The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 4,249
- 11,592
Baada ya majaji wa High court kukataa mapingamizi yote ya Tundu Lissu juu ya uhalali wa mahakama kuu kuendelea kusikiliza shauri hili, hatimaye amesomewa shitaka lake la uhaini leo 15/9/2025...
Baada ya kusomewa shitaka, swali kwa mshitakiwa kikawaida huwa ni KWELI au SIO KWELI. Kwa kimatengo tunasema: GUILTY or NOT GUILTY...?
Tundu Lissu hakujibu swali hilo kwa maana ya kukubali au kukataa kosa. Bali moja kwa moja aliweka pingamizi dhidi ya hati ya mashitaka kuwa haisemi kosa lake analoshitakiwa nalo ni lipi. Na kwa maana hiyo hajui akubali au kukataa nini...
Hali ilikuwa hivi👇🏻👇🏻
Karani wa mahakama: Anamsomea Mhe. Lissu mashtaka. Baada ya karani kusoma hati ya mashtaka anamuuliza Lissu aseme kweli si kweli?
Mhe. Tundu Lissu: Waheshimiwa majaji kabla sijajibu naomba twende kifungu cha 295 (1) na 294 (1) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai nchini. Waheshimiwa majaji katika vifungo hivyo nilivyovitaja mtaona kuwa siwezi kujibu kama ni kweli au si kweli kwa sababu kifungu hiki kinasema hati ya mashtaka kama haisemi kosa, basi inatakiwa iondolewe kwa mujibu kifungu cha 295 (1). Sasa hati iliyopo mbele yetu haionyeshi kosa la uhaini na kwa hatua hii na kwa ushahidi uliopo hata ikirekebishwa haiwezi kusema kosa na hivyo inapaswa kutupiliwa mbali. Sasa naomba nianze kujenga hoja yangu kwa kutumia kifungu cha 135 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai hapa nchini..."
##Hapa Tundu Lissu alichambua kwa kina sifa za hati ya mashitaka ya kosa la uhaini inavyopaswa kuandaliwa na kuwa akitumia ushahidi wa rejea wa maamuzi ya kesi mbalimbali za jinai zilizowahi kuamuriwa kwa kutumia kigezo cha kisheria cha "sifa ya hati nzuri ya mashitaka" inavyopaswa kuwa...
##Aidha kwa kutumia vifungu vya sheria, alitoa darasa la maana ya "uhaini" na ingredients zake kisheria zinazotengeneza kosa la uhaini. Anauliza maneno "tutahamasisha uasi" au "tutakinukisha" au "tutazuia uchaguzi" hayapo kabisa katika orodha si tu ktk makosa yanayoweza kutafsiriwa kama uhaini bali hata kwenye makosa ya jinai kwa mujibu wa sheria za Tanzania hususani sheria ya uchaguzi kifungu cha 7 hayapo...!!
Katika eneo hili hivi ndivyo ilivyokuwa👇🏻:
Mh. Tundu Lissu: Tuangalie tafsiri ya maneno haya kwa mujibu wa Kamusi mbalimbali za kiswahili
(a) 'Hamasisha:' Ni tia nia, msukumo kwa watu ili kufanya jambo fulani.
(b) Uasi: 1: Ni KITENDO Cha Uvunjaji wa Sheria kinachofanywa na kikundi cha watu kwa lengo la kubadili mfumo wa nchi yao....
2: Na maana ya pili ya neno "UASI" ni Kitendo cha kuwapinga wenye mamlaka au kupinga Sheria na taratibu zilizopo kama vile katiba ya taasisi, shirika au chama fulani...
Mh. Tundu Lissu: Waheshimiwa Majaji ninayo pia Kamusi ya kiswahili sanifu ya chuo kikuu Cha DSM (TUKI) nayo inatafsiri neno uasi vile vile kama hizi zingine nilizowasomea
Mh. Tundu Lissu: Waheshimiwa majaji, nina kamusi ya kiswahili fasaha ya Baraza la kiswahili Zanzibar (KAMIZA). Nayo anawasomea maana ya maneno hayo na kisha anawauliza maswali kadhaa majaji hapa
✔Je Mheshimiwa kuna uhaini hapo?
