Baada ya kusoma vitabu zaidi ya 300, nimegundua kumbe nilitakiwa kusoma Biblia tu

Bodo kuna vingi sivijui. Naendelea kujifunza. Na nitakufa vingine sivijui. Ila mleta maada huwezi sema kitabu kilichoandikwa miaka 1500 iliyopita kina kila kitu.

Sasa hivi tupo kwenye AI - Akili bandia. Hata hao mitume na waandishi wa biblia ukiwafufua leo wataona hii dunia ni uchawi tupu. Teknolojia ya leo sio ile ya kwenye biblia. Kila kitu kimebadilika
 
Mkuu,

Samahani wewe huwa unasoma vitabu vya aina gani zaidi? Philosophy, Physics/Engineering, Biological science, au ni vipi?
Nasoma vitabu vya mambo mengi tofauti.

Current events, history, science/tech, philosophy, sometimes fiction.

Kwa mfano. Nimemaliza kusoma "Going Infinite: The Rise and Fall of a New Tycoon" cha Michael Lewis akielezea story ya Sam Bankman-Fried and the rise and fall of his FTX crypto empire.

Awali mwaka huu nilimsoma Abdulrazak Gurnah, Muingereza mwenye asili ya Zanzibar aliyeshinda Nobel Prize in Literature mwaka jana, kitabu chake "Afterlives".

Pia nimesoma "Surrounded by Idiots" kimenisaidia kuelewa mambo mengi kuhusu saikolojia ya kujua kukaa vizuri na watu wajinga wengi.

Sasa hivi namsoma Dr. Robert Sapolsky wa Stanford, namfuatilia vitabu vyake kuanzia "Behave", ana kitabu kipya kinaitwa "Determined: A Science of Life Without Free Will" anaelezea jinsi gani idea nzima ya "freewill" isivyokuwa imejengwa katika ukweli wa mambo.
 
Sasa uvivu Biblia kifungu kimoja tu kinatosha. Ukikitafakari kinakutoa kwenye Biblia kinakituma hadi kwenye jalala nje ya nyumba yako ukaangalie na kuchunguza na kutafakari ubunifu wa sisimizi.

Au shamani jinsi panzi wanavyopiga kazi bila manager, supervisor au CEO.

Akili yako inafunguka kabisa.
Huyo steve Covey anaandika vitabu vingi ambavyo kwenye biblia vinakuwa summarized na kifungu, ukikitafakari kinakupa page karibu laki za kufikiri.

👇👇👇👇
Proverbs 6:6
[6]Go to the ant, thou sluggard; consider her ways, and be wise:

Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima.
Ni wapi sasa nitamsoma kwa kina huyo mdudu kwenye biblia? Nataka nijue kila kitu kuhusu huyo mdudu chungu.
 
Bodo kuna vingi sivijui. Naendelea kujifunza. Na nitakufa vingine sivijui. Ila mleta maada huwezi sema kitabu kilichoandikwa miaka 1500 iliyopita kina kila kitu.

Sasa hivi tupo kwenye AI - Akili bandia. Hata hao mitume na waandishi wa biblia ukiwafufua leo wataona hii dunia ni uchawi tupu. Teknolojia ya leo sio ile ya kwenye biblia. Kila kitu kimebadilika
Nimeweka contradictions na mapungufu kibao yaliyomo katika Biblia hapo awali kwenye uzi huu, watu hawataki kukubali kwa "cognitive dissonance" tu.

Ni kama vile umelelewa na baba kwa miaka 50, ukijua huyo ni baba yako mzazi kibaiolojia, halafu siku moja unaletewa DNA evidence kuwa huyo si Baba yako wa kibaiolojia.

Unaanza kuipinga DNA, unaihakiki mara tano, majibu yaleyale.

Unasema wanasayansi wamekosea, DNA haiko sahihi.

Yani watu wana imani zao za kale, halafu ushahidi wa kisayansi mpya usiopingika unaonesha imani zao ni potofu.

Badala ya kukubali kuwa imani zao ni potofu na kwenda na ushahidi wa elimu mpya, wanataka kung'ang'ania vitabu vyao vya imani za kale.
 
