Baada ya kupewa Talaka, Wastara Sasa Hali Mbaya

Baada ya kupewa Talaka, Wastara Sasa Hali Mbaya

mwanaume wa kweli huwezi kwenda Kumsema mkeo kwenye social media hata kama kakosea sana
 
Hivi warumi ile akaunti ni ya mh kweli? Au yule ambae wastara alisema wapo shega ndiye anayeirun????
ecf66178c13fd96d331a2994912cac35.jpg
 
Jamani! Isijekuwa hii ni bongo za muvi maana tumeambiwa hapo kuwa babu nae pia ni msanii wa filamu
 
Alianza yy wastara haumbuki kumsema mume huko insta akasahau jamaa n mwanasiasa mkubwa
 
Ha haa, yaani unamrekebisha na badala ya kushukuru au kujifunza kimya kimya anajifanya mjuaji

Mpuuzi Huyo Mkuu Achana Nae. Watanzania Ndivyo Tulivyo Ukikosea Halafu Mtu Tu Akikurekebisha Unaona Kama KAKUDHARAU Wakati Kumbe Amekusaidia. Mbona Hata Mimi Sometimea Huwa ( Navapa ) Nakosea Humu Na Wajuvi Hunirekebisha Na Wala Sijisikii Vibaya Na Tena Huwa Nawashukuru Sasa Yeye Kukosolewa Ndiyo Yamtoke Maneno Yote Hayo? Huo Muda Aliopoteza Kunijibu Na Kunitolea Maneno Yake Ya " Shomboninyo " Angeutumia Kujifunza Maneno Kadhaa Ya Kiingereza Sasa Hivi Angekuwa Wapi? Nimeshawazoea Hao Mkuu Wala Wasikupe Taabu.
 
Baada ya kupewa talaka kufuatia madai ya kuvunjika kwa ndoa yake na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Donge, Zanzibar, Sadifa Khamis Juma kisha kuzimia na kulazwa hospitalini kwa mshtuko, hali ya kiafya ya staa wa Bongo Muvi, Wastara Juma sasa inadaiwa kuzidi kuwa mbaya.

WASTARA-3.jpg


Akielezea hali ya Wastara, babu wa Wastara aliyelazwa Hospitali ya Misheni ya St. Herry Heath Centre mkoani Morogoro, Abdulaziz Babu ambaye naye ni msanii maarufu wa filamu mkoani hapa alikuwa na haya ya kusema:
“Tangu aolewe na huyo Sadifa, ndoa yake imekuwa na migogoro mingi. Majuzi Wastara aliamua kuachana na mheshimiwa huyo kisha akabeba vitu vyake na kuja kwangu hapa Morogoro.

“Aliamua kuja kwangu kupumzisha akili yake. Chanzo cha mjukuu wangu kuugua ni huyo mheshimiwa aliyekuwa anaposti kashfa kwenye mitandao ya kijamii dhidi ya mjukuu wangu.
“Baada ya kuona hizo kashfa ndipo mjukuu wangu akapatwa na presha na kisukari kisha akapoteza fahamu.

“Niliamua kumkimbiza hapa hospitalini na hali yake ni mbaya kama unavyomuona. Kikweli hali hii inasikitisha na inaniumiza sana lakini najua Mungu anampigania.”
Alipoulizwa kama Wastara akipona na kuweka mambo sawa na Sadifa atarudi kwenye ndoa yake, babu huyo alijibu kwa jazba:
“Hatuko tayari mtoto wetu kuendelea kupata manyanyaso kama aliyokutananayo kwa kipindi kifupi kutoka kwa huyo mwanaume.
“Kwanza Wastara mwenyewe anajuta na ameapa kutorudi tena kwa Sadifa.”

Maneno ya Sadifa:

“Wastara ni mlemavu, hana baba wala mama halafu leo hii aniseme vibaya?”
Alisema kuwa hadi akaamua kumuoa ni kwamba alimpenda hivyo anashangaa kwa nini amseme hivyo.
Wastara amepitia katika uhusiano na ndoa kwa wanaume kadhaa. Awali alizaa na Mwanamuziki wa Kizazi Kipya, Msafiri Kombo ‘Solo Thang’.

Mwaka 2000, alifunga ndoa na Ahmed Kushi kutoka Zanzibar na kuzaa naye mtoto mmoja aitwaye Fares. Baadaye alifunga ndoa na msanii mwenzake, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ambaye kwa sasa ni marehemu na alizaa naye mtoto mmoja aitwaye Farheem kabla ya kufunga ndoa na Sadifa alikuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Bond Bin Suleiman.
100% source ya hii news ni Global Publishers! Magazet ya udaku bwana!
 
Inavyoonekana kwa Wastara hajui anachokitaka au ana unrealistic expectations kwa wanaume anaoamua kufunga nao ndoa. Htimaye anakuwa disappointed (ukiachilia mbali huyo mume aliyefariki)

She needs to take it easy with marriage.
Ana tamaa,si mtu wa kuridhika
 
Wastara km anataka aheshimike aachane kwanza na hawa wanaume. Ajenge maisha yake mwenyewe. Kuwa na msururu wa list ya wanaume SIYO sifa nzuri.
Sijui tuseme ni fasheni au ni tamaa ya maisha mazuri na pesa? Jamii inakuheshim sana dadaang lakin kwa hii tabia yako inakufanya uonekane jamvi la wageni. Simama kidete jenga maisha yako; hawa wanatosha:

1. Solo Thang
2.Ahmed Kush
3.Sajuki
4.Bond
5.Sadifa
6.Na wengine ambao hta hawajulikani
 
talaka imepitia instagram???? ndo mambo ya usasa/digitally hayo mkuu.
Haya mambo kama ndivyo yanavyofanyika tunaelekea kubaya. Hakuna mafundisho ya dini yanayotuasa kufanya hivi.
 
Back
Top Bottom