Baada ya kuzikwa kaburini, binadamu huchukua muda gani kuanza kuoza?

Baada ya kuzikwa kaburini, binadamu huchukua muda gani kuanza kuoza?

Ndugu zangu , hongereni kwa weekend.


Binadamu akishazikwa kaburini, inamchukua muda kuanza kuoza na hatimae kupoteza sura yake ya awali ?

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
Inategemea kama mwili ulifanyiwa uhifadhi wowote. Wengine kama ilichukua siku 3 au 4 kabla ya mazishi, tayari mwili unaanza kuoza. Wengine waliofanyiwa embalming, hata mwezi au miaka unakaa, kwani unakuwa umekaushwa hivi.
 
Ki-Biolojia, decomposition husababishwa na bacteria. Sasa bacteria kuishi mahala fulani hutegemea vitu vingi kuwepo au kutokuwepo mahala husika, kama aeration, water, soil texture and so on. Kwa hiyo basi, mtu kuoza inategemea na mahali alipozikwa. Miaka ya nyuma kidogo, Tanzania iliamua kurejesha miili ya mashujaa wake waliokuwa wamezikwa Msumbiji miaka mingi iliyopita, lakini miili hiyo haikuharika, mingine ilionekana kama imezikwa jana tu.
Miili hiyo iliwekwa wazi? Uliionaje?
 
Ndugu zangu , hongereni kwa weekend.


Binadamu akishazikwa kaburini, inamchukua muda kuanza kuoza na hatimae kupoteza sura yake ya awali ?

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
Tendo la kuoza huanza pale mtu anapokata roho na akifika kaburini ni mwendelezo tu ambao chini ya masaa 72 sura hubadilika kabisa lakini pia inategemea alikaa muda gani kabla ya kuzikwa
 
Haya mambo magumu sana mwendazake alianza kuharibika akiwa hapahapa , walikua wanambadilishia majeneza tu, yaani kifo ukisikie tu, hapa aulizwe mwendazake maana yeye sasa ni mkuu wa malaika huko alipo
 
Joto + mgandamizo, nadhani hata siku mbili hutoboi, unavimba, tumbo lina pasuka, kila kitu kinamwagika sasa ndo muda wa wadudu kufanya yao, yaani wanakufumua fumua hovyo hovyo, halaf mbeleni huko sijui.
Wanaozikwa dareslaam kwa vikaburi vyao vile vinavyochimbwa futi 3 tu kwenda chini lazima waanze kuoza kesho yake tu
 
Kuoza unaanza masaa kadhaa tu baada ya kufa ndo maana unawekwa kwenye freezer na kwa waislam ukifa alfajiri saa 7 mchana unazikwa
 
Daaaa kweli ajira hakuna!?? Unawezaje kuwaza vitu kama hivi!?? Mbona kazi zipo tuu zakufsnya!??
 
Back
Top Bottom