Baada ya kumsikiliza Rais Magufuli, nasema wazi asante sana Jakaya Kikwete

Baada ya kumsikiliza Rais Magufuli, nasema wazi asante sana Jakaya Kikwete

Amani iwe nanyi wadau


Pamoja na kwamba Jakaya Kikwete amekuwa kiongozi kwa muda mrefu hadi kuwa rais wa Tanzania kwa miaka kumi ,nakiri wazi sikuwahi kuujua uzalendo wake kwa nchi ya Tanzania hadi leo November 2018 ndiyo nimegundua!

Nimejiridhisha pasina shaka kuwa Jakaya Kikwete ni mzalendo wa kweli wa nchi kuliko tunavyonfikiria.
Jakaya Kikwete ndiyo alikuwa na uamuzi wa mwisho nani awe rais ajae wa Tanzania lakini akatuletea Magufuli.
Jakaya Kikwete alikuwa anamjua Magufuli kuliko mtu mwingine yoyote , alikuwa anajua kabisa Magufuli hapendi rushwa na ufisadi ,alikuwa anajua kabisa Magufuli ana msimamo mkali usioyumba hata kwa dakika moja ,alikuwa anajua kabisa Magufuli kwake ni Tanzania kwanza na haoni shida kugombana na yeyote anayekanyaga masilahi ya Tanzania!

Swali kwa nini Kikwete pamoja na kuyajua yote haya bado akamteua Magufuli ?
Jibu ni rahisi tu ,Kikwete ni mzalendo wa kweli ndiyo maana alitaka amwachie nchi mzalendo wa kweli mwingine( Simba huzaa Simba). Kama Kikwete angekuwa ni fisadi kamwe nasema kamwe asingeruhusu Magufuli awe rais wa Tanzania na uwezo huo alikuwa nao.

Hotuba ya rais Magufuli leo kwenye kongamano pale udsm imeweka kila kitu wazi na kuacha bila shaka yoyote kwamba Magufuli anaijua Tanzania na ni mzalendo wa kweli kweli kwa nchi yake. Amezungumza kwa facts na data nchi ilipotoka ,ilipo na inaelekea wapi !
Magufuli ameonyesha wazi mchana kweupe kuwa ana uelewa mkubwa sana na inahitaji akili kubwa kumwelewa .Akili ndogo (chadema) kwa sasa hawatamwelewa Magufuli watakuja kuelewa baada ya miaka 20 ijayo.

Asante mzalendo Jakaya Kikwete kwa kuzaa mzalendo John Magufuli kwa manufaa ya nchi yetu .

Mungu akubariki sana na akupe maisha marefu.
Ningekuwa na LIKE zote

ningekupa Chief

Ila kuna wachafuzi wa mazingira,lazima wakuzogome kwelikweli

Vuta pumzi Bro

Povu litaendelea kuja zaidi na zaidi
 
Kabla ya kumuita jakaya kikwete mzalendo..jiulize ni Mali kiasi gani kajimilikisha ukianzia na mgodi wa dhahabu uliopo wilaya ya chunya mkoani mbeya.
Fisadi wa akili na mawazo

ukiulizwa ushahidi wa kweli

mnakimbia.....
 
Hivi ww uonavyo Magufuli ni mzalendo. Kuhutubia kwa kudanganya ndio uzalendo??? Kuua raia wako ndio uzalendo?? Kuua demokrasia ndio uzalendo. Ebu acha hizo Magufuli anafanya watanzania wote ni wapumbafu. Watanzania wote sio wajinga labda hao baadhi yenu na ccm yenu
Kamuua nani?!!!

Acha maneno ya ndotoni

Kama Demokrasia ni hiyo unayoisema ww na kuitamka,
Basi Bora ife kbs
Maana haina akili wala adabu kwa Wakubwa zake
 
Hujaisikiliza hotuba ya rais kwenye kongamano ,ndiyo maana unasema haya
Hotuba ni zile zile .
Uchumi sio hatuba uchumi ni kujenga Fursa na kuwawezesha wananchi kimitaji.

Ukiona serikali inawaonea wivu wananchi wake wanapomiliki biashara kubwa ujue haina uelekeo mzuri zaidi ya serikali ya Mateso.
Hata shetani ana Ufalme laki ni wa Giza.
 
Siku rais magufuli atakubali kutuletea katiba mpya hakuna mwanachi atakaye mpinga kwa hoja yoyote.
Anasema "vipi tuendeleen na rasimu ya Warioba au turudi tena kwa wananchi" hapa anamaanisha kua anajua kabisa haja ya wananchi ya kuipata katiba mpya.

Nakubaliana naye kua kama mlimchagua kwa ilani ile ya 2015-20, ambayo ndani yake haina Katiba mpya basi hana deni kwa mwananchi yeyote kwani hilo lipo nje ya ajenda ya Chama Cha Mapinduzi kwa sasa. Ila sote tumsubiri awamu nyingine hapo atahitajika kuijumuisha katiba Mpya ili hata aondokapo yale yote aliyoyasisi yabaki kisheria na yalindwe kikatiba.
 
Magufuli Jembe jembe
Rais wetu Jembe jembe
Amahakika tutakuja kumuelewa magu vizuri Kuwa ndio Chaguo letu Watanzania kwa wakati huu
Huyu anatufaa
nacho Kishukuru jamaa hatetereki
Yupo imala hatishwi
MUNGU ENDELEA KUMPA NGUVU NA UJASIRI
Chaguo la lubuva na tume, tuombe radhi.
 
