Baada ya kutengana na mwanamke nimeota ndoto mbaya

Desierto

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
901
Reaction score
3,112
Hii ndoto nimeiota saa nane usiku na usingizi ukayeyuka kabisa

Ni mwezi mmoja sasa unaishia toka ameenda kwao mpaka sasa hajarudi

Kisa cha kutorudi ni kwasababu wakati anaondoka nilimwambia asiende hivo nikakuta ameenda kwao kulikuwa na sherehe.

Lengo ilikuwa sio kumzuia lengo nilikuwa tu namzingua ili aende mchana maana kwao sio mbali hivo.

Sasa mm nikawa sijapenda yeye kuwaamsha watoto asubuhi maana sherehe ilikuwa ni siku inayofuata.

Basi tukazinguana kidogo nikampiga kofi la uso sababu ya kuamsha watoto kwa nguvu.

Nikamwambia kama anaenda aende ila asijekurudi tena.

Basi nikaingia zangu job nikarudi jioni nikakuta kasepa zake kachukua hela tuliyokuwa tumeitunza mahali kama 50 hivi.

Basi mm nikamkumbusha tu asijekuwahi kurudi.

Basi baada ya siku kadhaa akaniomba nimtumie nauli arudi.

Mm nimemwambia nauli situmi aje tu kwa nauli yake ila pia akija lazima nitamuadhibu. Kwa kukaidi amri yangu.

Basi tuishie hapo twende kwenye ndoto.

Nilikuwa na mtoto wangu wa kike mdogo hivi tupo kama pembezoni mwa mto wa maji yanayotembea sasa mtoto alikuwa anacheza uchi kwenye kina kifupi cha maji yanayotembea kwa kasi, ghafla nikamuona akijitupia kina kirefu na kuzama nilikuwa umbali kidogo kama mita 10 hivi basi ikabidi nikimbie na kwenda kuwahi kwa mbele kidogo nikapeleka mikono kama kuotea tu, ila nikafanikiwa kumshika nikamnyanya juu akawa anatapika yale maji na kulia. Basi nikatoka nae kwenye maji na kuelekea nyumbani.

Na usingizi ukakata ghafla.

Je hii ndoto inamaana gani?

Sipendi kutengana na mke wangu ila naona kama hakuna namna nyingine ugomvi ni umekuwa sehemu ya maisha yetu kila siku.
 
Huyo mwanamke ameshakuona fala tu huna jipya unawezaje kumwambia mkeo ustoke ye akatoka tena anajiandaa ukiwepo home then anafka uko anafanya yake anamaliza anakupgia cm tuma nauli nirud umejdai kataa ila umesema arud kwa nauli yake maana yake huna msimamo na ulichoksema akienda bila ruhusa yako asirud we ni ma.tako kbs na bdo akachota na kahela mlikokuwa mmetunza ndan huyo angekutana na mataikoni kama mimi ndo ilikuwa nitolee aisee..arud wp kwa mfano.
 
Nikukumbushe tu Kwenye misiba wanaume wanaangalia mke wa marehem hivyo hivyo kwa wanawake,Kwenye sherehe yoyote Ile wanaume tuna angalia pisi Kali hivyo hivyo kwa wanawake pia mwanamke akienda kwao piga ua atakutana na yule mwanaume wake wa kijijini hivyo mkuu umepigiwa ukweni!
 
Rudi kwa nauli yako. Wewe mzee mkeo alikaidi amri yako kwa sababu alijua kabisa huna msimamo. Kuhusu ndoto subiri Mshana Jr
 
Hii ndoto nimeiota saa nane usiku na usingizi ukayeyuka kabisa

Ni mwezi mmoja sasa unaishia toka ameenda kwao mpaka sasa hajarudi

Kisa cha kutorudi ni kwasababu wakati anaondoka nilimwambia asiende hivo nikakuta ameenda kwao kulikuwa na sherehe.

