Baada ya kutoa nilichojaaliwa kwa mtoto nimepata amani ya moyo

Baada ya kutoa nilichojaaliwa kwa mtoto nimepata amani ya moyo

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
5,715
Reaction score
13,739
Kuna muda nilikuwa nikikaa peke yangu najihisi huzuni sana, na nilikuwa sijui huzuni inatoka wapi. Au kuna muda mwingine nikiwa peke yangu najihisi kutaka kulia, kuna mwanamke miaka miwili iliyopita nilikuwa nae katika mahusiano.

Baada ya muda akawa amepata ujauzito na alikomaa kwelikweli kuwa huo ujauzito ni wa kwangu, mimi nilikataa ule ujauzito kwa sababu kwa tabia yake yule mwanamke alikuwa ni kiruka njia japo huduma ndogo ndogo nilikuwa natoa tu kama msaada baada ya muda yule mwanamke alienda kwao huko kanda ya ziwa kujifungua na mawasiliano yakawa yamekatika.

Kuna siku akanipigia huku akilalamika kuwa nimekataa kutoa matunzo kwa mtoto basi mtoto anamgawia mwanaume mwingine, toka kipindi hicho moyo wangu ulikuwa unakosa amani sana. Sasa juzi nimekwenda kanda ya ziwa na nikafika maeneo yale na kumuona yule mwanamke na kumpatia chochote nilichonacho na pia nimemfanyia shopping mtoto japo ukimtizama hanifanani hata kidogo.
 
Hii yote ni kwa sababu ya familia tunazotoka.....kiukweli familia zetu zimejaa watu wenye roho mbaya sana na hasa pale kama baba alioa mke zaidi ya mmoja
 
Back
Top Bottom