Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!

Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!

upo sawa kabsa mkuu, saiv DSM ipo salama kabisa chini ya mkuu wetu wa mkoa MHE PAUL MAKONDA.
hawafurukuti mkuu, kwao wanajua matusi tu na kulalamika na kazi yao kubwa ni kupokea MAKAPI NA KUANZA KUYASAFISHA.
 
Nimependa

Naona umewachoma mikuki wengi wao, wengine wamepita kimya kimya ha ha ha haaaaaaaa

Kweli ukweli unaumiza watu wavivu, wa ngada, wa wivu, wasio na mbele wala nyuma eeeeeeeeh

Inafurahisha mtu kusoma uzi kama huu na kukuta ni walewale yaani ID unaiona unasma huyo kapigwa eeeeeh

Na bado, mtazidi kuisoma namba na kunyooka.

Kingine nyie nyie jana mlikuwa namba moja kuongelea alichoongea kwa wivu na kujaribu kupindisha ila ikawa imeshatoka hiyo

Fans wa jembe la Taifa

Eeeeeeh, hamlali tangu jana sindano imewachoma haswa...mtanyooka tu
Hamna lingine bali kuendelea kulinda ID zenu msishushuane humu, mnatamani mngekuwa kama akina mie eeeeeh

Makonda oyeeeeeeeeeeeeee
 
Kwa maoni yangu Makonda atatufaa sana kumpokea Magufuli, maana kiukweli huyu Jamaa atatufaa sana kwa sababu ana uthubutu mkubwa zaidi kuliko hata Magufuli. Makonda akimpokea kiukweli kabisa Tanzania itanyooka.

Makonda konyesha uwezo wa uthubutu, jee mnalionaje hili la kwanini asiwe Makonda kumpokea Magufuli?.

Kwa kwa wale mashabiki wa upinzani mtanisamehe bure, kwenye urais upinzani ni bado sana.

Paskali.
 
Makonda alete vyeti maana urahisi sio KKK.....ana kesi jinai pale alipo....na wana fisiem hawawezi kamwe kumpitisha tena mfitini na mzandiki...huyo mtoto hafai hata!!! Angekuwa binti amezalishwa watoto 4 kila mmoja baba yake!!! Sema tu..........haishiki!!!
 
Makonda ana kipi special kiasi cha kumuona anafaa?
anza na mwaka wake mmoja wa ukuu wa mkoa ni innovation idea gan iliyowasaidia wananchi zaidi ya siasa za muda mfupi?

sio kwa makonda tu, fanya kwa viongozi wote waliopita na waliopo

ndo utagundua chuki mbaya sana
 
Kama wewe si mshabiki wa upinzani basi ni shabiki wa CCM, na kama ni hivyo basi ingeshangaza sana kama na wewe ungeona kwamba upinzani unafaa kutoa Rais iwe 2020 ama hiyo 2025. Mbali na U-CCM wako lakini pia kwa Makonda na Magufuli umepata sababu za ziada za kuwashabikia na siku hizi huoni haya kwa hilo!

Kama mpaka mwaka 2025 unaona ni CCM tu ndiyo inafaa kutoa Rais basi kuna tatizo, na tatizo la ziada ni pale unapoona anayefaa kugombea huo urais wenyewe. Hili na upinzani kuwa bado sana kwenye nafasi ya Urais ni kwa vigezo vya sayansi ya siasa ama ni kwa mtindo wenu wa kutumia kila zana haramu kuhalalisha ushindi wenu?

