Baada ya kusikia vitu kama mchanga unamwaga batini usiku wa manane nimetoka nje kuangalia ila sioni kitu, nini tatizo?

Baada ya kusikia vitu kama mchanga unamwaga batini usiku wa manane nimetoka nje kuangalia ila sioni kitu, nini tatizo?

Mwagia chumvi ya mawe.
Nyingine iache wazi humo ndani.
Nipe mrejesho asubuhi.
 
Ndugu, kama unalala ndani na wao wanafanya shughuli zao nje we unaogopa nini ? Hapo unapotokatoka nje kila wanapofanya vitu vyao wanaona wamekuwin na ndio furaha yao. Ikiwa hawezi kudhuru roho yako unahangaika nae wa nini? Ukimpptezea atajiona anachokifanya hakina faida kwako mwishowe atakuita mchawi.
 
Anza kuandika proposal ya kujifunza wanga wanavyofanya kazi . Ni field ambayo iko underexplored. PhD ziko nje nje ila hamtaki kujifunza.
 
Nipo mkoani kikazi kuna ki apartment nimelipia mimi na mwenzangu mwezi japo kazi ni ya wiki 2 tu,

tumeishi wiki moja bila tatizo ila kuanzia usiku wa juzi kulikuwa na shida, ni kama kuna ndoo iliyojazwa mchanga inamwagwa juu ya bati.

Siku ya juzi nilidhani labda ni ndege au mnyama sikuzingatia sana japo mwenzangu alikuwa anaweweseka sana kusema ni wachawi, mi wala sikujali.

Siku ya jana hali ilikuwa kawaida tu ila mwenzangu alianza kulala bila kuzima taa, nikabaki namshangaa.

Sasa na leo hali imejirudia kama ya juzi nilitoka nje kuangalia batini ila sikuona chochote, nikapotezea nikarudi kuchapa usingizi huku mwenzangu akiwa amepaniki usingizi wake umekata, ghafla tena hali ikajirudia nilitoka nje kama mshale nikiwa nimebeba kurunzi kumulika batini lakini sikuona chochote

Naombeni ushauri maana sielewi, mwenzangu ndio yupo hoi kabisa nahisi tanesco wakikata umeme atazimia.
Acha kutumia muda mwingi kustarehe na kula tunda, umegeuza safari yako kuwa fungate. Ninakushauri hakikisha kila siku angalau unatumia saa zisizopungua nane kulala usingizi ili ubongo wako upumzike, ukifanya hivi tatizo lako litakwisha.
 
Wachawi ni watu wabaya sana. Juzi usiku niliamkaa ghafla na nikasikia saudi za watu zikizungumza chumbani kwangu. Nikatulia na kuanza kusikiliza na kuangalia kwa umakini zile Sauti zikapotea.

Nilipoamka asubuhi nikashangaa t-shirt yangu nimevaa mbele nyuma. Na hiyo t-shirt nilivaa mda mrefu tu kabla ya kulala na niliivaa vizuri tu. Ikanibidi niivue niangalie kama nimechanjwa na kusikilizia maumivj ya chale lakini sijaona kitu. Nikajua huyo mchawi atakuwa ni binti tu ana alimaindi my six park 😂😂
 
Haha majirani wamekuja kukutembelea, kojoa kwenye kopo alafu mwagia huko batini, utakuja kunipa matokeo na hawatarudia tena washenzi hao
Shida ni wakiiba na huo mkojo Tena nahisi tuta mkosa mwana Bora ahame tuu😀😀
 
Shida ni wakiiba na huo mkojo Tena nahisi tuta mkosa mwana Bora ahame tuu😀😀
Mkuu amini nakwambia, mkojo ni kitu kitu kikubwa sana kinachokwamisha shuguri zao kufanyika. Yaani ni kama vile unavyosikia kitimoto ndio sawa na mkojo. Kama nyumbani kwako kuna mauza uza, jenga tabia ya usiku kukojoa kwenye ndoo au kopo alafu liache pembeni ya kitanda likiwa wazi. Hakika nakwambia vimbwanga vyao hautakuja kuvisikia tena.
 
ndrungu zango,

apo apartment si kuna mti apo ambao matawi yake yanakaribia kugusa bati?🐒

maana yake kukiwa na upepo hayo matawi yananesa hadi kugusa bati ndio mnaskia kama kumwagwa mchanga means ayo matawi yanakua kama yanafagia bati 🐒

kwahivyo msiogope wala kua na Imani potofu 🐒

By the way,
mchawi mwenyewe muoga kichizi ndio maana anafanya kazi zake usiku gizani🐒
🤝🤝
 
Nipo mkoani kikazi kuna ki apartment nimelipia mimi na mwenzangu mwezi japo kazi ni ya wiki 2 tu,

tumeishi wiki moja bila tatizo ila kuanzia usiku wa juzi kulikuwa na shida, ni kama kuna ndoo iliyojazwa mchanga inamwagwa juu ya bati.

Siku ya juzi nilidhani labda ni ndege au mnyama sikuzingatia sana japo mwenzangu alikuwa anaweweseka sana kusema ni wachawi, mi wala sikujali.

Siku ya jana hali ilikuwa kawaida tu ila mwenzangu alianza kulala bila kuzima taa, nikabaki namshangaa.

Sasa na leo hali imejirudia kama ya juzi nilitoka nje kuangalia batini ila sikuona chochote, nikapotezea nikarudi kuchapa usingizi huku mwenzangu akiwa amepaniki usingizi wake umekata, ghafla tena hali ikajirudia nilitoka nje kama mshale nikiwa nimebeba kurunzi kumulika batini lakini sikuona chochote

Naombeni ushauri maana sielewi, mwenzangu ndio yupo hoi kabisa nahisi tanesco wakikata umeme atazimia.
Punguza papara ukiwa unaangalia, leo nitakuja tena kumwaga fuso la mchanga hapo nyumbani kwako. jitahidi uwe makini.
 
Back
Top Bottom