Jifunzeni kutochanganya mambo ya maendeleo na siasa za nchi, hii video mlikosea kuchomekea humo mambo ya siasa, mara mnamponda Membe, mara ununuzi wa urais Dodoma, yaani hata kitu kizuri kinaishia kupondwa. Mjifunze tunavyotoa taarifa za mazuri ya Kenya, humo hatuchanganyi siasa, tunaiweka kizalendo ambapo inaishia kusifiwa na Wakenya wote wenye mitazamo tofauti ya kisiasa.
Makada wa CCM kwenye mitandao mnaharibu nchi yenu mkiona kwa macho, mnafaa mpate darasa jinsi gani ya kuunganisha nchi, hebu ona hata mpira juzi kule Misri, nilishangaa sana nchi yote mligawanyika kati, yaani mechi baina ya mataifa hufahamika kama njia ya kuwaleta wananchi wote pamoja na kuwa kimoja, lakini MaCCm mliiteka timu na kusababisha baadhi ya Watanzania kushabikia kushindwa kwa timu ya taifa, hivi kweli mumepofushwa kiasi hamuoni mnakoipeleka nchi, hamna kizuri ambacho hamkitii uchafu.
Hili la ndege mngeitangaza yenyewe kama yenyewe na kusifia nchi yenu kuwa ya kwanza kuipokea, lakini video imejaa tambo za kisiasa.