Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!


Evarist Chahali: Kila mwenye mapenzi ya dhati na Tanzania amwambie Magufuli "unaipeleka nchi kusikofaa"
 
GOD FORBID OOOH
 
Labda kama ni uthubutu wa kutumia vyeti vya watu na majina yao.

yaani watu ambao wanajibu hoja kwa mtutu wa bunduki, watu ambao wako tayari kuua au kupindisha katiba kwa manufaa yao ndio ambao wanapigiwa chapuo, I wonder ndio maana tuko hivi mpaka sasa.
 
Mayalla, usitutapishe
 



Kwani sifa ya urais ni kujua kusoma na kuandika tu?
 

Paskali mbona una matusi ya rejareja,fasihi ulotumia makonda aking'amua atatuma wale wasojulikana,be careful
 
Mayala, Hata kama raisni msukuma ndo mmeamua kutuuua? Kutuonea? Ni dhambi ipi kuwa upinzani? Halafu huu urais wa wasukuma hautaisha? Mmeamua kuvuruga nchi na kutesa watanzania? Haya ni wakati wenu.
Sio kwa sababu ya Usukuma wake, no!, kwa sababu ya uwezo wake.

P.
 
Kwani sifa ya urais ni kujua kusoma na kuandika tu?
No sifa ya urais sio kujua na kuandika, bali ni hizi

1. Uwe na umri kuanzia miaka arobain
2. Uwe na akili timamu
3. Uwe mtanzania wa kuzaliwa
4. Usiwe imewahi kushtakiwa na kuhukumiwa kwa makosa ya jinai, uhaini, uhujumi uchumi
5. Ujue kusoma na kuandika vizuri.
sifa za ziada
at least uwe elimu ya chuo kikuu degree moja na kuendelea

sifa hizi zote tano anazo!.
P
 
Uwe mtekaji, mtesaji na muuaji.


 
Sio kwa sababu ya Usukuma wake, no!, kwa sababu ya uwezo wake.

P.
Uwezo gani kaka? Achana na theory za propaganda za kila siku, kwamba kafanya hivi kafanya vile. Kuendesha, kukuza na kuendeleza nchi ni process ambayo sio ya siku moja ndio maana wenzetu wenye maarifa wana short term plans na long term plan lakini kaka yako anataka yote amalize Leo na ndio maana anashindwa.
Angalia uhalisia wa maisha kwa ujumla, utekelezaji wa Budget ya nchi na mifumo ya Elimu, Afya, Maji nk nayo ikoje.
Hapo hujagusa demokrasia na mahusiano ya kijamii nayo yakoje. Pascal, ukweli ni kuwa haijapata kutokea tangu Uhuru kipindi watu wamechukiana na kutengana kama sasa hivi. Na kwa vile hatuna threat kutoka nje, adui wa nje huwa wakati kama huu ndio wa kuweza kutuchapa kisawa sawa.
Tumwambie basi hata kwa lugha ya Nyumbani kuwa awe msikivu. Kuna watu wanajua mengi, wana maono awasikilize na tuondoe tabia ya chuki. Afanye yake kwa sasa na wengine wataendeleza baadae. Asilazimishe yote kwa pupa atakosa yote.
Pasaka njema.
 
Pasical ni vizuri ukatafuta vitabu vya leadership, hasa contemporary leadership kisha usome transformational leadership na transactional leadership ndipo utowe mapendekezo yako. Pasaka njema
 
Mkuu siku hizi umemkana Mzee wa Nyama choma festival?
 
Magufuli mwenye uthubutu akithubutu kuamrisha kikosi cha wanajeshi kikupige risasi kwa sababu anataka kukupora nyumba, utafurahia uthubutu huo?

Unaelewa kwa nini katiba inasema nchi iongozwe kwa sheria?

Unafahamu kwa nini Magufuli aliapishwa kuilinda katiba?

Unaelewa kwa nini Nyerere alikemea kuvunjwa kwa katiba?
 
Hapa nakubaliana na wewe ili kuleta maendeleo endelevu, lazima kuwe na malengo ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu, yaani short term objectives, medium term objectives na long-term objectives na objectives hizi ziwe SMART Objectives, hili tunalijua na ni ukweli usiofichika ku roll out SGR na Stiglers Gorge ni very ambitious projects, miaka 10 tuu haitoshi kwa implementations, ndio maana sisi waona mbali, tumependekeza Magufuli aongezewa muda apatiwe muda wa kutosha kutimiza malengo yake na katiba ndio kikwazo, tuibadili katiba Maugufuli aendelee, kwani katiba ni nini?, si ni kipande tuu karatasi!.
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
Kwenye hili la demokrasia ni kweli Magufuli ni dikiteta, lakini nchi hii mahali ilipofika, tulimhitaji sana mtu kama Magufuli, tena tulisali na kuomba, na hatimaye Mungu akasikia sala yetu, akatupatia Magufuli, sasa mnalalamika nini?.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!
Tumwambie basi hata kwa lugha ya Nyumbani kuwa awe msikivu. Kuna watu wanajua mengi, wana maono awasikilize na tuondoe tabia ya chuki. Afanye yake kwa sasa na wengine wataendeleza baadae. Asilazimishe yote kwa pupa atakosa yote.
Pasaka njema.
Hili keishaambiwa na sio tuu ameelewa, bali ameishaanza kubadilika, mwanzo aliwaona matajiri kama mashetani, wafanyabiashara kama wapigadili, sasa amebadilika, amewaita na kuwasikiliza, zamu inayofuata ni kwa wanasiasa.

Tusikalie kumlaumu tu Rais Magufuli na Serikali yake wanapofanya mabaya, kwenye mazuri, pia tupongeze!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…