Baada ya kumsikiliza Rais Magufuli, nasema wazi asante sana Jakaya Kikwete

Uchumi ni biashara sio siasa.
Suala la uchumi bado tunadanganyana.

Kikwete alikua kidogo anawapa watanzania uwezo wa kusafisha macho katika biashara za kimataifa. Hata Kenya walianza kuihofia Tanzania.
Watalii waliongezeka sana wakati wa JK. Kenya Uganda na Rwanda walifikia mahali wakawa wanatamani kuungana ili washindane na Tanzania katika biashara na uwekezaji.
Kuna mambo hua hatuyaangalii kwa undani lakini hata suala la makusanyo ya ndani wakati wa JK yalikua ni makubwa sana.
Leo hii mpaka vihela vya halmashauri na mashirika mbalimbali vyote vinaelekea Hazina lakini bado mambo ni magumu. Kodi zimekua kubwa sana lakini bado hatujafika hata 1.5 Tril. Pamoja na kuumiza wananchi kwa makodi na mafaini na hata kufilisi biashara za watu lakini bado. Hii ni dalili kuwa biashara hazijaongezeka wala kukua zaidi ya kutumia uchukuaji wa kodi kama kupora wanyonge vihela vyao kwa kisingizio cha wapiga dili. Hakuna wawekezaji wakubwa.
Mungu ametupa gesi ,jua, makaa ya mawe, ureniamu na upepo lakini bado Tunaharibu mazingira yetu ya asili kwa kukimbilia miradi ya Umeme wa maji MW 2000 tu bila kujali kuwa hizo zingepatikana kirahisi kabisa kupitia makaa ya mawe na upepo na Joto la ardhini jambo ambalo linalinda mazingira.

Kwa sasa watawala watashangilia sana mana wao sasa hivi ndio matajiri wenye uhakika wa kuvuna bila kupanda.

Zito Kabwe Endelea kuwafungua macho watanzania bila kujali vyama vyao.
 
Mimi ntampa kura tu, yani nasema hivi yangu nitampa kiroho safi kabisa
 
Mimi ntampa kura tu, yani nasema hivi yangu nitampa kiroho safi kabisa
Kura yangu ilishaharibika hat kabla ya wagombea kuchukua fomu. Nimechomwa na jua vya kutosha for nothing. Wacha liende, litafika tu!
 
Kura yangu ilishaharibika hat kabla ya wagombea kuchukua fomu. Nimechomwa na jua vya kutosha for nothing. Wacha liende, litafika tu!
Nasema hivi, yangu ntampa Magufuli kwa vipindi vyote atakavyo gombea.
 
Hivi hiyo katiba ndo dubwasha gani? Hivi sheria zikiwepo na hakuna anayezifuata zitakuwa na maana?
Kwa nchi hii ilipofikia hatuhitaji katiba mpya tunahitaji viongozi wenye fikra chanya na utekelezaji wa mikakati kwa maendeleo endelevu ya Tanzania
Elewa jambo moja mkuu! Hakuna mtu anae kataa maendeleo, lakini uwepo mwogozo wakuyasimamia hayo maendeleo yenyewe. Pengine huyu raisi wa sasa ni mzalendo kwa nchi yake. shida ikitokea tumepata raisi mwingine baada ya huyu na akawa siyo mzalendo itakuwaje? Yale yote mazuri yata yeyuka kama barafu.
Nasema bila katiba ya kueleweka bado tutakuwa tunapiga mawe chokaa mvua ikinyesha mawe yanarudi kwenye uchakavu.
 
Ebo!!! kiongozi utampata kwa utaratibu gani kama huna katiba? au hujui kuwa katiba ni mwongozo wa kila kitu katika nchi? katiba mbovu huleta viongozi wanaofanana nayo.
Hivi hiyo katiba ndo dubwasha gani? Hivi sheria zikiwepo na hakuna anayezifuata zitakuwa na maana?
Kwa nchi hii ilipofikia hatuhitaji katiba mpya tunahitaji viongozi wenye fikra chanya na utekelezaji wa mikakati kwa maendeleo endelevu ya Tanzania
 
Hujaisikiliza hotuba ya rais kwenye kongamano ,ndiyo maana unasema haya
 
NA KAKTIKA KIPINDI CHAKE CHA MIAKA KUMI YA URAIS HAKUWAHI KUPIGA PESA INAYOFIKIA 1.5 TRILIONI KAMA ILIYOPIGWA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MIWILI YA JIWE
Njoo na ushahidi .

Tuletee hiyo page inayoonyesha wizi wa 1.5T
 
Umeolewa?
Unawezaje kufananisha Magufuli (mwanadamu) na Chadema (chama); Wewe si bure, iko namna.
 
Ukimsiliza unaweza sema this is, lakini ukitazama anachofanya unaona vice versa nini tatizo?
 
Magufuli jembe
 
NYUMBA ZA SERIKALI, BIL 2 ZILIZOPOTEA KWENYE WIZARA YA UJENZI ILIYOKUWA CHINI YAKE, HAKIKA WEWE UNATOKA SOUTH SUDAN
 
Wapi TRIONI 1:3???
 
NYUMBA ZA SERIKALI, BIL 2 ZILIZOPOTEA KWENYE WIZARA YA UJENZI ILIYOKUWA CHINI YAKE, HAKIKA WEWE UNATOKA SOUTH SUDAN
Muulize Sumaye alikuwa waziri mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…