Lengo ilikuwa sio kumzuia lengo nilikuwa tu namzingua ili aende mchana maana kwao sio mbali hivo.

Sasa mm nikawa sijapenda yeye kuwaamsha watoto asubuhi maana sherehe ilikuwa ni siku inayofuata.

Basi tukazinguana kidogo nikampiga kofi la uso sababu ya kuamsha watoto kwa nguvu.

Nikamwambia kama anaenda aende ila asijekurudi tena.

Basi nikaingia zangu job nikarudi jioni nikakuta kasepa zake kachukua hela tuliyokuwa tumeitunza mahali kama 50 hivi.

Basi mm nikamkumbusha tu asijekuwahi kurudi.

Basi baada ya siku kadhaa akaniomba nimtumie nauli arudi.

Mm nimemwambia nauli situmi aje tu kwa nauli yake ila pia akija lazima nitamuadhibu. Kwa kukaidi amri yangu.

Basi tuishie hapo twende kwenye ndoto.

Nilikuwa na mtoto wangu wa kike mdogo hivi tupo kama pembezoni mwa mto wa maji yanayotembea sasa mtoto alikuwa anacheza uchi kwenye kina kifupi cha maji yanayotembea kwa kasi, ghafla nikamuona akijitupia kina kirefu na kuzama nilikuwa umbali kidogo kama mita 10 hivi basi ikabidi nikimbie na kwenda kuwahi kwa mbele kidogo nikapeleka mikono kama kuotea tu, ila nikafanikiwa kumshika nikamnyanya juu akawa anatapika yale maji na kulia. Basi nikatoka nae kwenye maji na kuelekea nyumbani.

Na usingizi ukakata ghafla.

Je hii ndoto inamaana gani?

Sipendi kutengana na mke wangu ila naona kama hakuna namna nyingine ugomvi ni umekuwa sehemu ya maisha yetu kila siku.
Ndugu acha ukaidi, huyo ni mkeo na effect wanapata watoto wako hapa humuadhibu mkeo unawaadhibu watoto. Jaribu kufikiria watoto kuamshwa asubuhi wakati wanatakiwa walale na up and down za watoto kwenda na kurudi wakati wanatakiwa wapumzike

Jaribu kusikiliza wimbo wa Michael Jackson heal the world. Natumaini utafeel pain kutoka kwenye huo wimbo na hutofanya hayo tena
 
Ndoto kama hii ya Desierto — inayohusisha maji, mtoto, na hisia za huzuni au hofu — mara nyingi hubeba ujumbe wa kisaikolojia na kihisia unaohusiana na maisha halisi ya mtu. Hebu tuivunje hatua kwa hatua:

---

🌊 1. Maji yanayotiririka kwa kasi

Maji katika ndoto mara nyingi yanawakilisha hisia, maisha ya ndani, au hali ya kiroho.

Maji yanayotiririka kwa kasi ni ishara ya hisia kali, mabadiliko, au migogoro ambayo ni vigumu kudhibiti.

Inaweza kumaanisha kuwa ndani ya nafsi ya Desierto kuna maumivu, huzuni, au majuto yanayotiririka bila amani — hasa baada ya kutengana na mke wake.

---

👧 2. Mtoto akizama

Mtoto anaweza kumwakilisha:

Sehemu ya ndani (innocent/self) ya Desierto — ile roho isiyo na makuu, upendo, au matumaini yake yaliyokuwa ndani ya uhusiano.

Au anaweza kumwakilisha mke wake, kwani katika ndoto za kifamilia, mtoto mara nyingi huwa ni ishara ya matokeo ya uhusiano (emotional bond).

Kuzama kwa mtoto ni ishara ya kuzama kwa hisia, uhusiano au matumaini.
Lakini pia, ni hofu ya kupoteza kitu chenye thamani — kama upendo au familia.

---

✋ 3. Kumwokoa mtoto na kumtoa majini

Hii sehemu ni muhimu zaidi.