✔Nikiitisha maandamano nchi nzima bila kibali ni uhaini?
Mh Tundu Lissu: Obviously, Sio uhaini...!
##Kwa siku ya leo tarehe 15/9/2025 Tundu Lissu amemaliza kujenga hoja yake kwa kusema👇🏻
Mh Tundu Lissu: “Kupinga waliopo madarakani katika nchi yenye mfumo wa vyama vingi vya siasa siyo kosa la jinai. Hata kama ni kosa la jinai, Je, ni la kumshitaki ili apatikane na kosa la kunyongwa kwa huyu mtu kwa mujibu wa sheria zetu..?"
Mh. Tundu Lissu: Ni kweli kwamba nilisema tutakinukisha. Maneno "tutakinukisha" siyo uasi. Maneno "nukaa" au "nukia" hayawezi kuwa "uasi" achilia mbali "uhaini". Na kwa mujibu wa kamusi hizi tatu hapa, maneno hayo siyo uhaini....
Mh Tundu Lissu: Kukinukisha unaweza kufanya mtu au kitu kinukee vibaya au kinukie vizuri. Je, huo ni uhaini? Uhaini dhidi ya nani? Huo siyo uhaini....?
Mh. Tundu Lissu: Kuhamasisha wananchi kuandamana kwa ajili ya kuzuia uchaguzi ambao mifumo yake imeharibiwa haiwezi kuwa uhaini. Unaweza kuwa kosa lingine lolote kama lipo lakini siyo uhaini...
Mh. Tundu Lissu: Nikisema tukazuie uchaguzi ili usiibiwe inakuaje kosa la jinai? Nikisema mfumo wa uchaguzi wetu ni hovyo inakuaje kosa la jinai? Nikisema katiba hii ni mbovu sana ibadilishwe inakuaje uhaini? Tutahamasisha uasi, tukinukishe, tukazuie uchaguzi. Maneno hayo hayawezi kuwa uhaini....!!
Mh. Tundu Lissu: Hayo ni maoni yangu na msimamo wangu. Je, ni halali kisheria kustahili kuniweka siku 160 gerezani kwa maneno haya kwa sababu tu kuna watu hawataki kuyasikia na hivyo kwa utashi wao tu kinyume kabisa cha sheria kuyageuza kuwa kosa la uhaini la kuhalalisha kunionea na kunitesa kwa kuninyang'anya uhuru wangu...?
##Kwa leo Tundu Lissu ameishia hapo na kwa sababu ataendelea kesho kuanzia saa 3:00ASB. Ataendelea kujenga hoja zake za kisheria ili kuonesha kuwa hati ile ya mashitaka haina uhalali wa kisheria kusimama na hivyo itupiliwe mbali na kesi ishie hapo..
##Tusubiri kesho tuone anakotaka kutupeleka...
================================================
MAONI YANGU
1. Kwa maoni yangu naona picha moja kubwa, kuwa hata hawa majaji watatu hawana tofauti na Franco Kiswaga wa Kisutu Resident Magistrate Court aliyeonekana wazi kutofanya maamuzi yake kwa kuzingatia sheria. Lakini hapa Jaji Ndunguru na wenzake nao wanaonekana kufanya yaleyale. Kesi hii ni kama haimuliwi kwa kuzingatia sheria bali utashi wa mtu.
2. Lengo bila shaka yaweza kuvuta muda mpaka Samia atangazwe mshindi wa Urais watoe. Na kwa maana tutakwenda hivihivi kwa sheria kusiginwa na baadae watoe hukumu hivyo hivyo kimagumashigumashi, baadae akate rufaa na Tundu Lissu akaipate haki yake huko kwenye Court of Appeal. Wakati huo uchaguzi (ukiwepo) utakuwa umeshapita..!!