Toa sababu ni kwa nini Upinzani haujawa tayari kutoa Rais?
Katiba ya nchi bado haitoi mwanya kwa mpinzani kutawala.. haitoi

Huu ni ukweli mchungu, Mbowe.. sumaye.. lowassa na wote wanajua hili
 
You are Kidding Right? Au Kwa Vile Umesikia Kilimanjaro Kiti cha RC Kiko wazi? Unajua Pascal Mimi Ningelikuwa nataka Mara tu ya Uchaguzi Ungekuta Ni DC au RC lakini for what? Uhuru haki na Demokrasia ni Muhimu kuliko vyote. Ndio Vinavyozaa maendeleo ya Kudumu na Ustawi wa Taifa. There is No SUBSTITUTE for FREEDOM and JUSTICE, Ndio Maana Jomo Kenyatta aliyekuwa na Maisha Mazuri Uingereza akarudi kupigania uhuru hata akafungwa Kama Gaidi, Ndio Maana Nyerere aliyekuwa Na Masters ya Ualimu wa Uchumi na Historia akaacha kazi Akakubali kutukanwa na Kudharauliwa KudaiUhuru, Ndio Maana Dr. Mondulane aliyekuwa Mkufunzi Marekani akarudi na akajitoa mpaka Kifo akidai haki na Uhuru wa Mozambique! Ndio Maana Mandela aliyekuwa Mwanasheria Maarufu akaamua Kuyatoa sadaka maisha yake na ya kukaa na familia yake na ya Mke wake aliyekuwa Mrembo sana Winnie, Ili wengi wawe na Uhuru!

Mandela_Winnie.jpg

Angalia Maisha aliyoyatoa sadaka!

Ndio Maana Aliyekuwa Mwanafunzi wa Udaktari Steven Biko aliamua Kukatiza Masomo yake ili awaunganishe Watu wake Kupata sio, kidonge cha Panadol au sifa ya kutazama kindege cha Bombardier kikiruka angani bali Uhuru! Na Demokrasia. Akajitoa Mpaka Kifo! Walimponda Kichwa na Kumwaga Ubongo wake bila sababu! Mtu aliyekuwa wa amani, hakuwatisha kwa Mitutu kama walivyomtisha wao! Lakini kwa Maneno yake ya KWELI, "Binadamu wote ni Ndugu" wakamuua! Lakini haya Maneno yanaishi Bado. Je Ndugu yako akiachishwa kazi akiwa na Miaka 40, Utamnyima Mafao yake, Watoto wake wakose shule wafe njaa umwambie asubiri miaka 25 atakapofikia miaka 65! Huku fedha zake ukijengea madaraja na Kununua Vindege ili tu baada ya Miaka mitano useme oneni mimi oneni mimi?

steve-bikos-body-in-the-ginsberg-section-of-king-williams-town-1977-AC56KD.jpg


steve-biko-300x300.jpg


Kuna Mifano Mingi naweza Kukupa, Kuna akina Che, kuna akina Thomas Sankara, Kuna akina Ayende, Kuna akina Sobukwe, Kuna akina Dedan Kimathi, Kuna akina Chris Hani, Kuna akina Walter Sisulu etc.

Magufuli kuna Mambo anayofanya ambayo Ni mazuri au kwa Nia Njema au Kwa Kujitafutia Utukufu Binafsi! Binafsi Anayechukua Uhuru wangu na Haki yangu! Hata angeuza ulimwengu anikabidhi simtaki. Its better to Die Free with smile than to live in fear and Full of tear!

Pascal Magufuli alishakukebehi maana ya Jina Lako! Usitake nimwamini alikuwa Sahihi.
I concur with you Marandu, truth should be told, bitter as they may be!
 
Wanabodi,
Kabla Magufuli hajawa rais wetu, sisi wengine wenu tulijua tangu mwaka 2014 na tukasema humu!.Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Miongoni mwa sifa zilizomuibua Magufuli ni sifa inayoitwa "uthubutu" unreasonably ambayo wengine huita ni udikiteta. Yaani kuachana na mambo ya kufuata sheria, taratibu na kanuni, ndiyo yametufikisha hapa, hawa viongozi wenye "uthubutu" hawahitaji kujua sheria, taratibu na kanuni, zinataka nini, bali hufanya lile linalowezekana,

