Baada ya kupewa Talaka, Wastara Sasa Hali Mbaya

Baada ya kupewa Talaka, Wastara Sasa Hali Mbaya

kazimia kwa furaha yakuweza kujinasua kwa muheshimiwa sana amaaa anaumia kumpoteza mheshimiwa
 
Baada ya kupewa talaka kufuatia madai ya kuvunjika kwa ndoa yake na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Donge, Zanzibar, Sadifa Khamis Juma kisha kuzimia na kulazwa hospitalini kwa mshtuko, hali ya kiafya ya staa wa Bongo Muvi, Wastara Juma sasa inadaiwa kuzidi kuwa mbaya.

WASTARA-3.jpg


Akielezea hali ya Wastara, babu wa Wastara aliyelazwa Hospitali ya Misheni ya St. Herry Heath Centre mkoani Morogoro, Abdulaziz Babu ambaye naye ni msanii maarufu wa filamu mkoani hapa alikuwa na haya ya kusema:
“Tangu aolewe na huyo Sadifa, ndoa yake imekuwa na migogoro mingi. Majuzi Wastara aliamua kuachana na mheshimiwa huyo kisha akabeba vitu vyake na kuja kwangu hapa Morogoro.

“Aliamua kuja kwangu kupumzisha akili yake. Chanzo cha mjukuu wangu kuugua ni huyo mheshimiwa aliyekuwa anaposti kashfa kwenye mitandao ya kijamii dhidi ya mjukuu wangu.
“Baada ya kuona hizo kashfa ndipo mjukuu wangu akapatwa na presha na kisukari kisha akapoteza fahamu.

“Niliamua kumkimbiza hapa hospitalini na hali yake ni mbaya kama unavyomuona. Kikweli hali hii inasikitisha na inaniumiza sana lakini najua Mungu anampigania.”
Alipoulizwa kama Wastara akipona na kuweka mambo sawa na Sadifa atarudi kwenye ndoa yake, babu huyo alijibu kwa jazba:
“Hatuko tayari mtoto wetu kuendelea kupata manyanyaso kama aliyokutananayo kwa kipindi kifupi kutoka kwa huyo mwanaume.
“Kwanza Wastara mwenyewe anajuta na ameapa kutorudi tena kwa Sadifa.”

Maneno ya Sadifa:

“Wastara ni mlemavu, hana baba wala mama halafu leo hii aniseme vibaya?”
Alisema kuwa hadi akaamua kumuoa ni kwamba alimpenda hivyo anashangaa kwa nini amseme hivyo.
Wastara amepitia katika uhusiano na ndoa kwa wanaume kadhaa. Awali alizaa na Mwanamuziki wa Kizazi Kipya, Msafiri Kombo ‘Solo Thang’.

Mwaka 2000, alifunga ndoa na Ahmed Kushi kutoka Zanzibar na kuzaa naye mtoto mmoja aitwaye Fares. Baadaye alifunga ndoa na msanii mwenzake, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ambaye kwa sasa ni marehemu na alizaa naye mtoto mmoja aitwaye Farheem kabla ya kufunga ndoa na Sadifa alikuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Bond Bin Suleiman.

Mnapoteza Muda Bure Kumuwaza ILA Ukweli Ni Kwamba Huyu Dada Ana LAANA Ya Sajuki Kwani Haiwezekani Kabisa Umetoka Tu Kumzika Mumeo Na Hazijapita Hata Wiki Tatu Tayari Akawa Ameanzisha Mahusiano Na Huyo Mbunge. Dada Zetu Hizi TAMAA Na DHIKI Mnazoziendekeza Zitazidi Tu KUWAUMBUENI Na Hivi MNATUDHARAU Sisi Mboga Moko Tunawatakieni Tu Kila La Kheri Na Hao WANAUME MATAJIRI Mnaowapapatikia. Halafu Ninachosikitika Kuna Members Humu Wakati Wastara Anaolewa Na Huyu Mbunge Walikuwa WAKIMPONGEZA KWELI Na Nashangaa Tena Leo Ndiyo WALE WALE Wanaomcheka Na Kumdhihaki. Hakika Sasa Nimeamini Ile Kauli Moja Niliyowahi Kuambiwa Na Mtu Mmoja Kuwa WATANZANIA WANA VITU VINGI NA KILA KITU ILA TATIZO LAO KUBWA NA AMBALO NDIYO LINAWAGHARIMU JAPO HAWATAKI KUAMINI NI TABIA YAO YA UNAFIKI KAMA SIYO UNDUMILAKUWILI.
 
Back
Top Bottom