Baada ya Liverpool kutolewa jana, leo ni zamu ya Real Madrid kuaga mashindano

Baada ya Liverpool kutolewa jana, leo ni zamu ya Real Madrid kuaga mashindano

Real anajua namna ya kuzicheza hizi mechi. Anaweza kukupa dkk 75 utawale ila akatumia dkk 15 kuimaliza mechi. Leo mtaitawala mechi ila real anasonga mbele.
 
Mim nataka Barcelona tuchukue
Barca mpinzani mkubwa wa kumhofia alikuwa ni Liverpool na Madrid, Atletico na Real. Sasa leo anaondoka mwingine ambaye ni tishio, hii ndo tunabeba. Leo natamani Atletico apite kuliko Real.
 
Hizi habari za madrid kwenye Knockout blah blah blah

Kwani madrid kashatolewa mara ngapi kwenye hizihizi knockouts mnazomsifia?

Au ndiyo kujizima data.
Man City fans hamuwezi kuipenda Madrid.
 
Sio rahisi kiasi hicho aisee....ingawa pale Atletico ni magumu sana kwa Real Madrid
 
Real anajua namna ya kuzicheza hizi mechi. Anaweza kukupa dkk 75 utawale ila akatumia dkk 15 kuimaliza mechi. Leo mtaitawala mechi ila real anasonga mbele.
Umeandika as if huwa wanafanya hivyo purposefully.

Kwamba wanaamua tumalize game ndani ya dakika 15 za mwisho.
 
Sijakuambia dkk 15 za mwisho, anaweza kutumia dkk 15 kuimaliza mechi. Unakumbuka fainali iliyopita Dortmund alicheza vizur sana lakin real alitumia dkk chache kuimaliza ile mechi. Zile dkk chache ambazo real wanacheza vizur ndizo wanatumia kuimaliza mechi tofaut na timu zingine.
 
Jana kulikuwa na mechi nzuri sana kati ya Liverpool dhidi ya PSG katika usiku wa Ulaya.

Mechi ikaisha kwa PSG kushinda kwa matuta huku wakiubonda sana mpira mwingi.

Ikawashtua mashabiki wengi wa soka ambao hawakutarajia kama Liverpool ingeondolewa hasa katika uwanja wake wa nyumbani.

Leo ni zamu ya kuondolewa mashindanoni kwa mabingwa wa kihistoria, Real Madrid.

Leo pale katika dimba la Wanda Metropolitano kuna bonge la mbungi.

Atletico Madrid watakuwa wanawakakaribisha majirani zao Real Madrid.

Naona kabisa leo Diego Simione akiiongoza Atletico kwenda hatua ya robo fainali. Tutakuwepo
Madrid hata iwe mbovu kiasi gani ikishafika 16 bora kwenye UEFA kila mchezaji anacheza kama Messi. Atletico Itafumuliwa mpaka wajute kushiriki UEFA msimu huu
 
Atletico wana timu nzuri ila leo wanatoka tena ndani ya dakika 90!!!
 
Nikikumbuka namna Mohamed salah alivyo teguliwa mfupa maeneo ya juu ya kifua na beki matata sergio nachoka kabisa
2018 hiyo

Nakumbuka goli la Benzema baada ya kipa wa Liver kuanzisha mpira uliomgonga Benzema.
 
Back
Top Bottom