Baada ya kupoteza kazi iliyokuwa inanipa heshima mjini pia nimepoteza na marafiki zangu wote

Baada ya kupoteza kazi iliyokuwa inanipa heshima mjini pia nimepoteza na marafiki zangu wote

Prisonerx

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2020
Posts
681
Reaction score
1,792
Hili jambo lisikie tu kwa watu baki, baada ya kupoteza tu kazi hata marafiki wamenikimbia.

Hadi naandika huu uzi mida hii moja haikai mbili hakai, hakuna kitu kinauma kwa mwanamme kama kuamka na kutokujua unaamkia wapi.

Niwakumbushe tu wanamme wenzangu wale mliopo kazini, heshimuni sana hizo kazi mlizonazo kwa wakati huu maana bila kazi ni kama upo uchi.

Mwisho kabisa tukumbuke kuwekeza pale tunapokuwa huko makazini, hizi kazi za private ni mtihani hasa maana muda wowote unaachishwa kazi.

Sitaki kuamini mimi huyu leo hata hela ya daladala inanitoa jasho 😒
Ni
 
Mkuu! Bado hujafikia kima cha chini kabisa cha ubinadamu... Yaani Ile kuona "Utakula... Au ndo Desh..."
Wewe mpaka una simujanja/kinakilishi?
 
You've slipped once. Uzuri ni kuwa sasa umeshapata mafunzo kutoka kwenye experience yako ya mwanzo. (Kuhusu ajira na marafiki).

Next time utakuwa umeshajua nini ufanye. Wengi tulishapitia huko nakujifunza wala usijishangae na kujilaumu. Pambana uinuke tena.
 
Pole kwa kupata marafiki wanafiki

Mimi ninae rafiki alinisaidia sana wakati nina shida,siwezi kumsahau,akinililia shida sijiulizi mara mbili

Hata akikosa kazi kesho nitampa mtaji bure kama atahitaji

Pole kwa masahibu na Asante kwa ushauri tutauzingatia

Matatizo yanakomaza,ukitoka hapo kwenye hizo shida umeiva kweli kweli
 
Hili jambo lisikie tu kwa watu baki, baada ya kupoteza tu kazi hata marafiki wamenikimbia.

Hadi naandika huu uzi mida hii moja haikai mbili hakai, hakuna kitu kinauma kwa mwanamme kama kuamka na kutokujua unaamkia wapi.

Niwakumbushe tu wanamme wenzangu wale mliopo kazini, heshimuni sana hizo kazi mlizonazo kwa wakati huu maana bila kazi ni kama upo uchi.

Mwisho kabisa tukumbuke kuwekeza pale tunapokuwa huko makazini, hizi kazi za private ni mtihani hasa maana muda wowote unaachishwa kazi.

Sitaki kuamini mimi huyu leo hata hela ya daladala inanitoa jasho [emoji19]
Ni
Mkuu, ichukulie hiyo hali kuwa kama ni phase nyingine ya maisha na Mwombe Mungu na usiache kumshukuru kwa kila jambo. Kuna mambo 2 yanayoweza kutokea sasa either upate kazi/shughuli nyingine ndani ya kipindi kifupi na hali yako kuwa bora labda hata zaidi ya ilivyokua kabla ikiwa hivyo ni heri na kwa ulichojifunza hadi sasa naamini kitakusaidia kufanya maamuzi bora au hali yako ikazidi kuwa ngumu zaidi kwa sababu ya kutopata kipato cha uhakika, ikiwa hivyo usikate tamaa endelea kupambana, kumbuka hauko pekeyako ktk hizo shida na wako wengi wana shida labda hata zaidi ya hizo ulizonazo.

Naomba nikushauri mambo 2 tu:
1) Usifanye wala kujaribu kufanya jambo/shughuli yoyote haramu ili upate fedha.

2) Epuka kukopa fedha na kutengeneza madeni maana hili shimo ukiliingia kutoka kwake itakugharimu sana.
 
Mkuu ulikuwa unapata pesa u akunywa na kula na marafiki tu bila kuwekeza?
Kama bado uko nyumba ya kupanga na una mke na watoto nakushauri,waambie waende kwa wazazi wako/wake ili ujipange upya.
La sivyo utadata na mkeo ataliwa na bodaboda au wauze genge/urembo kiulani.
Mwisho tueleze qualifications zako huenda ukapata mchongo mpya.
Kila la heri!
 
Mkuu haya mambo acha tu yaani kama hauna kazi kwa hapa Mjini ni kama uko uchi kiukweli, wacha nikupe mkasa ambao umenikuta nami mwaka jana tuu baada ya kupoteza mchongo ambao niliweza fahamiana na watu wengi hasa wale wenye uchumi mzuri tu watu ambao nilikua nikikaa nao tunaongelea kuhusu kupiga deals za pesa na Mipango lukuki huezi amini mara baada ya kusimamishwa kazini walianza kupukutika ghafla na mpka sahii wamebaki wachache ambao nao ni sababu ya ukaribu tu wa Mazingira ambayo tunaishi hivyo haipiti siku mbili lazima tutakutana. |Funzo pindi unapokuwa na wakati mzuri wa kipato tujijengee utaratiibu wa kuwekeza katika miradi mbalimbali ili hizi adha za kujiona tunakimbiwa na watu wa karibu zipunguwe.
 
Uliwekeza kwa mafukara wa akili na masikini hilo ndio tatizo
Chagua marafiki wenye maono ya kujikwamua na kujikita kwenye utafutaji zaidi kuliko wa kukutana nao pub
 
Back
Top Bottom