Inamaanisha bado ana hamu ya kurekebisha mambo, kuokoa kilichoharibika, au kubadilisha makosa aliyofanya.

Ni ndoto ya majuto na matumaini kwa wakati mmoja.

Hapa akili ndogo (subconscious mind) inaonyesha kwamba Desierto anajutia kitendo cha kumpiga mke wake na kumwambia asirudi — lakini ndani ya nafsi bado anaona anaweza “kumwokoa”, kama vile alivyookoa mtoto majini.

---

🛏️ 4. Kuamka na usingizi kukata

Hii ni ishara ya tukio lenye mshtuko wa kihisia (emotional awakening).
Ndoto hiyo haikuwa tu simulizi bali ishara ya nafsi kupaza sauti:

“Unaumia, lakini bado unampenda. Na ndani yako kuna hofu ya kupoteza kabisa familia.”

---

💡 Ujumbe wa ndoto hii

Ndoto haimaanishi jambo baya litakalotokea.

Ni kioo cha ndani kinachoonyesha majuto, hofu, na upendo ambao bado upo.

Kisaikolojia, ni wito wa kufanya mabadiliko ya tabia, mawasiliano, na kujitafakari — ili usipoteze tena kile unachokithamini.

---

🕊️ Ushauri wa kihisia na kiroho

1. Kubali makosa yako — si udhaifu, bali ni mwanzo wa uponyaji.

2. Omba msamaha (ikiwa bado inawezekana, hata kwa njia ya ujumbe wa amani).

3. Fanya mabadiliko ya kitabia — usitumie nguvu tena katika migogoro; badala yake, eleza hisia zako kwa maneno.

4. Tafuta ushauri wa ndoa au kiroho kama bado unampenda na ungependa kujenga upya.

---

Nikitumia tafsiri ya kisaikolojia ya Carl Jung na Freud pamoja na mitazamo ya kitamaduni ya Kiafrika, hii ndoto ni ishara ya nafsi inayopigana kurejesha amani na upendo uliopotea.
Kwa maneno mengine, moyo wake haujatulia kwa kutengana.
 
Hii ndoto nimeiota saa nane usiku na usingizi ukayeyuka kabisa

Ni mwezi mmoja sasa unaishia toka ameenda kwao mpaka sasa hajarudi

Kisa cha kutorudi ni kwasababu wakati anaondoka nilimwambia asiende hivo nikakuta ameenda kwao kulikuwa na sherehe.

Lengo ilikuwa sio kumzuia lengo nilikuwa tu namzingua ili aende mchana maana kwao sio mbali hivo.

Sasa mm nikawa sijapenda yeye kuwaamsha watoto asubuhi maana sherehe ilikuwa ni siku inayofuata.

Basi tukazinguana kidogo nikampiga kofi la uso sababu ya kuamsha watoto kwa nguvu.

Nikamwambia kama anaenda aende ila asijekurudi tena.

Basi nikaingia zangu job nikarudi jioni nikakuta kasepa zake kachukua hela tuliyokuwa tumeitunza mahali kama 50 hivi.

Basi mm nikamkumbusha tu asijekuwahi kurudi.

Basi baada ya siku kadhaa akaniomba nimtumie nauli arudi.

Mm nimemwambia nauli situmi aje tu kwa nauli yake ila pia akija lazima nitamuadhibu. Kwa kukaidi amri yangu.

Basi tuishie hapo twende kwenye ndoto.

Nilikuwa na mtoto wangu wa kike mdogo hivi tupo kama pembezoni mwa mto wa maji yanayotembea sasa mtoto alikuwa anacheza uchi kwenye kina kifupi cha maji yanayotembea kwa kasi, ghafla nikamuona akijitupia kina kirefu na kuzama nilikuwa umbali kidogo kama mita 10 hivi basi ikabidi nikimbie na kwenda kuwahi kwa mbele kidogo nikapeleka mikono kama kuotea tu, ila nikafanikiwa kumshika nikamnyanya juu akawa anatapika yale maji na kulia. Basi nikatoka nae kwenye maji na kuelekea nyumbani.

