1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 7,201
- 9,529
Uchumi ni biashara sio siasa.
Suala la uchumi bado tunadanganyana.
Kikwete alikua kidogo anawapa watanzania uwezo wa kusafisha macho katika biashara za kimataifa. Hata Kenya walianza kuihofia Tanzania.
Watalii waliongezeka sana wakati wa JK. Kenya Uganda na Rwanda walifikia mahali wakawa wanatamani kuungana ili washindane na Tanzania katika biashara na uwekezaji.
Kuna mambo hua hatuyaangalii kwa undani lakini hata suala la makusanyo ya ndani wakati wa JK yalikua ni makubwa sana.
Leo hii mpaka vihela vya halmashauri na mashirika mbalimbali vyote vinaelekea Hazina lakini bado mambo ni magumu. Kodi zimekua kubwa sana lakini bado hatujafika hata 1.5 Tril. Pamoja na kuumiza wananchi kwa makodi na mafaini na hata kufilisi biashara za watu lakini bado. Hii ni dalili kuwa biashara hazijaongezeka wala kukua zaidi ya kutumia uchukuaji wa kodi kama kupora wanyonge vihela vyao kwa kisingizio cha wapiga dili. Hakuna wawekezaji wakubwa.
Mungu ametupa gesi ,jua, makaa ya mawe, ureniamu na upepo lakini bado Tunaharibu mazingira yetu ya asili kwa kukimbilia miradi ya Umeme wa maji MW 2000 tu bila kujali kuwa hizo zingepatikana kirahisi kabisa kupitia makaa ya mawe na upepo na Joto la ardhini jambo ambalo linalinda mazingira.
Kwa sasa watawala watashangilia sana mana wao sasa hivi ndio matajiri wenye uhakika wa kuvuna bila kupanda.
Zito Kabwe Endelea kuwafungua macho watanzania bila kujali vyama vyao.