Baada ya kumsikiliza Profesa Mukandala, nakubaliana na CHADEMA kwamba wadai Katiba Mpya "kivyao"

Zito Zito Zito, upo peupe sasa.
Nilikuamini nilikuwa nakutegemea ila kwa hili, umeniangusha, na ACT umeivunja nguvu, itakosa uungwaji na watu makini.
Usicheze na Zitto afu ukabakia salama, sasa hivi Zanzibar imetolewa kwenye hoja ya kuwa na Mamlaka kamili na yenyewe nayo imejiunga na CCM bara kudai Tume huru ya uchaguzi, yaani walau sisi tuna afadhali watanganyika tusio na vyama tunaodai Katiba mpya.

Poleni wanzanzibar, hatuna namna ya kuwasaidia - kupanga ni kuchagua.
 
Ninaamini hata Chadema hawawezi kutupatia katiba tunayoihitaji. Kama tunafikiri kuna chama cha siasa kitatupatia katiba tunayoihitaji tunajidanganya..
Kumbe tutaipataje Sasa?

Jaribu kujazia hoja minofu,ni mbinu gani itakayotufanya tupate Katiba mpya nje ya kutumia vyama vya siasa kama waongoza dira?

Maana serikali,CCM na Vyama vya Briefcase wao wameungana kuwaambia wananchi wasubiri kwanza uchafuzi Wa serikali za mitaa na ule mkuu vipite kwanza.

Halafu wapo serious na wameshaanza utekelezaji bila kukawia,wananchi waende kwa nani?
 
Zitto kabwe ni dalali wa kisiasa
Zamani Nilikua nakataa kabisa Madai Haya Nikimuona Zitto kama Kijana Imara na mwenye Msimamo anaechukiwa kutokana na mafanikio yake Kisiasa.

Lakini Sasa Namuona kwa uhalisia wake...
 
Prof.Mukandala hawezi kwenda kinyume na Matakwa ya Serikali hata siku Moja!

Labda Mbowe awe Rais.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