Na usingizi ukakata ghafla.

Je hii ndoto inamaana gani?

Sipendi kutengana na mke wangu ila naona kama hakuna namna nyingine ugomvi ni umekuwa sehemu ya maisha yetu kila siku.
Ujinga wa mwafrika, bado hujaelimika mchawi wewe.
 
Hapo tatizo ni wewe, acha kukurupuka navmrudishe mkeo kisha tengeneza mahusiano upya
 
Huyo mtoto wako wa kike katika hiyo ndoto ni MKEO. Mtoto amebeba uhusika wa mama yake.

Kuwa mwanaume makini si lazima uwe mkali. Mwanaume amebeba heshima kuu ya Kiungu ndani yake kuliko mwanaume. Mwanaume ni kiongozi, ni sura/mfano wa Mungu.

Mungu ni mpole, mvumilivu, husamehe na wa hekima. Vaa uhusika wake, kuwa mpole, mvumilie, samehe na uishi nae kwa hekima/akili huku ukijua mwanamke ni chombo dhaifu kisicho na nguvu ila alipopungukiwa na nguvu, wewe mume wake ndio mtosherevu wa hiyo nguvu kwake.
 
Wewe ni mwanaume dhaifu sana,
Mkeo kaondoka bila ruhusa yako,kamaliza kufanya yake huko anataka nauli arudi na wewe unamwambia arudi kwa nauli yake! jibu lako lina ashiria kua unataka huyo Mwanamke arudi,nae amejua kua unamtaka arudi,

Umeshindwa kusimamia maneno yako kua asirudi kwa kuondoka bila ruhusa yako? hiyo msg yake ya kuomba nauli hukutakiwa hata kuijibu,hiyo ingemtia wasiwasi sana na kumuumiza,angetafuta njia yeyote ile kisha akarudi fasta.
 
Hii ndoto nimeiota saa nane usiku na usingizi ukayeyuka kabisa

Ni mwezi mmoja sasa unaishia toka ameenda kwao mpaka sasa hajarudi

Kisa cha kutorudi ni kwasababu wakati anaondoka nilimwambia asiende hivo nikakuta ameenda kwao kulikuwa na sherehe.

Lengo ilikuwa sio kumzuia lengo nilikuwa tu namzingua ili aende mchana maana kwao sio mbali hivo.

Sasa mm nikawa sijapenda yeye kuwaamsha watoto asubuhi maana sherehe ilikuwa ni siku inayofuata.

Basi tukazinguana kidogo nikampiga kofi la uso sababu ya kuamsha watoto kwa nguvu.

Nikamwambia kama anaenda aende ila asijekurudi tena.

Basi nikaingia zangu job nikarudi jioni nikakuta kasepa zake kachukua hela tuliyokuwa tumeitunza mahali kama 50 hivi.

Basi mm nikamkumbusha tu asijekuwahi kurudi.

Basi baada ya siku kadhaa akaniomba nimtumie nauli arudi.

Mm nimemwambia nauli situmi aje tu kwa nauli yake ila pia akija lazima nitamuadhibu. Kwa kukaidi amri yangu.

Basi tuishie hapo twende kwenye ndoto.

Nilikuwa na mtoto wangu wa kike mdogo hivi tupo kama pembezoni mwa mto wa maji yanayotembea sasa mtoto alikuwa anacheza uchi kwenye kina kifupi cha maji yanayotembea kwa kasi, ghafla nikamuona akijitupia kina kirefu na kuzama nilikuwa umbali kidogo kama mita 10 hivi basi ikabidi nikimbie na kwenda kuwahi kwa mbele kidogo nikapeleka mikono kama kuotea tu, ila nikafanikiwa kumshika nikamnyanya juu akawa anatapika yale maji na kulia. Basi nikatoka nae kwenye maji na kuelekea nyumbani.