Acha uongo...
Vitabu vipo direct to the point,
BIBLIA mambo ni mengi mpaka mtu akuongoze, na kila mtu anatafsiri kitu kwa utaishi wake na na namna alivyofunuliwa.
Ukisoma Bible kama story it's full of contradictions.
HUHITAJI ROHO MTAKATIFU kuelewa regular books
 
Nasoma vitabu vya mambo mengi tofauti.

Current events, history, science/tech, philosophy, sometimes fiction.

Kwa mfano. Nimemaliza kusoma "Going Infinite: The Rise and Fall of a New Tycoon" cha Michael Lewis akielezea story ya Sam Bankman-Fried and the rise and fall of his FTX crypto empire.

Awali mwaka huu nilimsoma Abdulrazak Gurnah, Muingereza mwenye asili ya Zanzibar aliyeshinda Nobel Prize in Literature mwaka jana, kitabu chake "Afterlives".

Pia nimesoma "Surrounded by Idiots" kimenisaidia kuelewa mambo mengi kuhusu saikolojia ya kujua kukaa vizuri na watu wajinga wengi.

Sasa hivi namsoma Dr. Robert Sapolsky wa Stanford, namfuatilia vitabu vyake kuanzia "Behave", ana kitabu kipya kinaitwa "Determined: A Science of Life Without Free Will" anaelezea jinsi gani idea nzima ya "freewill" isivyokuwa imejengwa katika ukweli wa mambo.

Gunnah..Nimesoma pia ni Novelist mzuri sana novels kama vile The Last Gift, Gravery heart, Paradise (Paradiso), na Pilgrims way pia nimesoma. Na ana misamiati adhimu sana. Napenda kalamu yake japo ana reflect sana jamii za visiwani yaani zanzibar. Pia sorrounded by idiots sikumalizaga kusoma. The four agreements pia nimekisoma na kufanya tafakuri ya kina sana na vitabu vingine vya Psychology na Science pia.
 
Nimeweka contradictions na mapungufu kibao yaliyomo katika Biblia hapo awali kwenye uzi huu, watu hawataki kukubali kwa "cognitive dissonance" tu.

Ni kama vile umelelewa na baba kwa miaka 50, ukijua huyo ni baba yako mzazi kibaiolojia, halafu siku moja unaletewa DNA evidence kuwa huyo si Baba yako wa kibaiolojia.

Unaanza kuipinga DNA, unaihakiki mara tano, majibu yaleyale.

Unasema wanasayansi wamekosea, DNA haiko sahihi.

Yani watu wana imani zao za kale, halafu ushahidi wa kisayansi mpya usiopingika unaonesha imani zao ni potofu.

Badala ya kukubali kuwa imani zao ni potofu na kwenda na ushahidi wa elimu mpya, wanataka kung'ang'ania vitabu vyao vya imani za kale.
What is your Mission Mkuu Kiranga?
 
Kichwa chako ndio kinacontradictions.

Hata wewe biblia imekuzungumzia. Walimu na debate zako ulizofuatilia kwa muda mrefu zimejeruhi mindest yako ktk biblia.

Quantum physics ni kitu kidogo sana. Biblia inazungumzia Quantum leap katika vifungu vingi, concepts qmbazo ukiziapply kwenye maisha zinakuvusha exponentially.
Unaweza kuhangaika na maequestions meeengi ila conclusion unakuta kwenye biblia tunakifungu tayari kimeshaizungumzia direct au kwa kukidecode.

Proverbs 23:7
[7]For as he thinketh in his heart, so is he:
Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo.
Ulianza vizuri kutetea hoja zako post za juu ila hapa umeshindwa kumpa Kiranga kifungu Cha Biblia kinacho elezea Quatum Equations / Quantum mechanics kwa ufasaha.
Pengine fasaha kiasi cha kuweza kutumika kwenye kutengeneza synthetic chemicals maabara.

Kweli Bible ina maarifa mengi lakini hayapo ktk maelezo ya kina au ufafanuzi wa kutosha kama vitabu vingine vya specialized subjects.
Hivyo haiwezi kuwa mbadala wa vitabu vingine vyote.
Haielezei au kufundisha kuhusu DNA kwa undani n.k.
 
Bible pia ina contradictions na makosa mengi.

Nimeweka nyingi sana hapa, lakini wanaoipaisha Bible wamekataa hata kujibu.
 
Back
Top Bottom