity ni strong hata kwa variants compared to vaccine immunity kwa mujibu wa baadhi ya research.So why hatuzungumzii kuwawezesha pia wale wenye natural immune(na ni wengi zaidi) badala yake tunawazodoa wasipochanja?kwanini hawawekwi kwenye jedwali na tunawalazimisha kuchanja?!
So you can see hii ni mijadala ya kisayansi na sio ya mere beliefs.
Inahitaji majibu na sio kuwa dragged.