Ndio maana tukasema humu, japo Magufuli kweli ni dikiteta, Tanzania mahali ilipofika ilimhitaji mtu kama Magufuli na Mwenyeenzi Mungu akaisikia sala yetu, akatupatia Magufuli!.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

Tukija kwa Makonda, muda mfupi baada ya kuteuliwa DC wa Kinondoni, akaonyesha uwezo, hivyo kama ilivyokuwa kwa Magufuli, mwaka 2014 tulisema ni Magufuli, na mwaka 2015 kweli akawa yeye. Vivyo hivyo kwa Makonda akiwa DC, akina sisi tukasema hivi Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
Na kweli haukupita muda akawa!.

Hivyo kwa hii kazi nzuri yote anayoifanya Magufuli, atakapoondoka ile 2025, kama hatamuachia nchi mtu mwenye kufuata nyayo zake, hii kazi nzuri yote ya Magufuli itakuwa ni kazi bure! . Hivyo nimeshauri Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Kwa vile katiba sio Msahafu, 2025 tuibadili katiba Magufuli aendelee indefinitely kama Mugabe, mpaka atakapo choka kabisa na kuwa hawezi tena kwa incapacitation, au tumsubirie Mungu, au Tanzania sasa na sisi tuanze mtindo wa spotting na headhunting na kumfantia grooming huyo headhunted.

Kwa maoni yangu Makonda atatufaa sana kumpokea Magufuli, maana kiukweli huyu Jamaa atatufaa sana kwa sababu ana uthubutu mkubwa zaidi kuliko hata Magufuli. Makonda akimpokea kiukweli kabisa Tanzania itanyooka.

Magufuli pamoja na mazuri yake, naye kama binadamu pia ana madhaifu na mapungufu yake, Vivyo hivyo Makonda pia sio malaika naye ana mapungufu yake, moja ya mapungufu makubwa ya Makonda ni inferiority complex inayopelekea ku practice superiority complex na kujikuta ana over do bila kujijua.

Mfano ni jinsi anavyojikomba komba kwa rais Magufuli mpaka kupindukia, karibu kila jambo lazima amtaje Magufuli tena kwa majina yake yote manne na sifa zake zote nne "Rais Wetu Mpendwa Mheshimiwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli" (si mnajua watu wa Kanda yetu kwa kupenda masifa). Makonda lazima afike mahali aonyeshe anaweza kusimama on his own na sio kila wakati kutegemea apron strings za Magufuli.

2025 atatufaa sana. Kwa kuanzia 2020 akalichukue lile jimbo la yule mama pale, au akampumzishe Musukuma na kumshikisha adabu. Atashinda na kupewa moja ya portfolio zenye impact, ili 2025 ampokee Magufuli. Kitendo cha Magufuli kushika nchi, ni dalili ya Tanzania kutenda haki ya wengi wape, yaani wenye haki na uhalali wa kutawala nchi ni wale walio wengi. Baada ya Magufuli aje Makonda, na baada ya hapo kule kule mpaka na wengine wawe ni walio wengi! .

Makonda konyesha uwezo wa uthubutu, jee mnalionaje hili la kwanini asiwe Makonda kumpokea Magufuli?.

Kwa kwa wale mashabiki wa upinzani mtanisamehe bure, kwenye urais upinzani ni bado sana.

Paskali.

Paskali ndugu yangu. Uthubutu bila hekima ni "liability" au "recklessness". Juzi kuna maofisa elimu wamesimamishwa kwa kuomba hela za stationary wakaulizwa kwanini hawatumii posho zao. Alithubutu lakini je ni hekima? Jukumu la stationary ni la nani? Kesho utaambiwa utumie posho yako kutengeneza barabara. Kodi hatulipi kwani? Kodi yetu iko wapi au inanunua vitu bila maridhiano na bunge?

Mimi sio shabiki wa upinzani, ni shabiki wa Tanzania
 
Back
Top Bottom