Baada ya kumsikiliza Profesa Mukandala, nakubaliana na CHADEMA kwamba wadai Katiba Mpya "kivyao"

Mkuu hebu tuelimishe na sisi wewe umeona ni sababu ipi hasa ni ya msingi ambayo kikosi kazi kimeitoa
 
Shime wananchi, katiba mpya ni lazima sasa.

Hawa wanufaika hawawezi kamwe kutuambia katiba mpya ni sasa.

Hao watu wanataka posho tu toka serikalini.

Wananchi walisha ulizwa na wakatoa maoni yao, msitufanye sisi majuha.

Ila Zito umejidhalilisha, ninakosa kukuamini tena.

Ila Ahmadi Rashidi nisha mziea ni mchumia tumbo toka zamani.

Zito umesha jipoteza kwa ushirika huu.

Tume hii inaiimarusha tu CHADEMA mana inaonekana wazi ndo inayobeba agenda za wananchi peke yake.
 
Hicho ndicho kilichosahihi kukifanya,na kwa bahati mbaya hiyo ndiyo furaha ya CCM kutugawa na kutawaliwe.

Yote haya tunayoyaona ni premeditated, vyama vyote visivyo na mvuto wala kukubalika na Watanzania wenye akili wamewekwa kapu moja huku CCM wanapiga muziki beat soft wao Kazi yao kuimba na kucheza huku CCM wakila vinono.

Jambo hili ni kinyume na ubinadamu.

Upatikanaji Wa Katiba mpya upo mikononi mwa CHADEMA wakiungwa mkono na wananchi wazalendo huku wakipingwa na CCM na Mamluki wao.

Unafikiri nani mshindi?

Yaani kweli tusubiri tena uporaji kama ule Wa 2019&2020 ufanyike ndiyo tuandike Katiba mpya?

Seriously? Hapana,sitaki kuamini kama kuna Watanzania wataunga mkono pendekezo hilo.

Wakitaka tupige kura ya mlolongo tuone muitikio Wa wananchi.

Ushauri:Kwa kuwa uchaguzi Wa 2024/2025 umeshaibwa na CCM itapita bila kupingwa na wengine wamekubali kujisalimisha;

Tusiandae uchaguzi Wa SM na Uchaguzi Mkuu na badala yake tuwaache waendelea kutawala Ila waruhusu sisi wananchi kuendelea kuandika Katiba ili ikikamilika ndiyo tufanye chaguzi.

Vinginevyo hata tukisema uchaguzi ufanyike kwa Katiba hii mbovu matokeo yatawaleta CCM kutawala huku tukipata hasara ya fedha na muda Wa wananchi.

Sijasahau Mh Kikwete alipoahirisha mchakato Wa Katiba kupisha chaguzi za 2014&2015 alisema,"Twendeni kwenye uchaguzi na baada ya hapo mrithi wake aendeleze mchakato "Je,mrithi alipopatikana alisemaje?

CCM watawale nasi wananchi tuandike Katiba yetu mpya na Mara ikikamilika tunaanua Matanga rasmi.
 
Nchi imejaa unafki hii. Kwa hiyo Zitto nae anataka Katiba mpya baada ya 2025
 
Ninaamini hata Chadema hawawezi kutupatia katiba tunayoihitaji.

Kama tunafikiri kuna chama cha siasa kitatupatia katiba tunayoihitaji tunajidanganya..
 
Zitto ni dalali mkuu wa CCM
 
Wote hao ni madalali wakubwa wa kisisasa
 
Zito amefikia malengo yake binafsi, na Rais amemhakikishia kuwa kwa miaka 9 atakuwa analipwa posho kama mjumbe wa kamati mchongo ya katiba.

Zito lengo lake kuu ni kuwepo kwenye payroll ya Serikali, na amekwishafanikiwa.
Mi nilitegemea hayo yaliyotokea ukiona hilo jambo Zitto yupo ujue hakuna kitu
 
Zito Zito Zito, upo peupe sasa.

Nilikuamini nilikuwa nakutegemea ila kwa hili, umeniangusha, na ACT umeivunja nguvu, itakosa uungwaji na watu makini.

Tambua wapinzani makini wote hawawezi kubaliana na wewe namna hii.

Sitaki kuamini kama wewe ni msaliti, naomba tu uniambie kwamba wamekutega uingie mtegoni.

Of all the leaders sikuweza kufikiri wewe unaweza kuzidiwa akili na CCM kirahisi hivi!

Ila binadamu ni binadamu, njaa ameumbiwa binadamu.
 
Katiba sio barua ya uchumba, kwamba unaamka unaweka tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…