Baada ya kutangaza ndoa, mchumba wangu kaniweka wazi ni single mother, upendo umeyeya nafikiri kumuacha

Baada ya kutangaza ndoa, mchumba wangu kaniweka wazi ni single mother, upendo umeyeya nafikiri kumuacha

Darwin Nunez

Member
Joined
Jun 12, 2022
Posts
90
Reaction score
212
Wakuu

Nimekuwa na mahusiano ya takribani mwaka mmoja na mwanamke ninayempenda mpaka kufikia kuamua kutangaza ndoa
Kila kitu kuhusu kutambulishana kilishafanyika kwao na kwetu, mahari pia nimelipa japo sijamaliza yote lakini wazazi wamebariki tuendelee na mchakato wa ndoa

Huyu mchumba wangu nimekuwa nikimuamini sana huwezi mdhania kwa mambo mabaya kwani kipindi chote hiki tumeishi kwa uwazi kumbe yeye aliwahi zaa miaka mitano huko nyuma akanificha

Moja ya kiapo ambacho nimejiwekea pia baba yangu mzazi hunisisitiza sana ni kutokuoa muke ya mutu i mean aliyekwisha zaa (single maza) kwani wanamadhira sana hawa watu pia hawezi achana na mzazi mwenzie

Sasa wakuu nimeingiwa mawazo sana, upendo ule wa mwanzo umeisha ghafla nimefikiria kuachana na huyu mwanamke hata kwa maumivu ya gharama kiasi gani lengo tu niepuke fedhea hii na madhira nayowezapata huko mbeleni

Naombeni ushauri.
 
Kwa kweli ndg, duuh pole Sana... Alikutegeshea ufike hatua ya kutangaza ndoa ndio akwambie akiamin hutamuacha.

Mkuu hapo huna mke ndg yangu jiongeze tu. Kama kakuficha issue sensitive Kama hiyo mkiwa wachumba je, mkiingia kwenye ndoa si utagundua mengine mengi ya kukuchachafya moyo na roho.
 
Oa Bwana mdogo acha kelele.Hata wewe kuna vitu umemficha.Chukua chuma hiko na maisha yaendelee.


Kwenye mahusiano tunaanza na uongo na baada ya miaka 20 ndani ya ndoa ndo utajua ukweli kwa hatua fulani wakati wingine ni mpaka mmoja afe ndo utajua au atajua.

Fiksi ni sehemu ya maisha ili yaendelee
 
Dah tukisema wanawake mashetani wanatupiga mawe humu ndani kumbe ukweli wenyewe ndio kama hivi.

Aisee pole sana mkuu hapo ni kuhesabu hasara tuu hamna namna.

Kwa kweli suala la kumtambulisha single maza kwa wazazi wako wakati wanawake wamejaa kibao ni kuwakosea adabu wazazi wako.

Hiyo piga chini fasta mwanawane
 
Ila hii theory mnayosemaga single mother hawezi kuachana na aliyemzalisha sijui huwa mnaipata wapi sijui. Mtoa mada na wenzio naomba nikuulize kidogo,

1. Ukioa asiye single mother na akawa na mabwana tisa ndani ya ndoa yako unapata faida gani
2. Huamini kabisa mtu anaweza akaachana na mtu mwingine mazima?
3. Ukioa asiye single mother lakini amewahi kutoa mimba 9 kuna faida gani?

Badilisheni mitazamamo yenu. Asilimia kubwa ya mwanamke ku cheat ni wewe mwanaume unavyoamua kuyapeleka maisha ( Najua wapo vipepe yes). Unaweza kuoa bikira ila huko mbele ukachapiwa kuliko kawaida

Kuwa positive. Maisha sio magumu kiasi mnachoyasemea mitandaoni na mitaani. Tatizo la kweli hapo ni moja tu, kwanini hakusema mwanzo japo inawezekana pia aliogopa utamuacha sababu ya akili zako au alikuwa hakuchukulii serious kiviiiile.
 
Oa Bwana mdogo acha kelele.Hata wewe kuna vitu umemficha.Chukua chuma hiko na maisha yaendelee.
Kwenye mahusiano tunaanza na uongo na baada ya miaka 20 ndani ya ndoa ndo utajua ukweli kwa hatua fulani wakati wingine ni mpaka mmoja afe ndo utajua au atajua.
Fiksi ni sehemu ya maisha ili yaendelee
ni bora uwe muwazi tangu mwanzo kama mtu atakubali sawa kama atakataa sawa, maana uongo ukija kujulikana utapunguza uaminifu
 
Alikosea kuficha toka mwanzo ila cheki na moyo wako. Binafsi nimeona single mothers wengi tu wameolewa na maisha yanaenda freshi. Hizo habari za hawezi muacha mzazi mwenza ni dhana tu ambayo watu wengi wanayo dhidi ya single mommas.

Kama unampenda we oa. Mtoto abaki huko huko alikokuwa siku zote.
 
Back
Top Bottom