LGE2024 Baada ya kuvuga uchaguzi, Mtendaji wa Kata akimbizwa kwa kutumia gari la Serikali, Mwalimu ambako masundukù ya kura za wizi yalifichwa, atoroka

LGE2024 Baada ya kuvuga uchaguzi, Mtendaji wa Kata akimbizwa kwa kutumia gari la Serikali, Mwalimu ambako masundukù ya kura za wizi yalifichwa, atoroka

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,362
Reaction score
48,879
Huko Kata ya Ruhuhu, wilayani Ludewa, mkoani Njombe, karatasi za kupigia kura hazikuwa na majina ya wagombea kupitia CHADEMA.

Wananchi waliweza kuzuia uchaguzi usifanyike. Mtendaji kata bwana Yusufu Lukuwi (mtoto wa Kidulile), alipoona wananchi wamechachamaa, alitoa taarifa Wilayani, na msimamizi wa uchaguzi akatuma gari, wakaondoka naye, haijulikani wameenda naye wapi.

Wakati wananchi wakidhibiti kuhakikisha hakuna box la kura linaingizwa kituoni, zilipatikana taarifa kuwa kuna maboksi yenye kura za wagombea wa CCM, yamefichwa nyumbani kwa mwalimu wa shule ya msingi Ngelenge, bwana Kayombo. Wananchi wakaamua kwenda kuyachukua maboksi hayo, lakini walipofika nyumbani kwa mwalimu huyo, tayari alikuwa ametoroka, na mpaka muda wa saa 1 usiku, alikuwa hajapatikana.

Wananchi wa Ruhuhu wamejiapiza kuwa mtendaji na huyo mwalimu, kamwe wasionekane kijijini pao.

Mpaka muda wa kupiga kura unaisha, hakuna aliyepiga kura.

Kwa uchaguzi huu, hakika Mchengerwa amevunja rekodi. Na hawa viongozi wa kupatikana kwa kupora haki za wananchi, watakuwa na wakati mgumu sana katika uongozi wao. CCM wasidhani wamewasaidia jwa huu uharamia, bali wamewapa majuto, na sia ajabu, wengi wataachia njiani.

UPDATE:
Maeneo ambayo CHADEMA waluweka wagombea, majina yao yakaenguliwa, kisha rufaa zao zikashinda, majina yakawekwa kwenye karatasi za kupigia kura, na uchaguzi kukamilika, matokeo ya mwanzo kutangazwa ni kijiji cha Lupingu: CHADEMA imeshinda:

Kijiji Cha LUPINGU imeshinda CHADEMA, kitongoji cha LUPINGU imeshinda CHADEMA kitongoji cha LUKUYUSI bado Matokeo yana ukakasi, kuna vurugu kubwa sanaaaa huko.

Kijiji Cha LUPINGU ina vitongoji 3 mpaka sasa tumeshinda kijiji na kitongoji 1. Kitongoji cha ISANGA wameshinda CCM.

Taarifa Imetolewa na mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Njombe, na Lupingu ndiko kijiji anachotokea huyu mwenyekiti.
 
Wananchi wa Ruhuhu wamejiapiza kuwa mtendaji na huyo mwalimu, kamwe wasionekane kijijini pao.
Taratibu mambo yatabadilika tu.
Muda si mrefu kwenye chaguzi zijazo, hali itakuwa kama hivyo maeneo mengi nchini.

Duniani kote hakuna utawala wa kidikteta uliowahi kuwashinda wananchi waliochoka
 
Taratibu mambo yatabadilika tu.
Muda si mrefu kwenye chaguzi zijazo, hali itakuwa kama hivyo maeneo mengi nchini.

Duniani kote hakuna utawala wa kidikteta uliowahi kuwashinda wananchi waliochoka

Wamenyimwa ufahamu na maarifa. Wanazidi kuwapandikiza hasira na chuki wananchi, dhidi yao. Watakuja kuondolewa kwa aibu kubwa.

Hakuna uovu usio na mwisho, kwani asili ya mwanadamu, ni kuuchukia uovu.
 
Wamenyimwa ufahamu na maarifa. Wanazidi kuwapandikiza hasira na chuki wananchi, dhidi yao. Watakuja kuondolewa kwa aibu kubwa.

Hakuna uovu usio na mwisho, kwani asili ya mwanadamu, ni kuuchukia uovu.
Actually maarifa hayo wamepewa japo wamechelewa. Maybe kizazi cha waliopo hawatoweza, kinachokuja ni shida
 
Back
Top Bottom