Haizidi 1.5 ya mwaka huu pekee.Mzalendo wa kweli,alikuwa ni ticha tu kwa maneno na vitendo japo alifail kwenye uchumi.
Kabla ya kumuita jakaya kikwete mzalendo..jiulize ni Mali kiasi gani kajimilikisha ukianzia na mgodi wa dhahabu uliopo wilaya ya chunya mkoani mbeya.
 
Hotuba ni zile zile .
Uchumi sio hatuba uchumi ni kujenga Fursa na kuwawezesha wananchi kimitaji.

Ukiona serikali inawaonea wivu wananchi wake wanapomiliki biashara kubwa ujue haina uelekeo mzuri zaidi ya serikali ya Mateso.
Hata shetani ana Ufalme laki ni wa Giza.
Bakhresa ameonewa wivu ?

Acha kujipa matumaini hewa
 
True kijani walijali kuokoa chama kwanza hata kama uchumi utaangamia.Maana White air bila figisu,bao la mkono,IT za kina marope chama chakavu chali saa NNE Asubui. Hivo inabidi kilindwe kwa mtutu,kwa gharama ya kuminya demokrasia.
Umeongea vizuri sana kuhusu Magufuli,sasa unaposema Kikwete ni mzalendo kwa kuwa alikubali Magufuli awe Rais unakosa insight.Ukweli ni kwamba hali ya chama wakati ule ililuwa tete sana.Waliona njia pekee ya kuiokoa CCM ni kumleta mtu ambaye atakubalika na Watanzania walio wengi,na huyu hakuwa mwingine,isipokuwa Comrade Magufuli.
Magufuli hakuchaguliwa kuwa mgombea wa CCM kwa kuwa CCM ilimpenda,no he was a thorn even to the CCM status quo!It was a choice out of desperation.Without Magufuli may be CCM would be an opposition party today.Kwa hiyo si kweli kwamba Kikwete ni mzalendo,motive ilikuwa kukiokoa chama ambacho kilikuwa kinazama,sio uzalendo.
 
Mwisho wa yote pasipo tija bado ni deni
Upo udhaifu wa hapa na pale katika utendaji wake lakini kwa kiasi kikubwa ukimtazama usoni unaona kuwa kile anachokiongea kinatoka moyoni.

Ananifurahisha ile tabia yake ya kufikiria nje ya boksi. Anakuwa na originality kwa kila anachokifanya, hataki kufanana na mwingine, ni kiburi fulani hivi ambacho wakati mwingine kinamsaidia.
 
Muumini bila maandiko ataangamia ni bure kabisa
Hivi hiyo katiba ndo dubwasha gani? Hivi sheria zikiwepo na hakuna anayezifuata zitakuwa na maana?
Kwa nchi hii ilipofikia hatuhitaji katiba mpya tunahitaji viongozi wenye fikra chanya na utekelezaji wa mikakati kwa maendeleo endelevu ya Tanzania
 
Alichofaulu ni kupunguza wafanyakazi sio kuajiri
Uchumi ni biashara sio siasa.
Suala la uchumi bado tunadanganyana.

Kikwete alikua kidogo anawapa watanzania uwezo wa kusafisha macho katika biashara za kimataifa. Hata Kenya walianza kuihofia Tanzania.
Watalii waliongezeka sana wakati wa JK. Kenya Uganda na Rwanda walifikia mahali wakawa wanatamani kuungana ili washindane na Tanzania katika biashara na uwekezaji.
Kuna mambo hua hatuyaangalii kwa undani lakini hata suala la makusanyo ya ndani wakati wa JK yalikua ni makubwa sana.
Leo hii mpaka vihela vya halmashauri na mashirika mbalimbali vyote vinaelekea Hazina lakini bado mambo ni magumu. Kodi zimekua kubwa sana lakini bado hatujafika hata 1.5 Tril. Pamoja na kuumiza wananchi kwa makodi na mafaini na hata kufilisi biashara za watu lakini bado. Hii ni dalili kuwa biashara hazijaongezeka wala kukua zaidi ya kutumia uchukuaji wa kodi kama kupora wanyonge vihela vyao kwa kisingizio cha wapiga dili. Hakuna wawekezaji wakubwa.
Mungu ametupa gesi ,jua, makaa ya mawe, ureniamu na upepo lakini bado Tunaharibu mazingira yetu ya asili kwa kukimbilia miradi ya Umeme wa maji MW 2000 tu bila kujali kuwa hizo zingepatikana kirahisi kabisa kupitia makaa ya mawe na upepo na Joto la ardhini jambo ambalo linalinda mazingira.

Kwa sasa watawala watashangilia sana mana wao sasa hivi ndio matajiri wenye uhakika wa kuvuna bila kupanda.

Zito Kabwe Endelea kuwafungua macho watanzania bila kujali vyama vyao.
 
True kijani walijali kuokoa chama kwanza hata kama uchumi utaangamia.Maana White air bila figisu,bao la mkono,IT za kina marope chama chakavu chali saa NNE Asubui. Hivo inabidi kilindwe kwa mtutu,kwa gharama ya kuminya demokrasia.
Nimesema walimchagua apeperushe bendera ya CCM kwa kuwa ndiye tu aliyekuwa anakubalika.Please note that.Nafurahi kusema kwamba he has met the expectations of many Tanzanians.
Hongera zake sana.
 
Back
Top Bottom