Na usingizi ukakata ghafla.

Je hii ndoto inamaana gani?

Sipendi kutengana na mke wangu ila naona kama hakuna namna nyingine ugomvi ni umekuwa sehemu ya maisha yetu kila siku.
Hakuna kitu kinaniumiza na kunisikitisha hususan ni wanaume kutreat wanawake kama watoto wadogo. Mwanamke unayelala naye hata kama unamzidi miaka 50 ni mkubwa mwenzako. Kejeri kama 'nikampiga kofi la uso' zinaonesha dharau. Mwanaume ukitaka kumheshimu mwanamke, kumbuka siku ukiwa na upwiru unavyohangaisha. Acheni hizo, watoto ndiyo wanapigwa si watu wazima kama wewe.
 
Hii ndoto nimeiota saa nane usiku na usingizi ukayeyuka kabisa

Ni mwezi mmoja sasa unaishia toka ameenda kwao mpaka sasa hajarudi

Kisa cha kutorudi ni kwasababu wakati anaondoka nilimwambia asiende hivo nikakuta ameenda kwao kulikuwa na sherehe.

Lengo ilikuwa sio kumzuia lengo nilikuwa tu namzingua ili aende mchana maana kwao sio mbali hivo.

Sasa mm nikawa sijapenda yeye kuwaamsha watoto asubuhi maana sherehe ilikuwa ni siku inayofuata.

Basi tukazinguana kidogo nikampiga kofi la uso sababu ya kuamsha watoto kwa nguvu.

Nikamwambia kama anaenda aende ila asijekurudi tena.

Basi nikaingia zangu job nikarudi jioni nikakuta kasepa zake kachukua hela tuliyokuwa tumeitunza mahali kama 50 hivi.

Basi mm nikamkumbusha tu asijekuwahi kurudi.

Basi baada ya siku kadhaa akaniomba nimtumie nauli arudi.

Mm nimemwambia nauli situmi aje tu kwa nauli yake ila pia akija lazima nitamuadhibu. Kwa kukaidi amri yangu.

Basi tuishie hapo twende kwenye ndoto.

Nilikuwa na mtoto wangu wa kike mdogo hivi tupo kama pembezoni mwa mto wa maji yanayotembea sasa mtoto alikuwa anacheza uchi kwenye kina kifupi cha maji yanayotembea kwa kasi, ghafla nikamuona akijitupia kina kirefu na kuzama nilikuwa umbali kidogo kama mita 10 hivi basi ikabidi nikimbie na kwenda kuwahi kwa mbele kidogo nikapeleka mikono kama kuotea tu, ila nikafanikiwa kumshika nikamnyanya juu akawa anatapika yale maji na kulia. Basi nikatoka nae kwenye maji na kuelekea nyumbani.

Na usingizi ukakata ghafla.

Je hii ndoto inamaana gani?

Sipendi kutengana na mke wangu ila naona kama hakuna namna nyingine ugomvi ni umekuwa sehemu ya maisha yetu kila siku.
Hivi wanaume wenzangu huwa mnapata wapi ujasiri wa kuwapiga wake zenu! Sasa ishu ya kuwaamsha tu watoto asubuhi ili aende nao nyumbani kwa wazazi wake kwenye sherehe, ndiyo umpige kofi!

Na bado anakuomba umtumie nauli, unamuambia atafute mwenyewe nauli! Na akiwahi kuja utamuadhibu! Huyo ni mke wako kweli? Yaani rafiki, mwenzi, na mpenzi wa maisha yako! Aisee mnazingua.

Mimi katika umri wangu huu, sijawahi hata kumuoneshea mke wangu kidole. Na maisha yanasonga. Kukoseana kupo, kununiana kupo! Lakini siyo kupigana makofi au kutoana ngeu. Hayo siyo maisha aisee. Tuwapende wake zetu.
 
Kuota kawaida.

Unaweza kuta hiyo ndoto haina maana yoyote
 
Back
Top Bottom