Baada ya kumsikiliza Profesa Mukandala, nakubaliana na CHADEMA kwamba wadai Katiba Mpya "kivyao"

Nchi ngumu sana.

Watu washapata ajira bwashee.

Tena wazee watupu vijana akina Nondo wanapambana na Putin wasiyemjua mitandaoni!
Heri yako kuyatambua hayo.

Hiyo ndiyo michezo ya CCM na Serikali yake.

Yako mambo utayaona kama ya kawaida, lakini yanakuwa planned in such the way that mtu wa kawaida hawezi kujua nini kinakuja.

Chadema waliona mbali sana
 
Wameulizwa na mh Rais Samia, nchi jirani zina Tume Huru ya uchaguzi je hazina migogoro?

Wakabaki wanacheka cheka tu kwa aibu.
Umeona uwezo wa Tume hii? Wameulizwa kaswali kadogo tu wanabaki wanaangaliana na kuchekeana.

Hii nchi kwa usanii huu kusonga mbele ni ndoto - demokrasia ni mdau mkuu wa maendeleo ya nchi.

Demokrasia hutegeneza nation identity, you move together you loose together, you survive together and finally you die together na KATIBA itokanayo na wananchi ndiyo funguo ya demokrasia hiyo.

Tanzania sisi bado tunaona demokrasia ni takwa la nchi zilizoendelea sisi halituhusu.
 
Binafsi sijajiunga na chama cho chote hivi sasa ingawa awali nilikuwa mwanachama wa TANU baada ya kuwa TANU Youth League nikiwa shule.

Kwa kifupi baada ya kuwasikiliza washauri na wapiga debe ningependa kutoa angalizo kuwa kuna watu wanaamini kuwa hiyo baada ya uchaguzi wa 2025 watakaosimamia huo mchakato ni CCM.

Mjue kuwa siyo lazima kama uchaguzi huo utakuwa huru kwa maana ya kuwa na mazingira rafiki ya kampeni, mazingira rafiki ya kupiga na kuhesabu kura na kisha ulazima wa kuheshimu maamuzi ya wapiga.

Wabobezi wa siasa wanasema katika ulimwengu wa siasa, juma moja ni muda mrefu sana; kwa maana lo lote linaweza kutokea kwenye hiki kipindi cha miaka iliyobaki kufikia 2025.

Ndiyo maana ni vizuri kila Chama kufikiria yajayo bila kujipangia Chama kitakuwa upande upi!

Hata wenzetu tunaowasanifu sasa ambao walikuwa wanafikiria siku zote watakuwa na madaraka walifikiri hivi hivi kama CCM na wapiga debe wake wanavyofikiri.

Naamini kabisa Nyerere hangefikiri hivi kama CCM inavyofikiri achia mbali kuunga mkono mpango wo wote wa kupotosha kura halali.
 
Tume kama ile ya Mto Mara🤣🤣🤣
 
Mchawi mkubwa wa hii nchi ni Tiss, kwa sababu ndio engineer wa maigizo yote haya tunayoyaona.

Ipo siku mtakubaliana na mimi kwa sababu hawafanyi tena yale chombo hicho kilichoundiwa kufanya, wao wamegeuka kuwa think tank ya kuvumbua mbinu ya kufanya ccm ing'ang'anie madarakani.

Yale yale wanayofanya FSB kule Russia ya kuhakikisha kwamba Putin anabaki madarakani ndio Tiss wanayofanya Tanzania.
 
Hongera mkuu kuujua ukweli
 

Hivi ni wewe au umedukiliwa?[emoji23][emoji23][emoji23] all in all safi sana kwa mawazo yako mkuu
 
Hii nchi bahati yetu mbaya,kila kiongozi ajaye na vituko vyake.

Mama Samia alikuwa Makamu Mwenyekiti Wa lililokuwa Bunge la katiba 2014.

Sasa atuambie,hiyo katiba ilipatikana?Haikuwa inahitajika?

Ilikuwaje akawa kiongozi Wa kitu kisichohitajika?

CCM tangia ule mchakato ambao licha ya gharama kubwa zilizotumika,ikaandikwa katiba pendekezwa,kilishindikana nini hata hiyo kupelekwa kwa wananchi ili waikubali ama waikatae?

Sijawahi kuwasikia mkiitetea katiba pendekezwa maana mnafahamu kuwa wananchi walikuwa waikatae na tungerejea alipoishia Mzee Warioba na kuandika tena katiba mpya kwa mawazo ya wananchi.

Ndiyo sababu kina Kikwete na Mwendaji wakaanza kuwindana kama paka na mbwa.

Haya basi tukubaliane vile mpendavyo nyie,mbona hamkurudi kwa mwenye shamba(wananchi Wa Tanzania)kumpatia mrejesho Wa Kazi aliyowatuma?

Mlikwama wapi na nini mapendekezo yenu kwa tajiri yenu(wananchi) kuhusu fedha zake mlizokula na Kazi hakuna?

Mnajiamini kuwa shamba limekuwa Mali yenu?

Kwa kiburi chenu mnataka kutuambia kwamba kamati/kikosi Kazi mlichounda ndiyo mbadala Wa mawazo ya wananchi Wa Tanzania?
 
Ukiona Chadema wamekataa au kuunga mkono kitu chochote, dont even think too much; those guys are smart, smart in thinking, smart on actions.
Siyo kweli bwashee, wakati mwingine wanapinga tu vitu ili waonekane ni wapinzani.

Chadema siyo watu wa kuwaendekeza hata kidogo.
 
Siyo kweli bwashee, wakati mwingine wanapinga tu vitu ili waonekane ni wapinzani. Chadema siyo watu wa kuwaendekeza hata kidogo.
Upinzani hauna uCCM wala uCHADEMA Bali ni hulka ya binadamu timamu kutofautiana na binadamu mwenzake.

Hatuwezi kuwaza sawa,sisi wote,kwa kila jambo,wakati wote kamwe.

Sasa hivi mwenye issue ya Katiba Mpya CHADEMA na wananchi wengi wanapigania Katiba mpya lakini CCM na mamluki wao wanapinga.

Hivyo kupinga ni haki ya kila binadamu.Tunatakiwa tukubaliane kutokukubalia au tukatae kukubaliana.

Hakuna aliye mpinzani Wa kila jambo na hakuna akubaliye kila jambo.

Lazima kubalance vitu kwa hekima zaidi.

Sote sisi ni watoto Wa Mama Tanzania.
 
Kuna vitu vidogo tu Chadema wajirekebishe na wawahubilie wanachama wake ambavyo havijengi chama.
 
Inaelekea Wazenji wameridhika baada ya kuona Maza yuko hapo.

Wasesahau ni muda tu.

Na muda hausimami.

Hata kama Tume ingekuwa ni muhimu, sasa hawa akina Duni na team yake hiv kweli wanafikiri Tume ya uchaguzi ya Bara itawasaidiaje huko Zenji.
 
Mapambio yanaanza kupungua ssasa"Anaupiga mwingi, nchi imefunguliwa, kila kitu mujarabu sasa, huyu ndiye nabii tuliyemtarajia, nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…